Aboud apinga urais wa kupokezana

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mohammed Aboud Mohammed amesema ni hatari Rais wa Muungano kupatikana kwa zamu katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika Zanzibar. Tamko hilo amelitoa alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar jana.

Alisema kuwa na mfumo wa kutoa urais kwa zamu ni mwanzo wa kuligawa taifa na kuvuruga umoja wa kitaifa wa Tanzania. “Ni hatari kuwa na mfumo wa kutoa urais wa muungano kwa zamu kwa sababu ni mwanzo wa kuligawa taifa vipande,” alisema Waziri Aboud.

Alisema utaratibu unaotumika sasa wa kupata mgombea wa nafasi ya urais kwa kuzingatia sifa na uwezo bila ya kuangalia anatoka upande gani wa muungano ndiyo unafaa kuendelea kutumika kwa sababu umesaidia kuimarisha muungano. Aidha, alisema kwamba mawazo kama hayo hayafai kupewa nafasi kwa sababu ni mwanzo wa kuanza kujenga ubaguzi jambo ambalo kinyume na misingi ya umoja wa kitaifa.

“Kama leo tukisema kuwepo na zamu ya urais wa Muungano baina ya Tanzania bara na Zanzibar badaye wataibuka watu wakitaka kuwe na zamu urais wa Zanzibar baina ya visiwa vya Unguja na Pemba”. alisema. Alisema kutokana na Tanzania kuwa na mikoa mingi kutaibuka watu wakitaka zamu ya kutoa urais katika mikoa yao kama Mwanza, Tabora, Rufiji, Kigoma na kuwa mwanzo wa kuzorotesha umoja wa Watanzania.

Waziri Aboud alisema utaratibu unaotumika sasa ni mzuri kwa sababu umesaidia kupata viongozi wanaofanyakazi bila ya kuzingatia wanatoka upande gani wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Waziri Aboud alisema katika kipindi cha miaka 48 ya Mapinduzi, Muungano umeleta faida kubwa katika kuimarisha amani na umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.

Alisema Muungano umesaidia kujenga misingi ya kiuchumi kutokana na wananchi wa Zanzibar wapatao milioni 1.2 kupata nafasi ya kulitumia soko la biashara la Tanzania bara la watu milioni 40. Hata hivyo alisema wakati huu wa kuelekea mchakato wa mabadiliko ya katiba ya muungano ni vizuri wananchi wakapata nafasi ya kujadili na kuamua wanataka katiba ya aina gani kwa maslahi ya maendeleo ya nchi na vizazi vijavyo. “Upande wangu mie binafsi napendelea mfumo wa serikali mbili ndiyo umesaidia kuimarisha Muungano wetu,” alisema.

source:ippmedia.com

Na hili jibu la Aboud kutoka kwa Mwandishi Mohammed Khelef

Nachukulia kuwa gazeti la leo (8 Januari 2012) na Nipashe, kupitia habari iliyotumwa na mwandishi wake wa Zanzibar (Mwinyi Sadalla), halijamzulia uwongo Mohammed Aboud, kwa kumnukuu akisema “Ni hatari kuwa na mfumo wa kutoa urais wa Muungano kwa zamu kwa sababu ni mwanzo wa kuligawa taifa vipande.”

Na ikiwa hivyo ndivyo, basi tuna haki ya kuijadili kauli yake na ikibidi hata kumjadili yeye mwenyewe mtoa kauli, maana mwisho wa habari hiyo amenukuliwa tena akisema yeye kama yeye, anaona mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili ndio unaofaa.

Mazingira iliyotolewa kauli hii yanaonesha kuwa ni kwa ajili ya kujibu ile ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ya mwishoni mwa mwaka uliopita, ambapo alisema kwamba ni jambo muhimu kwa Katiba Mpya inayokuja kuweka uwiano (mpokezano) wa nafasi ya uraisi wa Muungano baina ya pande zinazouunda Muungano huu, akipigia mfano wa Katiba ya Muungano wa Visiwa vya Comoro.

Mambo matatu ni ya kuyakumbushia hapa: kwanza, Aboud ni waziri katika serikali ya Zanzibar, ambayo inaogozwa na vyama viwili (CUF na CCM), ingawa matakwa ya kikatiba kwa sasa, sera ya CCM ndiyo inayopewa haki ya kuongoza serikali, kwani ndicho chama kilichotoa rais. Aboud ni waziri kutoka CCM. Pili, Aboud ni waziri kwenye ofisi ya makamo wa pili wa rais (kutoka CCM). Tatu, Aboud ni mtu aliyetumikia sehemu kubwa ya uwanasiasa wake akiwa kwenye serikali ya Muungano, sehemu kubwa ya hiyo hiyo sehemu kubwa akiwa amenyanyuliwa kutoka chini kwenda juu bila ya yeye mwenyewe kujituma kwenye umma (hapa nakusudia umma wa Kizanzibari).

Tuko wengi tunaowachukulia wanasiasa wa aina yake kuwa ni Tanganyika-oriented, kwa maana ya kuwa wamejengwa na kukuzwa kuyatumikia matakwa ya Tanganyika, haidhuru matakwa hayo yawe yako dhidi ya Zanzibar. Na mifano iko tele, chungu nzima!

Uhusiano wa mambo hayo matatu na kauli yake hii uko wazi. Kwanza, kimsingi CCM yenyewe (CCM yenyewe ni ya Dodoma) haiipi nafasi Zanzibar kama nchi huru ndani ya Muungano, bali kinyume chake. Miaka 48 ya Muungano huu kuwa kama ulivyo, ambapo Zanzibar imeminywa na kuminywa hadi kubakia majeruhi asiye matumaini, ni matokeo ya CCM Dodoma.

Kwa msingi huo, akiwa kama mwana-CCM wa aina hiyo, kauli hii si ya ajabu wala ya kutulazimisha kuijadili sana. Tunaijadili sasa kwa kuwa kuna mengine ndani yake. Nalo ni hili la pili: ofisi anayoiwakilisha, yaani Makamo wa Pili wa Rais. Kwa kusema hivi, ofisi hiyo inamjibu Makamo wa Kwanza wa Rais, ambaye ndiye aliyetoa hoja hii ya uwiano (mpokezano).

Na kwa hili, Makamo wa Kwanza aliwakilisha maoni ya Wazanzibari walio wengi na, hivyo, ofisi ya makamo wa pili imefanya kinyume chake. Mimi nasimama upande wa Makamo wa Kwanza, nikiamini alikuwa na ni sahihi na naipinga kauli ya ofisi ya Makamo wa Pili, nikiamini haikuwa na si sahihi kwetu Wazanzibari.

Aboud anasema utaratibu wa kupokezana uraisi wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar utaigawa Tanzania, kwa kuwa kuna siku mikoa mingine ya Tanzania itataka uraisi uwe wa kubadilishana kutoka kila mkoa. Nachelea kuuita ujinga, lakini najikusuru kusema kwamba haingii akilini ikiwa waziri kwenye serikali ya Zanzibar, naye anaamini kuwa Zanzibar ni kama mkoa tu mwengine wa Tanzania! Kwamba hoja inayotumiwa na Zanzibar kudai haki yake kwenye Muungano inaweza pia kutumiwa na mikoa mingine, na hivyo bora kuinyamazisha maana mwisho wake utakuwa mchafu-koge!

Mohammed Aboud Mohammed, Zanzibar si mkoa wa Tanzania. Zanzibar, hata kwa katiba uliyoapa, ni moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwanza, Dodoma na Singida hazikuungana pamoja kuunda Tanzania. Kwa ujumla wake, hizo zinaunda sehemu moja tu ya Tanzania, (Tanganyika). Na hili siamini kama ni somo ambalo nilipaswa hapa kulitoa kwako!

Nachelea kusema kwamba kwa viongozi wa serikali wa aina hii waliopo kwenye ofisi ya makamo wa pili wa rais, Zanzibar ina safari refu ya kuienda kabla haki yake haijaheshimiwa ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.

Hakuna siku nyengine yoyote huko mbele Zanzibar itatoa rais wa Jamhuri ya Muungano, maana kwa hakika wanaofanya maamuzi ya nani awe raisi wa Tanzania si Wazanzibari. Unaposema kwamba ulinganishe vigezo vya uwezo tu peke yake, Tanganyika kama ilivyo Zanzibar haina upungufu wa raia wenye uwezo wa kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kigezo hicho pekee kikitumika, mwisho wa siku wanaofanya maamuzi watapiga kura, na walio wengi (ama katika kuwapitisha wagombea kwenye vyama au katika uchaguzi mkuu) watamchagua yule mwenye sifa ya ziada kwao, yaani ukuruba. Huo ndio ukweli!

Lakini kwa nini kauli hii ikaja sas? Sababu moja ni hiyo niliyoitaja, kwamba anajibiwa Makamo wa Kwanza, Maalim Seif. Na kama nilivyoonesha, kwa kuwa kwa hili Maalim Seif aliwakilisha mtazamo wa Wazanzibari tulio wengi, maana yake ni kuwa ofisi ya makamo wa pili inatujibu sisi Wazanzibari kwa wingi na umoja wetu. Inatujibu kwamba kutokea upande wao, tusitarajie chochote katika Katiba Mpya inayokuja zaidi ya kuzishadidia shemere za Muungano zilizopo na hata ikibidi kuziongeza nyengine.

Sababu nyengine ni uwezekano kwamba Waziri Aboud na wengine katika ofisi wanayoiwakilisha, wanatupa macho yao mwaka 2015, maana ndipo pua zao zinapofikia. Wanaangalia uwezekano wa ama uraisi wa Zanzibar, uraisi wa Muungano au hata umakamo rais wa Muungano?

Yale yale yaliyoizamisha Zanzibar kwa miaka 50 kabla ya Maridhiano yaliyopo sasa, ndiyo haya haya ninayoyazungumzia sasa. safari tunayo, Wazanzibari wenzangu. Lakini tusivunjike moyo. Tutafika.

Wallahi tutafika, walaukarihalmunaafiqun!

Advertisements

18 responses to “Aboud apinga urais wa kupokezana

 1. Hongera ndugu yangu Khelef kwa kumjibu muhishimiwa waziri Aboud; sina hakika waandikia gazeti gani, lakini nakushauri hii makala uitoe katika magazeti mengi uwezavyo na hasa katika Zanzibar leo ili ujumbe uwafikie watu wengi zaidi hapa visiwani.

 2. Ama mimi kwa upande wangu nasema kama maneno wenyewe ndio hayo anayosema waziri mzima huyo ambaye aliteuliwa akiwa ni msomi na anajuwa kwamba Wazanzibar wanalilia nini saa ivi na huyo ndie ambaye akigombania apate Urais mimi bado namuomba arudi darasa la tisa akasome tena angalau ajuwe neno Muungano tu kisha aje achukuwe Uaziri, tulitarajia maneno kama hayo ayaseme angalau Pinda lkn anasema yeye hatahaoni kisisi? Na hayo kama ndio matarajio yake ya kupata Urais wa Zanzibar au Watanzania basi atoe tamaa maana hapo alipo hapawezi.Maöni yangu kuhusu katiba kwanza kuwe na serikali tatu ya Zanzibar, Tanganyika na serikali ya Muungano…

 3. Waziri Mohammed Aboud ana haki ya kutoa mawazo yake, lakini kwa mtazamo wangu Waziri Aboud amefikiri au kuwaza kinyume na hali halisi. Kiukweli ushirikishwaji wa haki baina ya Watanzania Bara na Wazanzibari katika kuiendesha nchi ni jambo la muhimu katika kudumisha Muungano, ikiwa muungano ndio takwa la wananchi wa pande zote mbili. Waziri Aboud anatakiwa kufahamu kuwa chanzo cha watu kuwa na upinzani dhidi ya Muungano ni kule kutoshirikishwa katika maamuzi ya uendeshwaji wa nchi.

  Kama Mzanzibari hana nafasi sawa na Mtanzania Bara katika maamuzi, ama kwa zamu au kwa mgawanyo wa madaraka ni nani atakayezijua shida za Wazanzibari? Na ni vipi Wazanzibari wataweza kuwa ni wenye kujitawala ikiwa nafasi ya utawala haikuwekea misingi ya kuilinda kuwafikia wao? Hili si kwa uraisi tu bali ni kwa nafasi zote za ngazi mbali mbali katika Muungano, iwe ni katika kutunga sheria, kutekeleza sheria au kutawala. 

Je waziri Aboud anafahamu ni kwa nini ikawekwa kwenye katiba kwamba mgombea mwenza lazima atoke upande tofauti na mgombea Uraisi katika Muungano? Sasa je mbona hasemi hilo nalo litaudhoofisha Muungano? Bila ya shaka atakayekuja kutoa dai hili ataonekana kuwa adui wa Muungano, mimi binafsi sioni tofauti ya kuweka mgombea uraisi na mgombea mwenza kutoka pande tofauti za Muungano na kuweka mgombea wa vipindi fulani vya nafasi ya uraisi wa Jamhuri kutoka pande zinazotofautiana kwenye Muungano.

  Je Dodoma ikiamua kwa muda wa miaka 50 ijayo wenye sifa zinazowastahiki kushika uraisi ni Watanzania Bara tu, Waziri aboud unadhani hilo litakuwa sawa? Bila ya shaka kama katiba iko kimnya itakuwa sawa katika mtazamo wa kisheria, lakini je hilo ndilo litakalojenga Muungano? Muungano hautajengwa au kuimarishwa na kauli tata na kuyapinga matakwa ya wananchi kinyemela kama anavyotaka kufanya Waziri Aboud.

  Wazanzibari wanataka kuwa na mamlaka na maamuzi katika uendeshwaji wa nchi yao na si vinginevyo, na mamlaka makubwa juu ya maamuzi ya nchi hii anayo rais wa Muungano. Nina hakika hata Watanzania Bara hawako tayari kuona kwamba Wazanzibari wanachukua nafasi ya uraisi kwa nusu karne ijayo mfululizo. Lakini maskini Waziri Aboud kwake yeye hilo ni sahihi, yuko tayari kuona hakuna Mzanzibari anashika nafasi hiyo hata miilele, kwa mawazo yake huku ndiko kuulinda Muungano.  Waziri Aboud kuendeshwa si kuungana bali ni kutawaliwa, sisi hatukuingia mkataba wa kuwa koloni la Tanganyika sidhani kama ninahitaji kukusomesha somo hili. Tuliingia mkataba wa kuwa nchi mbili zenye mamlaka kamili zitakazounda nchi moja, na mkataba huo bahati nzuri uliruhusu Zanzibar kuendelea kuwa nchi, ndio maana Zanzibar mpaka leo kuna Rais japo kuwa ana mamlaka hafifu mno, sasa Tanzania ni nchi yetu, Wazanzibari na Watanzania Bara, ili iende kwa amani basi lazima kuwe na mlingano wa haki baina ya pande husika, mlingano huo wa haki utajengwa na mambo mengi, mojawapo ni katiba itakayoruhusu ugawanaji sawa wa madaraka, sawa katika ngazi zote na sawa katika vipindi vinavyopishana.

  Siamini kwamba itafika wakati Zanzibar nzima kutakuwa hakuna mtu anayefaa kuwa rais wa Muungano, na kama katiba inaamrisha hivyo basi ni kwa nini iwe ndio msingi wa kudhoofisha Muungano?

 Ukweli ni kwamba iwapo hakuna kipengele kinacholinda mgawanyo wa haki za kutawala iwe kwa zamu au kwa ngazi mbali mbali basi hilo ndilo litakaloleta vurugu pale upande mmoja wa muungano utakapokuwa unatawala upande mwengine na upande mwengine ukajihisi kuonewa au ukawa unaonewa kweli. Hili ndilo linalodhoofisha Muugano sasa hivi, wengi miongoni mwa Wanzanzibari wanauona Muungano kama ukoloni tu.


  
Waziri Aboud, Zanzibar imerudi nyuma kiuchumi, kimaadili, kidini, kielimu na pia katika huduma za jamii kama vile afya. Watanzania Bara wameongoza kwa muda wa miaka ipatayo 40 kati ya miaka 50 ya Muungano, sisemi kwamba kila tuliporudi nyuma basi Rais wa Muugano peke yake ndiye anayestahiki lawama, lakini bila ya shaka tutakubaliana kuwa moja kati ya jukumu la rais wa Muungano ni kuhakikisha kuwa kuna uwiano wa maendeleo baina ya pande mbili za Muungano, ni wakati wa utawala wa Mwinyi tu ndio Wazanzibari tulijihisi kuishi maisha ya “ruhsa”, baada ya kuondoka kwake tukaletewa mambo kama vile TRA na kadhalika ndiyo yaliyotutoa “kapa” na na muuhiska wa kapa au mkapa nadhani tunamjua.

  Waziri Aboud lengo la pendekezo hili ni kuhakikisha kwamba pande mbili za Muungano zinapata haki zinazolingana katika kuitawala nchi hii, lengo na sisi tupate nafasi ya kutoa mchango wetu, na pia tutakapokwama tusinyoosheane vidole kwani tutakuwa tumeshirikiana kujikwamisha, pia Wazanzibari tuna uwezo wa kuindesha nchi kama walivyo Watanzania Bara.

  Wakati umefika wa viongozi wa Zanzibar kuwa wa kweli, kuwa na mawazo yanayowawakilisha wanao waongoza. Muungano hautalindwa kwa hila na ujanja ujanja bali utalindwa na uadilifu, uongozi bora unaofuata matakwa mema ya wananchi. Waziri Aboud muogope mola wako, uongozi ni jukuma na kuna siku utakwenda kuulizwa na siku hiyo hutaweza kusema uongo. 


 4. Huyu katika vibara walotengenezwa bara kwa ajili ya kuizika znz hizi njama za vibaraka na wanafiki jaws salwar salaam zetu wazanzibar hawamtaki na hawampendi kama alivyokua haipendi znz

 5. asalamu alaykum
  ndugu zangu mushishangae huyu ni MLEVI pengine alipokuwa akisema tayari kashaunywa, twiiiiiii.
  tumtizame tu .kwani hafai kabisa na sijui kwa nini kapewa uwaziri huyu.

 6. d
  Education.
  Name Course Started Completed Level
  Michakaini Primary School, Pemba Primary Educatin 1966-01-20 1975-11-20 Certificate
  Kibasila Secondary School, Dar es Salaam Secondary Education 1976-01-16 1977-12-03 Certificate
  MICHAKAINI SECONDARY SCHOOL SECONDARY EDUCATION 1973-01-23 1975-12-12 CERTIFICATE
  INTERNATIONAL CORRESPONSE SCHOOL U.K ENGLISH COURSE 1997-04-20 1997-10-20 CERTIFICATE
  MONTAIGNE SCHOOL OF ENGLISH U.K ENGLISH COURSE 2000-02-20 2000-04-20 CERTIFICATE
  CAMBRIDGE INTERNATIONAL COLLEGE U.K INTERNATIONAL DIPLOMA IN BUSINESS MANAGEMENT AND ADMINISTRATION 2001-04-20 2002-04-21 DIPLOMA
  CAMBRIDGE INTERNATIONAL COLLEGE U.K INTERNATIONAL DIPLOMA IN BUSINESS ECONOMICS AND COMMERCE 2002-06-20 2003-04-15 DIPLOMA
  ST.CLEMENT UNIVERSITY, WEST INDIES PUBLIC ADMINISTRATION 2008-01-20 2008-12-15 MASTER (HONORICAUSA)

  Position From To
  MINISTRY OF EAST AFRICAN COOPERATION DEPUTY MINISTER 2008-06-16 2010-10-31
  MINISTRY OF PUBLIC SAFETY AND SECURITY DEPUTY MINISTER 2006-01-05 2008-06-10
  PARLIAMENT OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MEMBER 2005-11-15 2010-10-30
  MINISTRY OF AGRICULTURE, NATURAL RESOURCES, ENVIRONMENT AND COOPERATIVES, ZANZIBAR MINISTER 2004-05-05 2005-10-30
  MINISTRY OF TRADE, INDUSTRY, MARKERTING AND TOURISM, ZANZIBAR MINISTER 2000-11-11 0000-00-00
  HOUSE OF REPRESENATIVES OF ZANZIBAR MEMBER 2000-11-09 2005-10-31

 7. Ama kwa hakika katika vitu vyema kuuma kuuna wazanzibari wenzetu ndugu zetu wakizungumza maneno pumba regardless kuw ni mawziri au si mawaziri kwa hapa nasema Dk shein amechemka. inabidi afikirie tena suala la uteuzi wake kwa abood.
  maalim na wazalendo wa zanzibar bado kazi tunayo kubwa sana maana hawa hawajui kinachotafutwa ndio kina HR wenyewe ndio kina hawa.

 8. Amani iwe kwenu. hakuna haja ya kumjibu chochote huyu Muheshimiwa Aboud. maana kila kitu anakielewe… bali anashikilia nafasi yake ya kutuvunja moyo na kutudhalilisha waZanzibari. ila M/Mungu ndie atakae mjibu huyu, kama wenzake walivyo kua washa tangulia mbele ya haki. nae ni maiti mtarajiwa. Inshaallah tutamsimamisha Mbele ya haki na kauli zake hizo aje atueleze kwa kina.

  Laana za M/Mungu zimteremkie.

 9. Binafsi nimefurahi sana na ninampongeza Waziri Aboud kwani kauli yake inatoa funzo kwa Wazanzibari kwamba wale tunaowategemea kutupeleka ktk Zanzibar huru ni wanafiki na vibaraka wa Tanganyika. Kilicho mbele yetu ni kutafuta njia mbadala na sio kuwategemea hawa watoto waliokula kiapo pale Dodoma kwamba heri punda afe lkn mzigo wa bwana ufike. Wazanzibari wenzangu, akina Aboud wamo wengi ktk serikali ya mapinduzi hivyo ni jukumu letu sote kwa umoja wetu kuhakikisha tunailinda Zanzibar yetu.

 10. nadhani wakati umefika wazanzibar kuwacha woga ilikupambana na viongozi wanafiki kama walioekwa madarakani kutetea masilahi ya bara hawa ndio vibaraka wenyewe na haistaki kuwepo madarakani lazima wanzanzibar tusimame kwa umoja wetu kuhakikisha viongozi kama hawa wanaondoka madarakani kabla hawajatumaliza ikiwa kiongozi wa znz anathubutu kuita znz mkoa wa Tanganyika wataije znz nchi.lazima tuhakishe kiongozi km huyu anaondoka madarakani kabla muda wake haujesha siohivyo atatuzika.

 11. Huyu ndie aliyeshirikiana na makafiri wenziwe kuinda bendera mpya ya smz. Kwa mujibu wa bendera ya zanzibar ilivyo ZANZIBAR SI NCHI NA WALA SI MKOA BALI NI WIZARA KAMA ZILIVYO WIZARA AU TAASISI ZA SEREKALI YA TANZANIA. Kwani bendera ni kiashirio cha nchi, jumuia, shirika, wizara na taasisi. Maelezo ya kina: hebu angalia bendera ya smz, bendera ya bunge la TZ, bendera ya polisi wa TZ, bendera ya askari wa uhamiaji wa TZ, bendera ya JWTZ, bendera ya askari wa mafunzo wa TZ n’k. Bendera zote hizi zina kibendera kidogo cha jamhuri ya muungano juu yake kikiwa kinaashiria wizara au taasisi za serekali ya TZ ikiwemo zanzibar. Masuali ya kujiuliza: jee kwanini rais wa zanzibar aapishwe bungeni kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum? Kwanini bendera ya zanzibar ifanane na bendera za wizara zote za serekali ya TZ? Kwanini bendera ya zanzibar iingizwe bendera ya muungano ndani yake kama zilivyo bendera zote za wizara za serekali ya TZ? Jee walioiunda bendera mpya ya zanzibar nini wazalendo au wasaliti wa zanzibar? Jee kile kibendera cha muungano katika bendera ya smz kinaashiria nini? Jee kuna nchi duniani iliyoingiza bendera ya jumuiya katika bendera ya nchi yake? Mfano: EAC, EU, AU n’k tukiangalia katika nchi wanachama kuna nchi iliyoingiza bendera ya jumuiya katika bendera ya nchi yake?

 12. HUU NDIO UKWELI KUHUSU ZANZIBAR NI NCHI AU SI NCHI. Naomba taarifa hizi ziwafike wazanzibar wote ili wapate kujua wapi walipofikishwa na viongozi wa smz. Huyu ndie aliyeshirikiana na makafiri wenziwe kuiunda bendera mpya ya smz. Kwa mujibu wa bendera ya zanzibar ilivyo ZANZIBAR SI NCHI NA WALA SI MKOA BALI NI WIZARA KAMA ZILIVYO WIZARA AU TAASISI NYENGINE ZA SEREKALI YA TANZANIA. Kwani bendera ni kiashirio cha nchi, jumuia, shirika, wizara na taasisi. Maelezo ya kina: hebu angalia bendera ya smz, bendera ya bunge la TZ, bendera ya polisi wa TZ, bendera ya askari wa uhamiaji wa TZ, bendera ya JWTZ, bendera ya askari wa mafunzo wa TZ n’k. Bendera zote hizi zina kibendera kidogo cha jamhuri ya muungano juu yake kikiwa kinaashiria wizara au taasisi za serekali ya TZ ikiwemo zanzibar. Masuali ya kujiuliza: jee kwanini rais wa zanzibar aapishwe bungeni kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum? Kwanini bendera ya zanzibar ifanane na bendera za wizara zote za serekali ya TZ? Kwanini bendera ya zanzibar iingizwe bendera ya muungano ndani yake kama zilivyo bendera zote za wizara za serekali ya TZ? Jee walioiunda bendera mpya ya zanzibar ni wazalendo au wasaliti wa zanzibar? Jee kile kibendera cha muungano katika bendera ya smz kinaashiria nini? Jee kwanini PINDA aseme zanzibar si nchi? Jee kuna nchi duniani iliyoingiza bendera ya jumuiya katika bendera ya nchi yake? Mfano: EAC, EU, AU n’k tukiangalia katika nchi wanachama kuna nchi iliyoingiza bendera ya jumuiya katika bendera ya nchi yake? Jawabu wasomi wa zanzibar wanasoma kwa ajili ya kujibu mitihani ya NECTA na vyuo vikuu tu na sio kupata elimu ya kuisaidia zanzibar au itakua wanajua ukweli lakini wanaufumbia macho kwa manufaa yao binafsi.

 13. HUU NDIO UKWELI KUHUSU ZANZIBAR NI NCHI AU SI NCHI. Naomba taarifa hizi ziwafike wazanzibar wote ili wapate kujua wapi walipofikishwa na viongozi wa smz. Huyu MOH’D ABOUD NA MAREHEMU DIRIA ndio walioshirikiana na makafiri wenzao kuiunda bendera mpya ya smz. Kwa mujibu wa bendera ya zanzibar ilivyo ZANZIBAR SI NCHI NA WALA SI MKOA BALI NI WIZARA KAMA ZILIVYO WIZARA AU TAASISI NYENGINE ZA SEREKALI YA TANZANIA. Kwani bendera ni kiashirio cha nchi, jumuia, shirika, wizara na taasisi. Maelezo ya kina: hebu angalia bendera ya smz, bendera ya bunge la TZ, bendera ya polisi wa TZ, bendera ya askari wa uhamiaji wa TZ, bendera ya JWTZ, bendera ya askari wa mafunzo wa TZ n’k. Bendera zote hizi zina kibendera kidogo cha jamhuri ya muungano juu yake kikiwa kinaashiria wizara au taasisi za serekali ya TZ ikiwemo zanzibar. Masuali ya kujiuliza: jee kwanini rais wa zanzibar aapishwe bungeni kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum? Kwanini bendera ya zanzibar ifanane na bendera za wizara zote za serekali ya TZ? Kwanini bendera ya zanzibar iingizwe bendera ya muungano ndani yake kama zilivyo bendera zote za wizara za serekali ya TZ? Jee walioiunda bendera mpya ya zanzibar ni wazalendo au wasaliti wa zanzibar? Jee kile kibendera cha muungano katika bendera ya smz kinaashiria nini? Jee kwanini PINDA aseme zanzibar si nchi? Jee kuna nchi duniani iliyoingiza bendera ya jumuiya katika bendera ya nchi yake? Mfano: EAC, EU, AU n’k tukiangalia katika nchi wanachama kuna nchi iliyoingiza bendera ya jumuiya katika bendera ya nchi yake? Jawabu: wasomi wa zanzibar wanasoma kwa ajili ya kujibu mitihani ya NECTA na vyuo vikuu tu na sio kupata elimu ya kuisaidia zanzibar au itakua wanajua ukweli lakini wanaufumbia macho kwa manufaa yao binafsi.

 14. TANGAZO: KWA MTU YOYOTE ATAKAENILETEA KICHWA CHA MH. MUHAMMEA ABOUD NITAMPATIA Tsh. 50,000000/- hapo hapo. pia, mtu yoyote atakaesababisha kifo cha mfanya kazi wa TRA ZANZIBAR tutamzawadia Tsh.20,000000/- hapo hapo. IF PEACE FUL MEANS FAIL USE FORCE. Bila ya kuwatiaadabu wale wote wanaodumaza maendeleo znz tutaendelea kutawaliwa milele. WANANCHI WA ZANZIBAR MUSIWE NA WASI WASI NITATOA NAMBA ZA SIM ILI UKIFANIKIWA TU KUUA MMOJA KATI YA WAFANYAKAZI WA TRA NA MH. Muhammed Aboud ili upate zawadi yako kwa haraka iwezekanavyo.

 15. TANGAZO: KWA MTU YOYOTE ATAKAENILETEA KICHWA CHA MH. MUHAMMED ABOUD NITAMPATIA Tsh. 50,000000/- hapo hapo. pia, mtu yoyote atakaesababisha kifo cha mfanya kazi wa TRA ZANZIBAR tutamzawadia Tsh.20,000000/- hapo hapo. IF PEACE FUL MEANS FAIL USE FORCE. Bila ya kuwatiaadabu wale wote wanaodumaza maendeleo znz tutaendelea kutawaliwa milele. WANANCHI WA ZANZIBAR MUSIWE NA WASI WASI NITATOA NAMBA ZA SIM ILI UKIFANIKIWA TU KUUA MMOJA KATI YA WAFANYAKAZI WA TRA NA MH. Muhammed Aboud ili upate zawadi yako kwa haraka iwezekanavyo.ZNZ BILA YA KUPATA UHURU KUTOKA TANGANYIKA HAIWEZI KUENDELEA. Bendera ya nchi haiwezi kufanana na bendera za wezara za nchi nyengine. Hii ni zarau kubwa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s