Karibu kwetu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na mgeni wake Mtoto wa Malkia wa Uingereza Prince Charles,mara baada ya kuwasili Ikulu Mjini Zanzibar,akifuatana na Mkewe Camela.(08/11/2011) leo
SERIKALI ya Uingereza imesema itaelekeza misaada yake zaidi katika sekta ya elimu, ikiwemo kutoa walimu kwa ajili ya kusomesha lugha ya Kiingereza Zanzibar. Kauli hiyo imetolewa na mtoto wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Prince Charles wakati alipotembelea kituo cha kufundisha walimu lugha ya Kiingereza huko Bububu nje kidogo ya mji wa Unguja, ambapo aliongozwa na Kaimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman.

Prince Charles alisema Serikali ya Uingereza kwa ujumla imeridhika katika matumizi ya misaada yake katika sekta mbalimbali, ikiwemo maendeleo ya elimu pamoja na ufundishaji wa Kiingereza. “Tutaendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu ikiwemo kutoa walimu kwa ajili ya mafunzo ya Kiingereza,” alisema akiwa amefuatana na mkewe, Camilla.

Mapema, Kaimu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman aliipongeza Uingereza kupitia mashirika yake mbalimbali kwa kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu. “Zanzibar imekuwa ikifaidika na misaada inayotolewa na Uingereza katika sekta ya elimu pamoja na mafunzo ya lugha ya Kiingereza,” alisema Haroun na kuongeza kuwa hali hiyo imesaidia kuwafanya wanafunzi kufaulu vizuri katika baadhi ya masomo ambayo yamekuwa yakifundishwa kwa lugha hiyo.

Mapema, Prince Charles aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume na kulakiwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha, kiongozi huyo alipata nafasi ya kutembelea Mji Mkongwe na maeneo ya jumba la kasri la Mfalme la Beit-el-Jaib na kutembelea wakulima wa mazao ya viungo huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi Unguja.

CHANZO: HABARI LEO

Advertisements

One response to “Karibu kwetu Zanzibar

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s