Mbio za ngarawa Zanzibar kukuza utalii wa visiwani Italia

Ngarawa ni moja ya vivutio vya Zanzibar

ZOEZI la maonyesho ya mbio za ngalawa lenye lengo la kukuza utalii wa Zanzibar nchini Italia yalianza jana visiwani hapa, kiongozi wa zoezi hilo alitangaza jana.Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Francesco Gambela, ambaye ni mtaalam wa mchezo wa ngalawa nchini Italia alisema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku kumi, Unguja na Pemba.

Alisema zoezi hilo litaambatana na maonyesho ya mbio za ngalawa katika bahari ya Hindi karibu na maeneo ya vivutio mbali mbali vya utalii kwenye mwambao wa visiwa vya Zanzibar, kama vile fukwe za Nungwi na Mangapwani.

Gambela alisema washiriki wa zoezi hilo linajumuisha wataalam wa picha za televisheni, wakiwemo wa Amref International ambao kazi yao ni kupiga picha juu ya maendeleo ya utalii visiwani Zanzibar , shughuli za shirika hilo za kusaidia jamii visiwani humo pamoja na za mwenendo wa zoezi lenyewe la mbio za ngalawa.

Mtaalam huyo ambaye pia ni mwalimu wa Shirikisho la Mbio za Ngalawa nchini Italia, alisema picha zitakazopigwa wakati wa zoezi hilo, zitaonyeshwa nchini Italia na sehemu ya fedha zitakazopatikana zitatumika kusaidia wagonjwa kisiwani Pemba, chini ya mpango wa Amref International.

Alipoulizwa kwanini amechagua kufanya shughuli za kukuza utalii wa Zanzibar na kuwasaidia wagonjwa kisiwani Pemba, Gambela alisema anataka kuondoa hofu iliyopo nchini Italia kwamba hali katika maeneo ya mwambao wa bahari ya Hindi, ikiwemo Pemba na Malindi huko Mombasa ni ya kutisha kiusalama.

Gambela na kikundi cha wataalamu wanne wa picha za televisheni waliwasili Zanzibar juzi na kukaribishwa na Waziri wa Habari na Utalii wa Zanzibar, Abdillah Jihad Hassan na Balozi mdogo wa Italia huko Zanzibar, Poalo Chiaro.

Wakizungumza katika mkutano wa kikundi hicho na waandishi wa habari, Waziri Hassan na Balozi Chiaro walisema Zanzibar imekubali kuwa mwenyeji wa zoezi hilo kwa sababu inaamini michezo ni moja ya njia zinazosaidia kukuza ushirikiano miongoni mwa jamii ya kimataifa.

Kw upande wake, Waziri Hassan alisema mbali na kukuza utalii wa Zanzibar nchini Italia, kufanyika Zanzibar kwa mara ya kwanza zoezi la mbio za ngalawa kutasaidia kuibua vipaji vya mchezo huo visiwani humo.

Habari kwa hisani ya Charles Mwankenja

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s