Barua ya watu wa Uzini kwa Rais Kikwete

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete

Kwa mshangao mkubwa sisi watu wa Uzini tukaletewa mtu alie nje mbali sana na jimbo letu kutoka jimbo la Bububu wilaya ya Magharibi na kuhamishiwa kwenye tawi letu na kupewa fomu ya kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi huku wanajimbo halisia wafikao kumi waliojitiokeza kugombea nafasi hii wakiangushwa kwa hila na ghilba na nguvu ya pesa aliyoitumia mwanachama wa CCM mwenzetu, mfanya biashara, bwana Moh’d Raza Daramsy, akisaidiwa na kusimamiwa na viongozi waliokuwa si waaminifu wa chama chetu, ambao wameshindwa kupima upepo wa siasa zetu, na ambao wamesahau historia ya mapinduzi yetu. Viongozi hawa wa ngazi ya jimbo na wilaya wasipoangaliwa kwa umakini mkubwa watakipeleka pabaya chama chetu.

BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI, CCM TAIFA, AMBAE PIA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE

22/12/2011
Mheshimiwa mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi, kwa heshima kubwa na kwa unyenyekevu uliotukuka juu yako tunaiandika barua hii tukiwa na majonzi makubwa juu ya maafa makubwa yaliyosababishwa na mafuriko yatokanayo na mvua kubwa zilizonyesha katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine na kusababisha kupelekea vifo vya watanzania wenzetu na uharibifu mkubwa wa mali na mionombinu. Tunatoa mkono wa pole kwako wewe binafsi kama mkuu wa nchi na kwa familia za wenzetu wote walioathirika na maafa hayo. Tunawaomba watanzania wote tuungane pamoja katika kuwafariji wenzetu hawa kwa hali na mali. Kwa wale ambao roho zao zimepotea, tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, Amin.

Mhe. Rais, uwamuzi wako wa kukatisha ziara yako mkoani Mara na kurejea Dar es Salaam leo ni uthibitisho kamili kuwa wewe ni kiongozi unaewajali wananchi wako. Tunaamini utatoa kauli ambayo itakuwa ni dira kwa watanzania kuweza kukabiliana na janga hili na majanga mengine ya namna hii ili yasiweze kutokea tena nchini mwetu.
Mheshimiwa, baada ya pole zetu hizo tunaomba kwa umakini sana usikilize kilio chetu sisi wanachama wenzako wa CCM, wa jimbo la Uzini liliyopo wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja. Tunachukua fursa hii muhimu kukuandikia barua yetu hii tukijua wewe ni kiongozi wetu makini, mahiri, msikivu, muajibikaji na mfuatiliaji hata kwa habari ambazo wengine huziona kuwa hazina maana, wewe huzipa umuhimu na kuzifanyia kazi. Hii ndio maana chama chetu cha Mapinduzi CCM, kimekuwa kikipendwa na kuzidi kuungwa mkono, na kimekuwa kikipata ushindi wa kishindo kila uchaguzi mkuu unapofika. Hivyo basi, barua yetu hii ya wazi kwako tunaamini utaichukulia kama ni changamoto na sio ukosefu wa adabu.

Mh. Mwenyekiti hivi sasa muda si mrefu tutaingia katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Uzini kwa nafasi ya uwakilishi ili kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na aliyekuwa mwakilishi wetu mpendwa marehemu Maalim Mussa tuliyemchagua kwa kura nyingi za wana CCM. Tunajinasibu na kujilabu kama jimbo hili ni letu tangu asili na dahari na wewe Mheshimiwa hili unalijuwa vizuri kwa sababu wewe ni sehemu yetu na uliishi hapa visiwani na ukakijenga chama cha CCM kilichotokana na Afroshirazi na TANU hapa katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui ukiwa mtendaji.
Mheshimiwa mwenyekiti tulipokea kwa furaha kubwa kalenda ya uchaguzi wa ndani ya chama chetu kwa nia ya kukamilisha taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama chetu ili kupata mgombea atakaesimamisha, kuipigania na kuitetea bendera ya chama chetu katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Uzini.

Sisi wazee wa chama na wenyeji wa jimbo hili tukijua huu ni uchaguzi wa jimbo ambao wanajimbo wenyewe wananaoishi ndani ya jimbo ndio wahusika tofauti na uchaguzi wa Rais kwani Rais hana jimbo maalum, ndio maana tukamchagua Dr Ali Moh’d Shein kutoka Pemba kuwa Rais wetu, kwa kuwa Zanzibar ni jimbo moja kwa nafasi ya urais kama tilivyokuchagua wewe kutoka Bagamoyo kuwa rais bwa Jamhuri kwa kuwa Tanzania ni jimbo moja kwa uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya muungano.

Kwa mshangao mkubwa sisi watu wa Uzini tukaletewa mtu alie nje mbali sana na jimbo letu kutoka jimbo la Bububu wilaya ya Magharibi na kuhamishiwa kwenye tawi letu na kupewa fomu ya kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi huku wanajimbo halisia wafikao kumi waliojitiokeza kugombea nafasi hii wakiangushwa kwa hila na ghilba na nguvu ya pesa aliyoitumia mwanachama wa CCM mwenzetu, mfanya biashara, bwana Moh’d Raza Daramsy, akisaidiwa na kusimamiwa na viongozi waliokuwa si waaminifu wa chama chetu, ambao wameshindwa kupima upepo wa siasa zetu, na ambao wamesahau historia ya mapinduzi yetu. Viongozi hawa wa ngazi ya jimbo na wilaya wasipoangaliwa kwa umakini mkubwa watakipeleka pabaya chama chetu.

Sisi wazee wa Uzini tunajivunia na kujifagharisha mno na Mapinduzi yetu Matukufu ya mwaka 1964 kwani sisi watu wa Uzini tumetoa mchango mkubwa sana kuyafanikisha Mapinduzi hayo. Kambi za kuandaa Mapinduzi ziliundwa katika jimbo la Uzini. Wapangaji na waratibu wa Mapinduzi wengi wao walitoka katika jiombo la Uzini. Hii ndio maana kati ya wanavuguvugu lililoleta Mapinduzi moja wapo ni Mzee Kesi, mwanasiasa maarufu aliyeshitakiwa na serikali ya kikoloni ya wakati huo ili kumkandamiza Maalim Muhsin. Baadae kwa kuthaminiwa aliteliwa kuwa waziri na MBM katika serikali ya mwanzo baada ya Mapinduzi.

Mwengine ni mzee Muhsin bin Ali ambae nae alipewa uwaziri na Karume kwa kuthamini mchango wake mkubwa na mchango wa watu wa Uzini katika Mapinduzi ya 1964. Na wengi wengineo ambapo ndio maana wazee wetu hawa wa jimbo la Uzini wakatuzalia vijana wazalendo wanamapinduzi kama alivyo Mhe Seif Khatib, Mbunge wa jimbo la Uzini ambae ametoa mchango mkubwa katika kuujenga, kuutetea na kulinda Muungano wa Tanzania. Wengine ni waziri wa elimu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Ranadhani Abdalla Shaaban na Mhe Ali Mwinyi Msuko, Afisa mtendaji katika ofisi kuu ya CCM. Na wengine wengi ambao itachukua muda mrefu kuwataja.

Mheshimiwa mwenyekiti, tumeandika haya na kuyafikisha kwako tukitumaini chama chetu bado kina vikao vyake vya juu ambavyo vitafikia maamuzi ya kutuletea mgombea ambae sisi wanachama ndio tutakaokuwa na nafasi kubwa ya kumsimamia ili aweze kushinda. Mhe Mwenyekiti, kwa kutumia vyombo vyako ulivyonavyo ambavyo vina mizizi mirefu vilivyoko ndani ya jimbo tunaamini vitakupa taarifa zilizo sahihi zilizomo ndani ya jimbo hivi sasa baada ya matokeo ya kura ya maoni. Jimbo limegawika na vijiji vimekatika na chama kimetikiswa.

Wako wanaokumbuka kama chama hichi hichi cha CCM kimefanya maamuzi mazito katika chaguzi za nyuma zilizopita kama vile jimbo la Kigamboni pale kilipofuta uteuzi wa Yussuf Manji na pale Kawe kilipofuta uteuzi wa Adam Jee na kwengineko ili kukinusuru chama. Maamuzi kama haya yanahitajika katiaka jimbo la Uzini ili kukinusuru chama hasa kwa jimbo hili la Uzini kwa historia yake, nafasi yake na mchango wake mkubwa kwa chama chetu.

Mheshimiwa mwenyekiti, demokrasia iliyopana ni fujo kwa wale wenye dhamira zao za tamaa na ulwa au kufichia waliyonayo. Kwa mwenendo huu ambao chama chetu kinaendeshwa na baadhi ya watendaji waliokosa uadilifu watatufikisha pahala pabaya jambo ambalo sisi wana CCM wazalendo na wanamapinduzi hatulikubali. Kwani mchelea mwana kulia mwisho hulia yeye. Sauti ya wanyonge ni sauti ya Mungu. Mkoa wa kusini Unguja ni Mkoa ambao hakijatoka kiti chochote kikenda upinzani tokea 1957.

Kwa mwenendo huu sasa ambapo kila mwenye fedha zake nyingi ndie anaefanya maamuzi ya wazalendo ni hatari inayotaka kuepukwa kwa gharama yoyote. Hatuyasemi haya kwa kukusudia ubaguzi sisi ubaguzi hatunao. Lakini jee itakuja kuwa sahihi kama Mkunduchi Haruna Ali Suleiman – Muhindi, kwa Muyuni, Jaku – Muhindi, na kwa Uzini, Raza Daramsy – Muhindi? Tungojee na Chwaka mwakani – Noushad Moh’d. Tuje tumalizie na Koani Abdulsatar Haji Daud. Wote wahindi.

Mheshimiwa mwenyekiti tunakushukuru sana kuchukua muda wako mkubwa sana kwa kusoma barua yetu hii. Tunamalizia kwa kuomba kwako radhi na tunaamini utatusamehe kwani wewe ni kiongozi mwenye busara, na utalifanyia kazi suala nyeti tuliokueleza kwa madhumuni ya kurejesha umoja wetu na kudhibiti ushindi wa jimbo letu.

Wanachama wenzako,
Haji Juma Kibwana wa kijiji cha Uzi,
Omar Haji Mo’hd wa Kijiji cha Umbuji,
Kassim Juma Khatib wa kijiji cha Mgeni haji,
Selemani Bakari Bushiri wa kijiji cha Tunduni,
Fatma Herezi Said wa Kijiji cha Bambi,
Mustafa Khamisi Mustafa wa kijiji cha Kiboje,

Nakla kwa:
1. Makamo mwenyekiti CCM – Zanzibar, Dr Amani Abeid Karume
2. Naibu Katibu Mkuu CCM – Zanzibar, Vuai Ali Vuai
3. Wahariri wa vyombo vyote vya habari Tanzania

Advertisements

15 responses to “Barua ya watu wa Uzini kwa Rais Kikwete

 1. Salaam,

  Kuna uhakika gani kama hii barua inawakilisha mawazo ya wapiga kura wengi wa Uzini? Jee haiwezekani kuwa hawa walioandika hii barua wanatumiwa na mmoja wa wagombea? Una njia yoyote ya kulihakiki hili?

 2. for me its just a pointless, kwanini akashinda kwa kura nyingi sana kwenye kura za maoni wanachama wa hilo jimbo wamempa kura nyingi sana hawakujua hilo? huu ni upuuzi tu wa watu fulani fulani, by the way hawa watu wanjuana wenyewe ila kwa taarifa nilizonazo huyu bwana ameshawaagiza watu wa jombo hilo wafungue account kwa ajili ya kuingiza mishara na posho zake zote kutoka baraza la wawakilishi na ametenga jumala ya shilling millioni 200 kwa ajili ya wananchi ili wajiendeleze . waliowengi wanasema wamewajaribu hao wasio wahindi kwa muda mrefu hawana jipya walilokuja nalo sasa wanataka waone japo tofauti ndogo. waache ubaguzi wenyewe kwa wenyewe , hata hivyo sijui sheria ya uchaguzi , katiba na sheria ya nchi juu ya sifa za mgombea vyenginevyo mm sioni tatizo lolote hapo zaidi ya siaisa za makundi zinazowasumbua baadhi yao.

 3. Hao walioandika ujumbe huu ni watu wanodhani kuwa watu wa jimbo la Uzini wana mawazo finyu na hawajui kizuri wala kibaya na wao wanadhani kuwa ndio wanaweza kuwasemea watu wa Uzini. Sisi wana CCM wa jimbo la Uzini Tumetoa maoni yetu tarehe 11/12/2011 na huo ndio mtazamo, kwenda kinyume na mtazamo huo ni kuliuwa kabisa jimbo hilo. Sisi tunachotaka ni maendeleo, UKABILA, UMAJIMBO, UDINI KWA SASA HAUNA NAFASI. iKIWA MOH’DRAZA ANAISHI MBALI NA JIMBO JEE, MOH’D SEIF YEYE ANAISHI WAPI NA AMEFANYA NINI KWA KIPINDI CHOTE CHA MIAKA 20 YA UBUNGE WAKE, TUMECHOKA ukiritimba usio maslahi kwetu.

 4. JIMBO LA UZINI LINA WANACHAMA WA CCM WENGI SANA NA SISI HATUKUMBUKI KUTOA KILIO HICHO, HAYA NI MAWAZO YA WATU 6 WANAOTUMIWA NA WATU FULANI KUPAKA WENZAO MATOPE. NA HII INAONESHA WAZI JINSI WALIVYOFILISIKA KISIASA. NITASHANGAA SANA KAMA VIONGOZI NAO WATAKUWA NA MAWAZO NA MTAZAMO KAMA HUU.
  KURA YA MAONI NDIO SAUTI YA WANA CCM WA JIMBO LA UZINI.

 5. Naomba sana hawa watu waseme ukweli wasiropokwe. Ndugu Moh’d Raza hakutoa hata senti tano katika kampeni zake ila amewaahidi watu maendeleleo tu. Waliotoa pesa mbana mnawaficha. Ndugu KHALIFA ametoa pesa kwa kila mtu hata akapata jina la MMIMINA , JEE HILI HAMLIHUI ? KAMA HOJA NI PESA BASI KHALIFA ANGEPATA KURA ZOTE. Moh’d Raza anapendwa na watu wa Uzini si Jengine. Kama pesa hata Moh’d Seif anazo mbona ameshindwa hata kujenga Hospitali ya kwao alikozaliwa.

  Raza hana mbadala acheni chuki na Ubaguzi

 6. KAMA VIONGOZI WA JUU WA CCM HAWAKUTUMIA BUSARA BASI JIMBO HILI LITAVURUGIGA KWA KUPUUZA MAONI YA WATU WENGI. HIYO NDIO SAUTI YAO NA HIYO NDIYO NDOTO YAO. KURUDISHA JINA LA MGOMBEA MWENGINE NI KULIPOTEZA JIMBO HILO. CHADEMA WAKO MITAANI WAKIJUA KABISA KAMA JINA LA RAZA HALIKURUDI NJIA KWAO ITAKUWA NYEUPE. NA HUO NDIO UKWELI. RAZA NI CHAGUO LETU.

 7. hawa watu wanaojiita watu wa Uzini ni waongo kwani tumewatafuta katika matawi husika mbona hatukuwaona, hayo ni majina ya kupanga tu yaliyotumiwa na kigogo fulani wa jimbo la Uzini kuendeleza azma yake ya kumpinga RAZA asiwe mwakilishi wa Uzini kwa kuhofia kufichuka aibu zao.Mikakati ya kumuengua RAZA ilipangwa mapema lakini yote imegonga ukuta sasa imebaki kutengeneza uongo na kuupeleka kwa wakubwa, kwani hao wakubwa lipi wasilolijua kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi jimbo la uzini. RAZA JUU JUU

 8. Fitna na majungu tumeshayachoka ..tunataka maendeleo. kama ni mapinduzi na watu wa uzini ndio waliochangia ..sasa hatutaki blah blah ..tunachotaka ni kuona maendeleo yalioletwa na mchango wetu kwenye Mapinduzi na sio fitna na majigambo !

 9. Kesho ndio kesho (KAMATI MAALUM ZANZIBAR) tutajua mbichi au mbivu watu waliolishwa maneno kumpinga RAZA tunawajua na hakuna watakachoweza kubadilisha, RAZA AMETEULIWA NA MUNGU. fitina, majungu yafae nini sasa. Fanyeni upembuzi zakinifu ni mkereketwa gani wa CCM aliyemudu kukichangia chama kuliko Nd. MOH’D RAZA. AU NDIO ” BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA”

  UZINI NA RAZA, RAZA NA UZINI. HATUKUFANYA MAKOSA KUMCHAGUA NA HATUFANYA MAKOSA KAMWE.

 10. SASA AMKENI TUTAFANYA,TUTATEKELEZA,TUTAWASHUGHULIKIA NA MENGINEYO YAMEPITWA NA WAKATI SASA LA LEO LIFANYWE KAZI KWENU WA UZINI MNATAKA MAENDELEO AU MAREJEO WAKATI WA KUBADILIKA UMEFIKA KUWENI IMARA

 11. Mo’hd Raza ndio chaguo letu watu wa Uzini, acheni chuki binafsi, sisi tunachotaka ni maendeleo na si pesa zake, kwani hata katika kampeni zake hakutoa pesa wala hongo je? waliomwita mwarabu kafikia wapi? kama ingelikua wanachagua kwa kufuata pesa si agepata huyo aliyekua anaitwa mimina?,Hawa ni kikundi cha Othman Maulidi tunawajua malengo yao, na tunawambia kuwa Raza ndio chaguo la Wanauzini.kwahiyo Muheshimiwa Rais kua makini na watu hao sisi tunaamini kuwa wewe unathamini democrasia ya wengi, hivyo usije ukatoa maamuzi yakasababisha watu wakihame chama makini na kujiunga vyama vyengine, kama Chadema , CUF, na kadhalika.

 12. Ubaguzi tu, mnawatukana wahindi? Ao weusi wenzenu wamekufanyieni kipi cha maana? Moh’d Seif mnapajuwa anapoishi? Mmeshawahi angalau kumsikia akisema lolote la maendeleo ya uzini? Zenu ni siasa za kishamba, ona jimbo lilivokufa, njaa, maendeleo duni utadhani hakuishi watu loo, any way mtajijuwa wenyewe maana ndo mmeamua kuukumbatia mbuyu! na mchana utabakia kuwa mchana milele hata kama Juwa halitatoka.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s