Mpango wa haki za watoto wazinduliwa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein

RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein jana alizindua mpango wa miaka mitatu juu ya haki za watoto na kuwataka wadau kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa mpango huo.Aliwaambia wadau wa mpango huo katika mkutano uliofanyika Zanzibar Beach Resort kuwa serikali kwa upande wake imechukua hatua zote muhimu za kufanikisha utekelezaji mpango huo.

Dk Shein alisema hatua hizo ni pamoja na kutunga na kupitisha sheria na sera kwa ajili ya maendeleo ya watoto na kuwalinda dhidi ya vitendo vya aina yoyote vinavyowapora haki yao .

“Sasa hivi Zanzibar kuna sheria ya kulinda haki za watoto, sera mpya ya elimu, uhifadhi na maendeleo ya mtoto, sheria ya ajira mbaya na mwongozo unaowalinda watoto dhidi ya ajira hiyo,” alisema Dk Shein katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Balozi Seif Ali Iddi.

Hata hivyo, alisema licha ya serikali kujenga mfumo wa sheria na sera, bado watoto wanaendelea kukumbana na vitendo vya udhalilishaji na kutumikishwa katika ajira mbaya.

Alisema anaamini ukitekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa wadau, mpango uliozinduliwa utaleta mafanikio katika suala zima la kulinda haki za watoto .

Hatua hiyo, alisema inahitaji ushirikiano mkubwa wa watekelezaji wa mpango huo ambao ni pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Save the Children Tanzania , Shirika la Maendeleo la Kimtaifa la Sweden (Sida) na Jumuiya Ulaya (EU).

Miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi wa mpango huo ni pamoja na Mabalozi wa Sweden na EU nchini, Lennarth Hjelmaker na Tim Clarke.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi Clarke alisema mpango huo unatekelezwa chini ya mradi unaogharamiwa na EU kwa lengo la kuwalinda watoto na kuwaondoa katika ajira mbaya.

Alisema utekelezaji wa mpango huo visiwani Zanzibar utavinufaisha vikundi 50 vya kijamii katika wilaya 9 huko Pemba na Unguja ambako watoto 5,000 pamoja na wazazi wao watashirikishwa katika mafunzo ya elimu ya ufundi.

Balozi Clarke alisema sehemu ya ufadhili huo, EU pia itatoa msaada wa kiuchumi kwa familia 1,000 visiwani Zanzibar katika hatua ya kupunguza udhalilishaji wa watoto.

Habari hii kwa hisani ya Charles Mwankenja

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s