Karume akabidhiwa nishani ya shujaa wa Zanzibar

Mzee Hassan Nassor Moyo akimkabidhi Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume nishani ya Shujaa wa Zanzibar iliyotolewa na Swahili Performing Arts Centre (SPAC) ambapo nishani kama hiyo tayari ameshakabidhiwa Maalim Seif Sharif Hamad kutokana na mchango wa viongozi hao walisimamia maridhiano ya Zanzibar, walioshuhudia makabidhiano hayo Mwenyekiti wa SPAC, Kheri Abdallah Yussuf na Mjumbe wa Bodi, Ismail Jussa

Nishani kama hiyo ya ‘shujaa wa Zanzibar’ alitunukiwa pia Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika kilele cha sherehe za maridhiano huko uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba tarehe 3
Desemba 2011.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tarehe: 25 Desemba, 2011

Yah: Swahili Center yamtunikia Rais Mstaafu Dr. Karume nishani ya ‘Shujaa
wa Zanzibar’

Taasisi ya Swahili Performing Arts Center, inapenda kuvitangazia vyombo
vya Habari juu ya muendelezo wa mradi wa 100% Zanzibari kama ifuatavyo:-.

Kituo cha Sanaa za Maonesho za Waswahili (Swahili Performing Arts Center)
Zanzibar kimemtunukia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Dr. Amani Karume,
nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’ ikiwa ni hatua ya mwisho katika
kuadhimisha kufikiwa kwa maridhiano na hatimaye serikali ya umoja wa
kitaifa nchini Zanzibar.

Dr. Karume alikabidhiwa nishani hiyo na mwanasiasa mkongwe Mzee Hassan
Nassor Moyo  siku ya Ijumaa tarehe 23 Desemba 2011 katika hafla fupi
iliyofanyika nyumbani kwake huko Mbweni nje kidogo ya Mji Mkongwe.

Akiwasilisha risala yake katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili
Performing Arts Center Kheri Jumbe alitoa shukrani kwa Dr. Karume kutokana
na jitihada zake katika kuleta amani ya kudumu nchini Zanzibar.

Jumbe alieleza kuwa, taasisi yake iliona umuhimu wa kuandaa sherehe za
maridhiano kupitia mradi wa sanaa uliopewa utambulisho wa 100%  Zanzibari
(Mzanzibari asilimia moja) ili kuwaenzi waasisi wa maridhiano hayo na
kueliimisha wananchi juu ya umuhimu wake.

“Kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Oktoba 4 hadi Desemba 3, tumekwenda
katika mikoa yote ya Zanzibar na kuwasilisha ujumbe juu ya umuhimu wa
kuimarisha misingi ya umoja na kuweka mbele uzalendo, ‘ alisema Jumbe.

Akikabidhi nishani hiyo kwa Rais mstaafu, Mzee Hassan Nassor Moyo alirejea
wasia wake wakutaka viongozi wakuu wa Zanzibar kutowavumulia watendaji wa
serikali wanaovuruga maridhiano.

Katika kuipokea nishani hiyo, Dr. Karume aliwapongeza watendaji wa Swahili
Center pamoja na wasanii walioshirki katika mradi huo kwa juhudi zao
katika kuyaendeleza maridhiano kupitia sanaa zilizobeba ujumbe huo.

Nishani kama hiyo ya ‘shujaa wa Zanzibar’ alitunukiwa pia Makamo wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika kilele cha
sherehe za maridhiano huko uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba tarehe 3
Desemba 2011.

Wengine waliohudhuria katika uwasilishwaji wa nishani hiyo kwa Dr. Karume
ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe Ismail Jussa pamoja na
Mkurugenzi wa Sanaa was Swahili Center, Mahsin Basalama.

Kupitia mradi wa 100% Zanzibari wasanii 130 kutoka vikundi 11 vya sanaa za
maonesho walishiriki katika kambi za kjenga umoja na kufanya maonesho
nchini kote.

Mradi wa 100% Zanzibari umedhaminiwa na Ubalozi wa Norway pamoja na
kampuni ya mawasiliano ya Zantel.

Kwa maelezo zaidi kuhusu taarifa hii, tafadhali wasiliana nasi kupitia
anuani ifuatayo: –

The Swahili Performing Arts Center
Ground Floor, Old Dispensary Building
Mizingani Road, Stonetown
Zanzibar, United Rep. of Tanzania

Email: media@swahili-center.org
Homepage: http://www.swahili-center.org

Facebook: Swahili Performing Arts Center

 

Advertisements

2 responses to “Karume akabidhiwa nishani ya shujaa wa Zanzibar

  1. Mkataa wengi mchawi lakini mimi ninamaoni tofauti, suala ambalo nimekuwa nikijiuliza hivyo baba nyumbani kuwalisha watoto na kuwavisha na kuwapa makaazi mema kwa kufanya hivyo huwa anastahiki baba kuzawadiwa na jee ikiwa kwa siku zote alikuwa hayafanyi wajibu wake huyo kipindi chote hicho watoto wamfanye nini baba yao? Hapa ndipo ninaposhawishika kutoipenda democrasia hunipa mashaka inakuwaje ? Ngom’be wa mbele akikosea kwa kuwa tumo kundini anaepingwa wa nyuma kwasbabu yupo karibu na mchunga.

    abuu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s