Serikali ya Muungano yalaumiwa na wawekezaji Zanzibar

Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Wawekezaji Zanzibar (ZATI), Simai Mohammed Said akisalimiana na Prince Charles alipowasili nchini Zanzibar katika ziara yake

WAWEKEZAJI Zanzibar, waliilaumu vikali Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kishindwa kulinda usalama wao na mali zao visiwani Zanzibar. Walisema usalama wao na mali zao unatishiwa na vitendo vya uhalifu na juhudi za polisi kupambana na wimbi hilo ni mdogo.

Wawekezaji hao walitoa malalamiko hayo katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wawekezaji Zanzibar (ZATI) katika sekta ya utalii uliofanyika Zanzibar Beach Resort, Mazizini Zanzibar..

Akichangia taarifa ya ZATI ya mwaka juu ya mendeleo ya sekta ya utalii Zanzibar , `Mkurugenzi wa Kampuni ya Parasailiung, Mahmoud Thabit Kombo alisema hali ya usalama kwa wawekezaji, hasa wageni inatisha hivi sasa na kunahitajika juhudi za makusudi kuimarisha ulinzi na usalama wa wageni na wawekezaji.

Alisema hali hiyo inasababishwa na udhafu wa huduma za polisi kwa wawekezaji, watalii na jamii kwa jumla visiwani Zanzibar ambao hutolewa. Kombo alisema matukio ya wawekezaji kushambuliwa hayashughulikiwi kwa muda muafaka yanapotokea kwa sababu polisi hawana vitendea kazi kama wlaivyokuwa navyo polisi wengine nchini Tanzania.

Alisema hali hiyo imesababisha polisi wengi kutumia simu zao binafsi za mkononi kupeana taarifa juu ya matukio ya uhalifu. “Tatizo hilo linatokana na serikali ya Muungano kutenga bajeti ndogo kwa Jeshi la Polisi Zanzibar, wakati mwingine bajeti ya Zanzibar inafanana na inayotolewa kwa wilaya kama Sengerema,” alisema Kombo.

Aidha aliishauri ZATI kuitisha semina kwa Wabunge wa Zanzibar kuwafahamisha hali halisi juu ya ufinyu wa bajeti ya Jeshi la Polisi Zanzibar na tatizo la uhalifu ambalo linaonekana kuota mizizi kila siku zinavyosonga mbele.

Alisema anashangaa anapofuatilia vikao vya Bunge, hasikii Wabunge wa Zanzibar kuzungumzia tatizo hilo , tofauti na wenzao wa Tanzania bara ambao ameshuhudia wakiibana serikali kuongeza vituo vya polisi katika majimbo yao.

Kiongozi mwandamizi wa Taasisi ya Aga Khan Zanzibar, Mohammed Bhaloo, alisema polisi visiwani Zanzibar hawana magari, vyombo vya mawasiliano na mafuta. Alisema matatizo hayo yatatafutiwa ufumbuzi, vitendo vya uhalifu vinavyotishia usalama wa wawekezaji na mali zao vitapungua.

Kombo na Bhaloo walitoa ushauri huo baada ya Meneja Mkuu wa Hoteli Kitalii ya Hakuna Matata, Dk Fritz Geuen, kuuambia mkutano huo jinsi alivyovamiwa na majambazi na kunyang’amwa mali katika eneo la Bububu, Mkao wa Mjini Magharibi mwezi uliopita.

Dk Fritz alisema watu waliomvamia walikuwa na bunduki na visu na walimtaka atoke kwenye gari aliposita kufanya hivyo wakampora mkoba wake uliokuwa na fedha na vitu kadhaa vya thamani.

Alisema kilichomshangaza ni kitendo cha polisi kutokuwa tayari kumsikiliza na kuchukua hatua baada ya kuripoti tukio hilo katika kituo cha Malindi, kilometa sita kutoka eneo la tukio.

“Polisi wanachelewa sana kupokea taarifa za matukio ya uhalifu na kuchukua hatua,” alisema Dk Fritz huku akiongea kwa hisia kali na kukumbusha tukio la wafanyakazi wawili wa Hoteli ya Kitalii ya Mbweni Ruins walivyouawa na majambi kwa kupigwa mapanga mwaka huu.

Mmoja wa wawezekeaji katika kampuni ya ulizi ya G4S, Michal Miller, alisema wageni wamekuja Zanzibar na vitega uchumi hawapaswi kuwa na bunduki na mbwa kwa ajili ya usalama wao na mali zao kwa sababu kazi hiyo ni ya polisi.

“Police duty is not smiling and saying karibu sana , that is not the duty of security,” alisema Bi Michal akiwa na maana kuwa kazi ya polisi ni kulinda usama wa raia na mali zao badala ya kubaki watu wa kukaribisha wageni na kuwachekea.

Mjumbe wa Bodi ya ZATI, Simai Mohammed Said alisema kutokana na polisi kuelemewa, Zanzibar iwe na kikosi cha polisi, maalum kwa ajili ya ulinzi na doria katika sekta ya utalii.

Alisema utendaji wa kikosi hicho uhusishe askari kutoka vikosi vya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) na askari wa Valantia.

Simai alisema Seychelles imeweza kufanikiwa kutoa ulinzi kwa sekta ya utalii kwa tumimia kikosi kama hicho na akashauri kituo kidogo cha polisi Forodhani kiwe kituo maalum kwa ulinzi na doria katika Mji Mkongwe na kifanye kazi kwa saa 24. Simai ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZATI na pia ni mwekezaji mzalendo Zanzibar alisema eneo la Mji Mongwe ambalo amewekeza mkahawa wake lina matukio mengi ya uhalifu dhidi ya watalii wanaotembelea hifadhi ya mji huo.

Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kusini, Yussuf Macalani alisema malalamiko yote ya wawekezaji dhidi ya polisi yatafikishwa kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) Ali Khalil Mirza na uligharamiwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s