Msiongeze wake ovyo-Maalim Seif

Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiveshwa koti la uokozi (life jacket) wakati akijitayarisha kuvuka bahari na kuelekea Kisiwa cha Kojani Kisiwani Pemba

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema wakulima wa karafuu kisiwani Pemba wanatarajiwa kutia mifukoni kiasi cha shilingi bilioni 50 hadi mwishoni mwa msimu wa zao hilo mapema mwakani, na kuwahimiza fedha hizo zitumike kwa maendeleo na wajiepushe na tabia ya kuzitumia kwa kuongeza wake bila sababu za msingi.
Maalim Seif alisema mafanikio hayo kwa wakulima wa karafuu wa Zanzibar ni matokeo ya utekelezaji ahadi za serikali za kuhakikisha wananchi wanakuwa na maisha bora, wakiwemo wakulima, wafanyakazi na wavuvi, ambao ndio wanaochukua asilimia kubwa ya wananchi wa Unguja na Pemba.

Alisema serikali ya awamu ya saba iliazimia kupandisha bei ya mazao mbali mbali, ikiwemo la karafuu kwa nia ya kumuona mkulima ananufaika na mazao yake kwa asilimia 80, ambapo hivi sasa wakulima wa karafuu wanauza karafuu zao kilo moja daraja la kwanza kwa shilingi 15,000 kutoka shilingi 5000 msimu uliopita.

Alisema hayo leo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kisiwa kidogo cha Kojani, mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya siku nne kisiwani Pemba. Makamu wa Kwanza wa Rais alisema bei nzuri ya karafuu ni neema kubwa kwa wakulima kwasababu huko nyuma wakulima walikuwa hawapati hata asilimia 30 ya mapato yatokanayo na mazao yao, lakini hivi sasa baada ya serikali kuona umuhimu wa mkulima kunufaika na imeweza kupandisha bei katika kiwango kwenye maslahi.

“Mkulima wa karafuu sasa anapata asilimia 80 ya mazao yake, tunatarajia hadi mwishoni mwa msimu huu wa karafuu bilioni 50 zitakuwa zimeingia Pemba, zitumie fedha hizo kwa mambo ya maendeleo, na sio kuoa wake wengi zaidi bila ya sababu za msingi”, alisema Maalim Seif.

Alisema baada ya mafanikio kuanza kupatikana katika zao la karafuu, serikali inaelekeza nguvu kubwa katika zao la mwani, ambalo hadi sasa wanunuzi wanawalipa wakulima kwa bei ya chini, ambayo hailingani na kazi wanayoifanya pamoja na kulihudumia hadi kufikia hatua ya kuwauzia wafanyabiashara hao.

Akipokuwa katika ziara katika kisiwa kidogo cha Tumbatu, wiki mbili zilizopita, Makamu wa Kwanza wa Rais alisema serikali itaendeleza mazungumzo na wanunuzi wa zao la mwani kuwataka wapandishe bei angalau ifike shilingi 1000, lakini iwapo watakataa, serikali itafikiria zao la mwani linunuliwe na serikali kupitia Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC), kama inavyofanya kwa zao la karafuu.

Akielezea mafanikio mengine ya serikali hii ya awamu ya saba yenye mfumo wa umoja wa kitaifa alisema ni kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 25, kiwango ambacho ni kikubwa na kwamba ni nchi chache zinazoweza kuongeza mshahara katika kiwango kama hicho kwa mara moja.

Maalim Seif alisema nyongeza hiyo ya mshahara inakwenda sambamba na kulipwa wafanyakazi ambao kwa muda mrefu walikuwa hawajapewa nyongeza zao, ambapo pia mafao ya kada muhimu kama vile madaktari yameongezwa, ili kwends sambamba na majukumu mazito wanayoyakabili, lakini pia walingane na wenzao wa Tanzania Bara.

Alisema baada ya hatua hiyo ya kuzingatiwa mafao ya madaktari hakuna sababu hivi sasa wakahamie sehemu nyengine kama vile Tanzania Bara kwasababu maslahi ambayo wangeweza kuyapata huko wanalipwa hapa hapa Zanzibar.

Akizungumzia sekta ya uvuvi, Maalim Seif alisema matumaini makubwa ya mafanikio yameanza kujengeka kufuatia juhudi zinazoendelea kuchukuliwa kuvutia wawekezaji katika sekta hiyo, ambao wataweza kuwanufaisha wavuvu wadogo wadogo wa Unguja na Pemba.

Aliwaleza wananchi wa Kojani ambao asilimia kubwa ni wavuvu kuwa, baadhi ya wawekezaji wa sekta hiyo tayari wameonesha nia ya kuja kufungua viwanda vya kusindika samaki, kutengeneza boti za kisasa kwa ajili ya wavuvi wadogo wadogo wa Zanzibar pamoja na kuleta meli kwa ajili ya shughuli za uvuvi wa bahari kuu, ambapo wavuvi wa Zanzibar ndio walengwa wakuu wa ajira katika meli hizo.

Huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara, Maalim Seif alisema mbali na wawekezaji katika sekta ya uvuvi kuonesha dhamira za kuja kufungua miradi Zanzibar, juhudi nyengine zilizokwisha chukuliwa na serikali ni kuwapeleka wavuvi kutoka vikundi mbali mbali vya Zanzibar nchini China kujifunza mbinu za kufuga samaki na baadaye wao wawafundishe wananchi wengine.

Hata hivyo, alionya kwamba juhudi hizo zitakuwa na mafanikio makubwa iwapo wananchi wa Zanzibar watatoa kipaumbele katika kuyalinda na kuyahifadhi mazingira ya bahari kwa kujiepusha na aina zote za uvuvi haramu na uharibifu wa matumbawe ambayo ndiyo mazalia ya samaki na kuepuka kukata miti ya mikoko.

Maalim Seif alisema kwamba siri kubwa ya mafanikio yaliyoanza kujitokeza Zanzibara ni kuendelea kudumisha amani na utulivu tokea kufikiwa maridhiano ya kisasa na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo hivi sasa imetimiza mwaka mmoja na kuhimiza wananchi wote kuhakikisha umoja na mshikamano huo unalindwa, ili kuleta mafanikio zaidi.

Akizungumzia mipango ya CUF akiwa kama Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif alisema lengo la chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2015 ni kushinda nafasi ya Urais wa Zanzibar na kutoa Makamu wa Pili wa Rais.
Habari na Khamis Haji, Picha na Salmin Said (OMKR)

Advertisements

3 responses to “Msiongeze wake ovyo-Maalim Seif

 1. This is too much Maalim Seif.Who do you think you are to control people rights of marriage defined by Allah.Its non of your business to to deal with Marriage affairs.You are not a religious nor traditional leader but political leader.There are so many issues you should address like your irresponsible government that let thousands drown in the sea as a result of corruption and unscrupulous government officials.You should also tell your friend Mazrui and Bopar not to import Mapembe rice which is not good for human consumption and recently the main cause of Cancer in the Islands.Please show us that you care.Do what is important and urgent.Leave the marriage to the religious leaders and God! You can not tell people how to spend their money.Its theirs not your huh!

 2. This is too much Maalim Seif.Who do you think you are to control people rights of marriage defined by Allah.Its non of your business to to deal with Marriage affairs.You are not a religious nor traditional leader but political leader.There are so many issues you should address like your irresponsible government that let thousands drown in the sea as a result of corruption and unscrupulous government officials.You should also tell your friend Mazrui and Bopar not to import Mapembe rice which is not good for human consumption and recently the main cause of Cancer in the Islands.Please show us that you care.Do what is important and urgent.Leave the marriage to the religious leaders and God! You can not tell people how to spend their money.Its theirs not yours huh!

 3. ASALAM ALAYKUM!
  Ninachokiona nikua Maalim Seif alikua asme kua “watu kutokana na kipato kuongezeka ni kujitahidi kuleta maendeleo.” Quran limeleza jambo la kuoa zaidi ya mke mmoja kwenye Plural, 2, 3, 4 ukishindwa kua muadilifu ubaki na mmoja. Sasa kisha tunaambiwa “Hatokuja kiumbe kwenye ardhi ila ana rizki yake.” Hoja ni za kisiasa lakini zinapingana na mafundisho ya dini. Moja ya tabu za khutba za hapo kwa hapo “extempore” ni kua maneno yanakuja tu na kukosa kipimo. Kuoa ni haki ya mtu, kuongeza ikiwa kunakupelekea kuweza kutimiza uadilifu hakuna wakukuambia Bee wala Tee.

  Leo unaposoma suala la kukua kwa Idadi ya watu utaona afkar mbalimbali zinaelezewa. Unakuja kuona idadi inaongezeka, lakini hapohapo unakuja kuona idadi inavyopungua. Mashaka ya mambo haya nimoja ni suala la Climate Change, mabadiliko ya tabianchi mengine uchumi wa dunia kuingia katika msukosuko, jengine ni nchi aghlabia za Ki-Africa kutokua na mipango madhubuti. Wengi wa magwiji wa Idadi ya watu hutoa vitisho kama vya Rev. Malthus, lakini wasomi mambo leo hua hawalioni jambo la kuongezeka kwa idadi ya watu ni mashaka, wao walionalo ni uongozi, udhibiti, ubadhirifu, rushwa kuifisidi na kuimaliza taifa ndio vyenye kuchangia kuzifanya nchi kua kwenye dimbwio la Ufukara na shida nyengine wala sio Kuoa wake wengi. Kuna moja ya Mihadhara ya Dr. Zakir Naik juu ya Polygamy kama utaisikiliza utaona kua kuzuia idadi ya watu hususan nchi zinazoendelea na Africa ni mbinu za nchi tajiri kudhibiti rasilmali za nchi hizo na kuwatia uoga.

  Wakojani waendelee na neema walioipata ila watapotaka kuongeza wawe na sababu na wajue kuna watu watafufuliwa wanakwenda bega moja upande siku ya Qiyama sababu walikua sio wadilifu kwa wake zao kwa kuelemea upande mmoja.

  Ben Rijal

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s