Makahaba wasambazwa Unguja

Ngome Kongwe ni miongoni mwa vituo vikubwa vinavyotumika kuuzia ulevi katika sherehe mbali mbali

*Wafungua danguro Paje, na kuliita Vuvuzela,*Yadaiwa ni mbinu mpya ya mfumokristo

*Ni katika kudhoofisha Uislamu Zanzibar

 Na Waandishi wetu

Pamoja na hujuma mbali mbali za kudhoofisha jamii na maadili ya Kiislamu katika Visiwa vya Unguja na Pemba,kamailivyo kote walipo Waislamu, mbinu mpya zimebainika, hali iliyoibua hoja mbali mbali za waumini.Katika siku za karibuni Waislamu waZanzibarwameripoti kubaini wimbi la harakati za mfumokristo zinazolenga kuudhoofishaUislamu,TanzaniaVisiwani.

Mbinu hizo ambazo baadhi zimekuwa na mizizi ya tangu asili na zama, zimedaiwa kuelekezwa sasa kila ambapo pametengamaa na maadili mema au harakati za kawaida za Waislamu, zikiwamo pia sehemu za ajira na taaluma.

Katika kile kilichowashitua na kuwashangaza Waislamu wa Visiwa hivi kwa siku za karibuni, ni huduma ambazo hapo kabla hazikuwapo na wala hazikubainika, kinyume na hali ilivyosasa.

Huduma hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa vituo vinavyoitwa vya burudani ambavyo lengolakenikuhamasisha biashara za ulevi na ukahaba.

“Wapo vijana ambao tuna kila ushahidi wanaletwa hapa kwa makusudi ili kutuharibia jamii yetu”, alisema Maalim Ali, Mkaazi wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja, sehemu ambayo kwa sasa imesibiwa kwa kiasi kikubwa na vitendo hivyo.

Masikitiko ya Waislamu wa Paje na Vijiji vya jirani vya Jambiani, Bwejuu na Michamvi ni kwamba ndani ya maeneo hayo kumekuwapo na ongezeko kubwa la mabinti wa kutoka nje ya Zanzibar ambao wanajiuza kwa thamani ndogo kabisa hali inayotishia kwa kiasi kikubwa mporomoko wa maadili ya vijana wa Kiislamu.

“Naona sasa hawa jamaa wa mfumokristo wamepania maana kila tukikataza na wao wanakaza kamba wanafanya makusudi hawa kuuharibu Uislamu”, alisema Sheikh Kassim mmoja wa Wasomi wa Kiislamu, katika vijiji hivyo.

Uchunguzi umebaini kuwa kero kubwa katika maeneo hayo kwa kipindi cha karibuni ni kuwapo kituo kijulikanacho kwa jina la Vuvuzela, ambapo walevi na makahaba wa kigeni huonekana hapo katika kila siku za wiki.

Waislamu wa maeneo ya vijiji hivyo wamesikika wakilalama kwamba makahaba hao wanaojiuza kwa ujira mdogo wanaletwa kwa makusudi ili kudhoofisha maadili.

“Hatujui ni nani awaletaye, lakini twajuwa hii ni mbinu ya makusudi ya maadui wa Uislamu”, alisema Saidi Ameir, mmoja wa walezi wa Madrasa iliyopo Paje.

Tayari Waislamu walishapanda ngazi katika Serikali Kuu yaZanzibarili kuishitaki kadhia hiyo thakili ambayo kwa ujumla imewanyima haliyaoya utulivu na ustaarabu katika maeneo hayo ambayo kabla yalipigiwa mfano kwa maadili ya Kiislamu na taaluma ya dini.

“Serikali na wakubwa walijaribu kufuatilia ikawa nafuu kwa kiasi Fulani, lakini twaona sasa mambo yamerudi tena kulikoni vile mwanzo”, alisema Sheikh Said Ameir.

Wapo wanaoamini kuwa kuwapo kwa hali hiyo kunaelekezwa makusudi katika maeneo hayo ili kuziteka fikra za vijana na watoto wa Kiislamu waliolelewa hapo kabla na maadili mema ya kidini.

Katika Shura ya Waislamu wa Paje na vitongoji vya jirani walioketi hivi karibuni kutafakari mustakbali wa jamii na vizazi vyao, wengi hawakuacha kuhoji, “wapi mfumokristo unakoipelekaZanzibar”.

Mbali ya hujuma za aina hiyo kumeripotiwa pia hujuma na mbinu za kuwateka na kuwaritadisha vijana hasa mabinti wa Kiislamu.

Katika kile kilichoripotiwa hivi karibuni katika moja ya Taasisi za Fedha za Jamhuri ya Muungano, iliyopoZanzibar, mabinti wapatao watano wamesharitadishwa, kwa kisingizio cha hururi tu za ajira na masurufu ndani ya taasisi hiyo.

Wengi wa Waislamu waZanzibarwanaamini kuwa hiyo ni katika mbinu za makusudi zinazoandaliwa kanisani ili kuwalenga Waislamu kifikra na kinadharia, na ili hatimaye kuidhoofisha jamii ya Kiislamu.

“Usishangae hawa jamaa… utaona wanavyojipenyeza humu mitaani ukiwapa sehemu siku ya pili wasikia tayari wataka kujenga kanisa, Waislamu lazima wawe makini”, alisikika akisema Ustadh Nassor wa Mwanakwerekwe, mjini Unguja.

Advertisements

9 responses to “Makahaba wasambazwa Unguja

  1. Nikweli tusipokua makini tutaumia lakin mara hii hatukubili ni lazima kieleweke tutajua wazanzibar km mdobwedo au wanywa urojo hapo mtakapo kataa kunjaa muungano blood itamwagika mara hii ushehe tunauweka pembeni kwanza

  2. DAWA YAO NI KUWATIA MOTO WAO, PAMOJA NA HILO DANGURO LAO, VUVUZELA, REGADLESS MUNAJAMAA ZETU KWENYE HILO DANGURO AU LAA!!

  3. asalam alaikum kwakeli inaniuma sana kusikia habari kama hizi. Lakini kwanini serekali haiwarejeshi kwao hao wanaofanya ukahaba na hicho kikundi cha vuvuzela kivunjwe mara moja. Watatuharibia vizazi vyetu pamoja na maadili ya wazanzibari. Hapa znz wametoka mashekh wakubwa lakini angalia saivi znz inavyoshuka hadhi. Ya rabi ijalie serekali yetu ya znz ifunuke akili ili haya mambo machafu yasitendeke hapa znz. Amin.

  4. Kwanza naanza kwa kulaani kwa nguvu zangu zote hasa kama nikweli lengo lao ni kuupotosha umma. la pili wakazi wa Paje wenyewe wana makosa au wanahusika nani aliyeuza hicho kiwanja? tatu ni nani mteja wa hao makahaba? na la mwisho wazanzibar tuamshane katika hili tutalaumu watu lakini kwa upuande wa pili tunahusika. wasalaam

  5. cha msingi kila mtu awa katika nafasi yake na aelewe anafanya nini sio kuwalaumu hao makaaba kwani wanakulazimisha kutemea nao?

  6. Hili ni tatizo kubwa mno na tena linakua. Hatari yake likikua mpaka likatuzidi itakua ni maangamizi makubwa. Siasa zinatufikisha pabaya. Wengi wa hao makahaba ni wageni ambao wanavyo vitambulisho vya Uzanzibari ndo maana hawaulizwi. Viongozi ndio wa mwanzo mtakaoulizwa Dunia tuapita tu. Mmemsahau Mwenyezi Mungu kwa marupurupu manono mnayopewa. Yatakuja kukutokeeni puani hayo. Kifo hakina ubaguzi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s