Polisi jipangeni kupambana na uhalifu-Maalim

Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad akifahamishwa mbinu za kujua noti bandia na Afisa wa Polisi, wakati alipotembelea banda la maonesho la Jeshi la Polisi, viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amelitaka Jeshi la Polisi kuzidisha bidii katika kuwapa watendaji wake taaluma ya utambuzi wa njia zinazotumika kufanikisha uhalifu kupitia mtandao (cyber crimes) kwa nia ya kukomesha uhalifu wa aina hiyo hapa nchini.

Maalim Seif alitoa wito huo alipokuwa akitembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho yaliyoandaliwa maalum kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yanayoendelea katika viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.

Alisema uhalifu wa aina hiyo ambao tayari umeripotiwa kuingia Tanzania umekuwa ukisababisha madhara makubwa kwa wananchi, na wahalifu hujihusisha na kufanikisha wizi wa mamilioni ya fedha kwa kutengeneza nyaraka bandia kupitia kompyuta.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema madhara mengine ya wizi wa mtandao ni kuzagaa vyeti na hati bandia pamoja na baadhi ya wananchi kutumia mtandao kutuma ujumbe wa matusi, mambo ambayo iwapo hayatadhibitiwa, jamii itapata madhara makubwa katika nyanja za kiuchumi na kijamii.

Aidha, Maalim Seif amelipongeza Jashi la Polisi kuanzisha kitengo maalum cha kupambana na uhalifu wa aina hiyo tokea mwaka 2006, pamoja na kuwapa mafunzo watendaji wa Jeshi hilo yanayolenga kuwapa uwezo wa kukomesha uhalifu huo.

Alisema mikakati madhubuti haina budi kuwepo kudhibiti uhalifu wa aina hiyo pamoja na wizi wa magari kutoka nchi moja hadi nyengine kwa kutumia Polisi wa Kimataifa hasa kutokana na hivi sasa wahalifu wanatumia mikakati mingi inayorahisishwa na teknolojia ya habari na Mawasiliano (IT).

Aidha, wakati akitoa majumuisha ya ziara yake ya kutembelea maonesho hayo kwa waandishi wa habri, Maalim Seif alihimiza vijana wawezeshwe kusomea teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwasababu hisi sasa imekuwa ikizaa ajira kwa watu wengine.

“Wakati huu tulionao TEKNOHAMA imekuwa na faida kubwa sana hasa katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wetu, … hivi sasa vijana wanaajiriwa na makampuni yaliyoko nje ya nchi yao kufanya kazi kupitia mtandao na kuendesha maisha yao vizuri”, alisema Maalim Seif.

Alisifu hatua ya serikali kuanzisha maonesho kama hayo kwasababu yanawawezesha wananchi na wageni kujua mambo na hatua mbali mbali zilizochukuliwa na serikali tokea nchi ilipopata uhuru hadi wake hadi sasa, ambapo kuna mambo mengi yamefanywa huku wananchi wengi wakiwa hawayajui na badala yake wanalalamika.

Alisema lengo hilo litafanikiwa iwapo serikali zitakuwa na tabia ya kuandaa maonesho na matamasha mengi zaidi na kuondokana na utaratibu wa maonesho yanayoandaliwa pale yanapotokea maadhimisho maalum ndipo yaandaliwe.
Makamu wa Kwanza wa Rais alisema baadhi ya nchi Duniani, kama vile Misri zinapata mafanikio makubwa kutokana na utaratibu ziliojiwekea kuandaa maonesho na matamasha mbali mengi, ambayo huwafanya wageni na wananchi kuyazowea na kuyafuatilia.

Habari na Khamis Haji, na Picha na Salmin Said -OMKR

Advertisements

One response to “Polisi jipangeni kupambana na uhalifu-Maalim

  1. ENYI WAZANZIBAR NA WAISLAM WATE WA TANZANIA TUSISHEREHEKEE UHURU WA TANGANYIKA WA 9/12/1961 KWANI HUU NI UHURU WA WAKRISTO NDIO WENYE HAKI TZ. Makanisa yanalipya mabilioni ya shilingi lakin waislam hawapati hata cent 1 kutoka serekali ya TZ. Uhuru wa waislam TZ bado. BALI WAISLAM WOTE TZ TUITANGAZE 9/12/1961 kuwa ni siku ya HUZUNI KWA WAISLAM TANZANIA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s