Alhamdulillah Yarabbi Umoja huu uendelee zaidi

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, (wa pili kushoto) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Seif (kushoto) na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, wakisikiliza maelezo kutoka kwa mjasiliamali , Biubwa Said aliyekuwa akiwaelezea jinsi ya kuandaa Clips za Viazi, Mihogo na Tambi za Unga wa Dengu, wakati wa fanyabiashara wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26.

Ametakasika Mwenyeenzi Mungu mwingi wa Rehema na Neema na yeye pekee ndiye anayestahiki kushukuriwa na waja wote bila ya shaka. Zanzibar imetoka mbali na bado ina safari ndefu lakini kwa umoja na mashirikiano bila ya shaka tutafika Inshaallah inafurahisha kuona nyuso zilizohukuwa na huzuni leo hii zina furaha na tabasamu za aina yake ALHAMDULILLAH. ALHAMDULILLAH nilipokuwa naitazama picha hii nimetokwa na machozi sana machozi ya uchungu nikikumbuka zamani lakini na machozi ya furaha nikiwaza sasa tulipo. Nikiifikiria Zanzibar ilipotoka na sasa tulipo na wapi tunakwenda Wallah ..tunapaswa kusema ALHAMDULILLAH -ALAA KUL- HAL  sihaba tumetoka mbali na safari yetu bado inapaswa kuendelezwa na kila mmoja wetu ili tufike safari yetu kwa salama inshallah. Huko nyuma kwa hakika hatukuwa na kabisa na ukuruba na function kama hizi ambazo zinashirikisha jamii yetu ipasavyo, nakumbuka hata ile siku ambayo huadhimishwa kama ni siku ya wanawake duniani basi wanawake wa Zanzibar huwa na makundi mawili CUF huwa wanaadhimisha kwa upande wao na CCM huwa ndio wanaadhimisha kitaifa kwa kufanya maandamano na matembezi na kupokewa na waziri wa wanawake. ALHAMDULILLAH leo tunaona hapo yupo Mama Awena (Mama wa makamu kutoka CUF)  anafuatiwa na Mama Asha (Mama wa makamu kutoka CCM) anafuata Mama Fatma Ferej ni Mwakilishi kutoka CUF na anafuatiwa na Mama Mgeni ambaye ni Mwakilishi wa CCM: NASEMA TENA ALHAMDULILLAH Mwenyeenzi Mungu ajaalie umoja wetu udumu zaidi Inshallah.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s