Al Shabaab:Tunakimbilia jahazi inayozama

Shamsi Vuai Nahodha

Marekani kwa visa vyake na malengo yake, ilitangaza kuwa watawala wa Afghanistan, Taliban, ni magaidi, ikaamua kuwapiga. Lakini ikataka pia msaada wa Pakistan. Rais wa zamani wa nchi hiyo, Pervez Musharraf, akakubali kutumika kuwapiga jirani zake na kuruhusu ardhi yake kutumiwa na jeshi la Marekani. Lakini wakati vita ikiendelea Afghanistan, ikajengwa mazingira kama haya ya kuona kuwa Al Shabaab sio tatizo la Somalia, bali la Kenya na Tanzania. Kwa hiyo polisi na jeshi la Pakistan nalo likatakiwa kuwapiga Taliban ndani ya Pakistan na jeshi la Marekani likajipa uhuru kuingia Pakistan kushambulia maeneo yaliyodaiwa kuwa ni vituo vya mafunzo vya magaidi.
Al Shabaab: Tunakimbilia jahazi inayozama
*Tukitumia japo 10% ya akili tutasalimika
*La, tukimuiga Goyim Musharraf, tumeumia

Na Mwandishi Maalum
Baada ya ile kauli ya awali ya Jeshi la Polisi juu ya kitisho cha Al Shabaab ikifuatiwa na ile ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, wiki hii vyombo vya habari vimeripoti tena juu ya kitisho hicho.Safari hii amenukuliwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akisema kuwa amelazimika kusitisha mikutano yote ya kidini kwa kuhofia kipigo cha Al Shabaab.

“Tishio la kigaidi la kundi la Al Shabaab la nchini Somalia, limeulazimisha uongozi wa serikali mkoa wa Dar es Salaam kusitisha utoaji wa vibali vya kuruhusu mikutano ya kidini kwa hofu kwamba kundi hilo linaweza kutumia mwanya huo kufanya mashambulizi.”

Hivyo ndivyo ilivyosema habari iliyoandikwa na mwandishi Nora Damian katika gazeti moja la kila siku mapema wiki hii.
Habari hiyo iliyopewa kichwa cha habari, “Viongozi Dar es Salaam wahofia Al Shabaab”, inamnukuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik akisema kuwa uamuzi wa kisitisha vibali vya mikutano ya kidini ni wa tahadhari za kiusalama.

Ukisema kuwa unasitisha mikutano Dar es Salaam kwa hofu kuwa magaidi wa Al Shabaab wanaweza kutumia mikutano hiyo kufanya mashambulizi, unachosema ni kuwa ndani ya nchi, ndani ya Dar es Slaaam kuna magaidi wa Al Shabaab.
Maana kwa mfano, haiwezi magaidi hao wakawepo Mogadishu au Kismayu wakafanya shambulio katika mkutano unaofanyika Jangwani, Kidongo chekundu au uwanja wa Barafu, Kinondoni. Wanaoweza kufanya hivyo ni Marekani, Ufaransa na Uingereza ambao wanaweza kupiga mahali wakiwa umbali wa maelfu ya maili au wakatuma ndege na Drone zikapiga na kurejea.

Al Shabaab hawana uwezo huo. Kwa hiyo tukisema kuwa tuna hofu ya kupigwa na Al Shabaab Kariakoo, tunachosema ni kuwa Al Shabaab wapo nchini. Sasa swali ni je, kama tuna uhakika kwamba Al Shabaab wapo Dar es Salaam, kwa nini hatuwakamati tukawafikisha mahakamani? Kwa nini, tunasubiri mpaka watupige?

Ufupi wa maneno habari hii kama ilivyoandikwa na mwandishi Nora inakoleza kitisho cha Al Shabaab na kuzidi kuwatangaza kuwa ni maadui, sio tu wa Somalia na Kenya, lakini maadui wa Tanzania pia. Ambayo tafsiri yake ni kuwa serikali ya Tanzania, kwa namna yake nayo ipo vitani na Al Shabaab. Kenya wao tayari wapo vitani kijeshi ndani ya Somalia. Kwa mwendo huu, sijui Tanzania nayo itaishia wapi.

Kiasi wiki moja iliyopita wanajeshi wapatao 28 wa Pakistan waliuliwa na majeshi ya Marekani na wengine kadhaa kujeruhiwa. Miongoni mwa waliouliwa ni pamoja na maafisa wawili wa jeshi mmoja akiwa na cheo cha meja na mwingine kapteni.

Askari hao waliuliwa baada ya kushambuliwa na ndege za kijeshi za Marekani/NATO ambazo kama kawaida yake ziliingia ndani ya ardhi ya Pakistan kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kusaka na kuwapiga Taliban wanaodaiwa kuwa ni magaidi.
Kufuatia mauwaji hayo ambayo sio ya mara ya kwanza, serikali ya Pakistan imetoa kauli ikiitaka serikali ya Marekani kufunga mara moja kituo chake cha kijeshi kilicho ndani ya ardhi ya Pakistan, Shamsi Air Base, Baluchistan, ambacho ndicho hutumiwa kurushia ndege zisizo na rubani, drones, zinazouwa wananchi wa Pakistan na Afghanistan wasio na hatia kila uchao. Na kwamba nchi hiyo inatizama upya ushirikiano wake wa kijeshi na Marekani katika hii vita inayoitwa ya ugaidi. Vita ambayo kwa kujitia mshirika mtiifu kwa Marekani, Pakistan imejikuta ikiruhusu ardhi yake kuwa ngome na kambi za kijeshi za Marekani na NATO. Askari na makachero pamoja na ndege za kivita, huingia zitakavyo bila ya kuomba kibali kutoka serikali ya Pakistan na kufanya mashambulizi.

Kupitia mashambulizi hayo, mamia kwa maelfu ya watu wasio na hatia wameuliwa. Watoto wakiwa shule, madrasa, waumini wakiwa misikitini, sokoni na hata kwenye harusi, wamekuwa wakishambuliwa na kuuliwa kisha hutolewa kauli kwamba ilidhaniwa kuwa ni magaidi.

Pakistan ni nchi iliyofikia kuwa na silaha za nyukilia ikipimana ubavu na India, lakini kwa kujiingiza katika mchezo huu wa Marekani, inadhoofishwa kila uchao huku ikifanywa nchi isiyokalika kwa vitendo vya kigaidi ambapo watu huuliwa kila uchao kupitia mashambulizi ya ndege za drone na zile za kawaida za kijeshi.

Kwa bahati mbaya rekodi yetu imekuwa ile ya kukimbilia kudandia majahazi yanayozama wakati waliomo ndani wakihangaika kutaka kujinusuru. Historia, uzoefu na yaliyowakuta wengine, haitusaidii hata kidogo kusoma na kuchukua hadhari.

Pakistan hivi sasa inatafuta namna ya kujinasua katika ushirika wake na Marekani, haiwezi. Lakini ukiangalia yanayoikuta hivi sasa mpaka raia na askari wake wanauliwa ovyo na nchi imekuwa haina usalama tena, ilianza kwa mchezo na usanii kama huu tunaofanya wa Al Shabaab.

Ipo hivi: Marekani kwa visa vyake na malengo yake, ilitangaza kuwa watawala wa Afghanistan, Taliban, ni magaidi, ikaamua kuwapiga. Lakini ikataka pia msaada wa Pakistan. Rais wa zamani wa nchi hiyo, Pervez Musharraf, akakubali kutumika kuwapiga jirani zake na kuruhusu ardhi yake kutumiwa na jeshi la Marekani. Lakini wakati vita ikiendelea Afghanistan, ikajengwa mazingira kama haya ya kuona kuwa Al Shabaab sio tatizo la Somalia, bali la Kenya na Tanzania. Kwa hiyo polisi na jeshi la Pakistan nalo likatakiwa kuwapiga Taliban ndani ya Pakistan na jeshi la Marekani likajipa uhuru kuingia Pakistan kushambulia maeneo yaliyodaiwa kuwa ni vituo vya mafunzo vya magaidi.

Zipo taarifa nyingi zilizochapishwa na watafiti na waandishi mbalimbali zikionesha kuwa makachero wa Marekani pamoja na vibaraka wa Kipakistan, walikuwa wakitumiwa kulipua maeneo mbalimbali ili kuonesha kuwa kitisho cha magaidi wa Taliban na Al Qaida ni cha kweli. Kupitia mchezo huo, wananchi wengi wameuliwa na kutiwa vilema. Na kupitia mchezo huo, Marekani ilipata sababu kwanza ya kuishinikiza serikali ya Pakistan kuongeza nguvu katika kuuwa raia wake wenyewe ikidaiwa ni kupambana na magaidi.

Kwa upande wa pili, Marekani ilipata sababu ya kujiimarisha zaidi kijeshi na kikachero ndani ya Pakistan. Nchi hiyo hivi sasa ni kama imezingwa na chatu, uwezo wake wa kinyukilia haukuisaidia chochote. Inabomolewa kila uchao. Chanzo ni kuingizwa kijinga kwenye vita kichaa dhidi ya dui wa kutengenezwa kwa masilahi ya beberu, Marekani.

Ukitaka kujua kuwa ni adui wa kubuni, soma habari za kusilimu mwandishi Yvonne Ridley. Huyu ni mwandishi mwanamke aliyekwenda kuandika habari za Taliban akiwa na picha kichwani ya kukutana na watu magaidi katili kama walivyokuwa wakitangazwa na vyombo vya habari vya Magharibi. Kwa bahati mbaya au nzuri kwa upande mwingine, Yvonne alikamatwa na Taliban.

Kutokana na wema aliofanyiwa katika muda alioshikiliwa kabla ya kuachiwa, ilimpelekea kutambua kuwa Taliban waliokuwa wakiitwa magaidi, sio waliokuwa wakitawala Afghanistan. Taliban magaidi walikuwa zimwi la kuundwa na wanasiasa wa Marekani pamoja na vyombo vyao vya habari. Aliporejea Uingereza Yvonne aliamua kusoma Qur’an na Uislamu kwa ujumla ili ajue mafundisho yaliyowafanya Wataliban kuwa watu wema, rahimu na wakarimu kiasi kile. Aliishia kusilimu.

Lakini kama tunavyoimbishwa Al Shabaab hivi leo, Musharraf alitakiwa kushiriki kuwapiga Taliban na na ndugu zake wa Afghanistan kuwatangaza kuwa ni magaidi kama Kenya inavotumiwa hivi leo kuwapiga na kuwauwa ndugu zao na jirani zao Wasomali. Kinachoikuta Pakistan hivi leo, ni matokeo ya mchezo kama huu inaofanya Kenya.

Wasomali wamekaa wakivurugana na kuuwana bila ya kuwa na serikali kwa zaidi ya miaka 16. Wakafika mahali wenyewe wakapata ufumbuzi nchi ikatulia. Marekani haikutaka. Ikiitumia Ethiopia, ikavunja serikali iliyorejesha amani na utulivu Somalia. Vita ikarudi, Al Shabaab wakaibuka kupinga uvamizi na kukaliwa na majeshi ya Ethiopia na mengine ya kigeni. Leo tunaimbishwa kuwa hawa ni magaidi na sisi tunajitahidi kuimba kwa hima kubwa na kujitisha na kuweka mbinu za medani kupambana nao. Tunageuzwa kuwa Musharraf wa kupambana na ndugu zetu, jirani zetu na Waafrika wenzetu Wasomali.

Tunachotakiwa tufahamu ni kuwa kinachoikuta Pakistan hivi leo ni gharama inayolipa kwa ujinga wa ki-Goyim uliofanywa na Musharraf. Juzi hapa Waziri Mkuu wa Pakistan, Yusuf Raza Gilani, amenukuliwa na Shirika la Habari la Reuters pamoja na televisheni ya CNN akisema kuwa hakuna tena bishara ya kushirikiana na Marekani kijeshi.

“Business as usual will not be there,” alinukuliwa Gilani akijibu swali la mpasha habari wa CNN aliyetaka kujua nini itakuwa hatma ya ushirikiano wa Pakistan na Marekani katika vita dhidi ya ugaidi kufuatia shambulio lililofanywa na ndege za kijeshi za Marekani/NATO na kuuwa askari 28 wa Pakistan.

Hata hivyo, hii yaweza kuwa kauli ya kujikosha tu ya serikali ya Pakistan. Maadhali Marekani ishajichimbia kijeshi ndani ya ardhi ya Pakistan ikiwa na kambi za kijeshi na ndege za drone pamoja na silaha nzito za kijeshi, Gilani na serikali yake hawana ubavu wa kuiambia Marekani toka. Ishakuwa kisa cha ngamia na mwenye hema.

Sasa tuna hiyari, kupanda boti inayozama ya Goyim Musharraf ambayo kwa bahati mbaya Kibaki na Raila Amollo Odinga tayari washaidandia au tutumie japo asilimia kumi tu ya akili zetu tusalimike.

Chanzo Gazeti la Annuur

Advertisements

2 responses to “Al Shabaab:Tunakimbilia jahazi inayozama

  1. Duh! maneno yamekamilika wallahi lakini ndio hivyo, viongozi wetu wanongozwa na kufuata hewallah bwana, utumiaji wa akili haupo!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s