Muungano, Mswaada na Zanzibar: kamba ya kuvuuka ama kitanzi cha kujitundika?

Muungano huu haujadiliki kwa sababu haupo. Kwa hiyo kuulinda kwake ni kuweka hijabu nzito baina ya kitu ambacho hakipo na akili ambazo zikiachiliwa kuujadili zitakhitimisha kuwa haupo! Na ndio maana tumeletewa tuujadili muswada wa “Sheria kwa ajili ya kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa madhumuni ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba…” Na maoni ya wananchi yatakusanywa wakati tayari kazi ya kuusambaratisha uongozi wa CUF na CCM uliosimamia Maridhiano imeshaanza kufanyiwa kazi.

Tayari kuna viongozi wenye nyadhifa za juu ndani ya uongozi wa CUF ambao wameshapangiwa na wameshapangwa wauchukue uongozi kutoka waasisi wa Maridhiano, Maalim Seif, Ismail Jussa na wenzao. Yakifaulu mapinduzi hayo (na Inshaalla hayotafaulu), na uongozi wakapewa mabwana X na X, basi tayari mpasuko wa kijamii uliozibwa na Maridhiano na Katiba ya Zanzibar utarudi tena Zanzibar .

Wapangaji (na Allah anapanga, na Allah ni Mkubwa wa Wapangaji) wanaona iwapo mapinduzi hayo yatafaulu, basi asilimia kubwa ya wapiga kura ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano itakwenda arijojo. Kwa hiyo kwa upande wa CUF Zanzibar, litapatikana nofu zuri la “HAPANA.”

Pia tukumbuke mwakani 2012 kutafanyika uchaguzi mkuu wa CCM na hapo pia panatakiwa lizibwe pengo litakalowachwa na Muasisi wa Maridhiano na wenzake, Rais Mstaafu Dkt. Amani Abeid Amani, ili upatikane uongozi mpya chini ya Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Dkt Ali Mohammed Shein.

Lengo ni upatikane uongozi mpya chini ya Dkt Shein utakaoyatumikia malengo yale yale ambayo yatatumikiwa na uongozi mpya ndani ya Chama cha Wananchi (CUF). Safari hii wanataka kufanya Mapinduzi Kamili ndani ya CCM Zanzibar ifikapo 2012. Nofu jengine hilo la kura za maoni ya wanachama wa CCM linasubiriwa kutetemeshwa miguu na kuvoti “HAPANA.’

Ni rahisi kuona pia kuwa kutakuwa na njama za kuvionyesha vyama vya CUF na CCM udhaifu wa chama cha upande wa pili, ili viongozi ambao wanataka kubebwa juu zaidi waone fursa yao ya kufika wanapotaka kufika itakapowadia 2015. Kumbe zote hizo ni khayali za Dajjal za kutaka kuirudisha nyuma Zanzibar ili ishuke zaidi na ikae chini ya tumbo la chatu.

Ukiangalia kwa undani zaidi utaona kuwa kwa ilivyosukwa na Tanzania Bara, huu muswada wa 2011 ni siafu mweusi, aliyepo chini ya jiwe jeusi, ndani ya giza nene. Ni udanganyifu mtupu ambao hakuna mwenye uwezo wa kuupanga isipokuwa Dajjal mwenyewe na kwa hiyo hata ukifaulu hautodumu, lakini utaimaliza Zanzibar moja kwa moja. Na sisi sote wenye kuisoma barua hii tutakuwa tumeshatangulia alikotutangulia marehemu Janab Ali Baucha.

Na ukiutupia jicho la mbio mbio muswada wa “Sheria kwa ajili ya kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba… “ http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/constituentreview.pdf” (Kiswahili kuanzia Ukurasa 27) kutokea mwanzo mpaka mwisho; na ukavichukuwa baadhi ya vifungu na baadae ukajaribu kuvitengenezea mkufu, basi utaona wazi kuwa sonara wa mkufu huo ni yule yule aliyemo ndani sifa kumi za alama za siku ya mwisho – bingwa wa kudanganya na kupoteza – Dajjal.

Wazanzibari 999 kati ya 1000 wamekabiliwa na hatari ya kudanganywa kwa sababu yule siafu mweusi, chini ya jiwe jeusi, ndani ya giza totoro, hawamuoni, na kwa hiyo hatari kubwa iliyopo mbele hawaioni. Wakulaumiwa ni viongozi (wa dini na wa kisiasa na wa jamii) ambao wana wajibu wa kuwailimisha Wazanzibari kuwa njia iliyobakia ni kuwafuata wale vijana wa Ahlil Kahf na kuukimbia Muungano kabla kidani cha muswada hakijageuzwa kikawa kamba na kitanzi cha kuturejesha kunako Katiba ya 1977.

Kifungu (4) cha Muswada wa Sheria ya kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba kinasema: “Endapo wingi wa kura ya maoni utakuwa ni “HAPANA”, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, itaendelea kutumika.” Maana yake tutarudi kule kule kwenye miaka 47 iliyopita na kwa hiyo itakuwa bora tukajitayarisha kushereherekea miaka 50 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania bila ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na bila ya Jamhuri ya Tanganyika . Waladhaa Liin!!

Na kama wingi wa kura za maoni ya Wazanzibari utakuwa “NDIO” kifungu cha 27 (2) kimeshatuwekea wazi: “Katika utekelezaji wa kifungu kidogo cha (1), Tume ya Uchaguzi Zanzibar itaandaa, kuendesha na kusimamia upigaji wa kura ya maoni, kisha itawasilisha kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi matokeo ya kura zilizopigwa Tanzania Zanzibar kwa ajili ya kutangazwa.”

Tuna njia mbili mbele yetu Wazanzibari. Ya imma tukubali kuanzia hivi sasa kuwa washatumaliza na “mpira umekwisha” na tuendelee kwenye 100% Tanzania . Au tuamue kuiunga mkono 100% ZANZIBARI na tuiongeze miba ya yule myama aliyemezwa na chatu bila ya kumuuwa kwanza na Zanzibar ilipasue tumbo lake, ili ipate haki yake ya kuishi duniani.

Na madam ni dhahiri kuwa Tanzania Bara haitaki kututapika, basi ni dhahiri Zanzibar itabidi ijitapishe au itakufa ndani ya tumbo la Muungano au ndani ya kisima cha Bahari ya Hindi.

Sote kesho tutakuja kuulizwa tuliifanyia nini Zanzibar na vizazi vitakavyokuja . Uamuzi ni wa kila mmoja wetu kujinusuru na huu Muswada wa Dajjal.

Makala ya Aretas Ghassany, 18 Novemba 2011

Advertisements

4 responses to “Muungano, Mswaada na Zanzibar: kamba ya kuvuuka ama kitanzi cha kujitundika?

  1. hawa ccm wa zanzibar wanakosa uzalendoo wa kutetea nchi yaoo mungu upande wake siku zote unashinda wazanzibar tusichoke kudai nchi yetuu mtizameni gadafi mubaraka na rais wa tunis kwa zamani hitla msolini basi urusi ina nguvu la kini muungano wa kisoviet ulisambaratikaa ijekuwa muungano huuu

  2. hata hao cuf na seif wao wanahemukwa na matamasha ya ngoma tu huku wakishiriki katika kuifididi nchi hao wabunge wao ni maviii kwa hiyo iko siku tutakufa ili zanzibar itoke kwenye muungano huuu

  3. Kitakacho tusaidia Wazanzibari kwa sasa ni sisi wenyewe kuamua kujitoa tu ndani ya muungano huu lakini sikupitia kura ya maoni wala katiba tutaishia chini ya walio chini hapa duniani na kesho akhera tutakua mas-uula mbele ya Allah kwa maana hio nawaomba wazanzibar tusijibwete tukategemea viongozi wengi wao wapo kwa maslahi yao binafsi ni vyema tukashirikiana na kujiondoa kwenye udhali huu kwapamoja tutashinda na Mungu atatusaidia

  4. MKOA WA ZANZIBAR NI MALI YA BARA. Walioshiriki mapinduzi ya ZANZIBAR SI WAZANZIBAR NI WATU KUTOKA TANGANYIKA TUNAHAKI YA KUFANYA CHOCHOTE ZANZIBAR. Hata kuwafira wazanzibar wote.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s