Wazee wamkingia kifua Maalim Seif

Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika moja ya mikutano ya chake cha CUF katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania

“Heshima ya Maalim Seif kwetu sisi ni zaidi ya Katibu Mkuu au Makamu wa Kwanza wa Rais, kama mnataka tukwambieni ukweli wa mambo jamaa zangu”, alisema Mzee Saidi Makame, mmoja wa Waasisi wa CUF kutoka Mkoa wa Kusini Unguja alipoongea na Waandishi wa habari waliokuwamo katika msafara wa Viongozi wa Kisiasa waliozuru maeneo ya Uzi Wilaya ya Kusini, Unguja mwanzoni mwa wiki.

*Washutumu magazeti, mamluki, *Wasema wanaochechea watakwama

Baadhi ya wazee wa Chama cha Wananchi, CUF, wameibuka na kuvurumisha shutuma kali kwa waliowaita watu wachache wabinafsi na mamluki. Wameshambulia pia vyombo vya habari walivyodai kuwa havifahamu hadhi halisi ya Maalim Seif kwa Wazanzibari.

Wakiongea na waandishi wa habari kwa nyakati na mazingira tafauti ya Visiwa vya Unguja na Pemba, wazee hao ambao pia ni Waasisi wa CUF wamesema kuwa hakuna njama zozote zikazoweza kumchafua Maalim na kupoteza hadhi yake na kukubalika kwake kwa Wazanzibari.

“Heshima ya Maalim Seif kwetu sisi ni zaidi ya Katibu Mkuu au Makamu wa Kwanza wa Rais, kama mnataka tukwambieni ukweli wa mambo jamaa zangu”, alisema Mzee Saidi Makame, mmoja wa Waasisi wa CUF kutoka Mkoa wa Kusini Unguja alipoongea na Waandishi wa habari waliokuwamo katika msafara wa Viongozi wa Kisiasa waliozuru maeneo ya Uzi Wilaya ya Kusini, Unguja mwanzoni mwa wiki.

Mzee Makame alikaririwa akisema kuwa ni ukweli usiopingika kwamba heshima ya Maalim Seif ni kubwa katika Siasa na Maslahi ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, zaidi ya wanavyoelewa “baadhi ya wana magazeti wanaotumiliwa na watu wachache wabinafsi ndani ya CUF sasa hivi”.

“Mnavyomuona nyie Maalim Seif na hao jamaa zenu, sivyo kabisa,…sisi tutaendelea kumpenda wala asijidanye mtu bwana na nyie mkadanganyika”, alisema kwa hisia za hali ya juu Mzee Kassim Machano wa Chaani ambaye pia ni sehemu ya Waasisi wa CUF.

Hayo ni maneno yaliyosikika akiyatamka pia Mzee Denge Fumu wa Matemwe ambaye pia alisikika akisema hakuna anayeweza kuchukua mahali ya Maalim Seif katika mioyo ya Wazanzibari. Mzee Fumu ambaye ni miongoni mwa watu wenye heshima ya juu na Waasisi wa CUF katika Mkoa wote wa Kaskazini Unguja, amesema, inashangza kuona “watu wakipumbazika magazetini” wakidhani kinachoitwa mgogoro kitaisambaratisha CUF.

Kwa upande wa Mzee Juma Machano wa Donge, yeye anasema kuwa anahisi wanaoleta uasi ndani ya CUF wanapoteza muda kama siyo kuishiwa kisiasa kwani hawatafanikiwa. Mzee Machano alihoji akisema, “Ee bwana CUF wamekutana na waasi wengi wengine waliopandikizwa na hakuna aliyefua dafu, watafaulu hawa leo ambao wamekuja mambo yashakwisha?”

Baadhi ya viongozi wa CUF walipohojiwa juu ya mtazamo huo wa Waasisi, kutokana na kile kinachoendelea kuripotiwa na magazeti “ati suitafahamu ndani ya Chama hicho, na ambacho sasa ni Sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, walisikika wakisema “Seif na Chama si wa-kulumbana magazetini” na Wazee hao waasisi wanaona mbali…..wachilia mbali haki itajulikana muda ukifika”.

Pamoja na hayo Viongozi na Watendaji Wakuu wa Chama cha CUF wanatarajiwa kukutana kesho (Jumamosi) mjini hapa kujadili kile kilichobainishwa kuwa mustakbali na hatma ya Chama. Wakati huo huo Chama cha Wananchi, CUF, kimetoa salamu za rambi rambi kutokana na maafa yaliyolikumba Jiji la Dar es Salaam , na maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara, ndani ya juma hili.

Maafa hayo ni yale yaliyotokana na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyopekea vifo na uharibifu mkubwa wa mali, makaazi na miundombinu. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma wa CUF, Bw. Salim Bimani, jana mjini hapa, ilieleza kwamba Chama hicho kitatumia Vituo vyake vya Zanzibar na Tanzania Bara kuhamasisha huduma na misaada ya haraka ya kibinaadamu.

Alisema, CUF inaungana na waathirika wa maafa na mafuriko pamoja na wananchi kwa ujumla katika kukabiliana na athari za hali hiyo ya kusikitisha.

Chanzo Gazeti la Annuur

Advertisements

5 responses to “Wazee wamkingia kifua Maalim Seif

  1. Maalim seif ni Mandela wa Zanzibar ..I got none but respect for maalim Seif . thumbs up if u feel the same way.

  2. Mimi si mwanachama wa CUFila ni Mzanzibari. Sifurahishwi na maneno maneno yanayojitokeza sasa kwani hayaashirii kheri kwa Wazanzibari.

  3. Simlaumu Hamad Rashid kugombea nafasi yoyote katika chama cha CUF, hii ni haki yake ya kidemokrasia. Ila namlaumu Hamad Rashid kwa kutofuata taratibu za kichama kuelezea hisia zake, badala yake akawa anaropoka yalokuwemo na yasokuwemo. Chama chochote chenye heshima kinakuwa na taratibu zake za kichama, na ni wajibu wa wanachama kuzifuata hizo taratibu.

  4. Wanao fikiri wanaweza kumchafua Maalim Seif au kuwachafua Wazanzibari kwakweli wamechelewa,haya walitakiwa kuyafanya kabla ya kura ya maoni ya kuamua serikali ya umoja wa kitaifa,kwahiyo kama lengo lao ni kututoa kwenye njia ya kujadili katiba mpya na mungano,na kutaka tuwajadili wao ss hatuna muda nao wachwe waende wanako taka na waiche Zanziba ikiwa shari kama ilivyo.ss hatushawishiki lengo letu ni moja nikuiona Zanzibar ni nchi hao kama wanadhani Zanzibar haitokua na mamuzi yake basi hilo wasahau.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s