Zanzibar kushiriki maonyesho ya utalii London

Mkurugenzi Mkuu wa Kanisheni ya Utalii Zanzibar; Ali Khalil Mirza akizungumza na waandishi wa habari, Idara ya habari Zanzibar (MAELEZO)

Na Charles Mwankenja

4th November 2011

Zanzibar itawakilishwa na ujumbe wa watu sita katika maonyesho ya dunia ya soko la utalii yanayoanza leo mjini London, Uingereza, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Ali Khalil Mirza, alisema ujumbe huo utaongozwa na Waziri wa Habari na Utalii, Abdillah Jihad Hassan.

Alisema ujumbe huo unaondoka hapa leo kwenda London ambako uwakilishi wa Zanzibar umeyashirikisha makampuni 16 kati ya 55 yatakayoshiriki kutoka Tanzania.

Alisema wakati wa maonyesho yaitwayo, World Travel Market, nchi za Afrika Mashariki zimetengewa Novemba 9, mwaka huu kuwa siku maalum ya kukuza vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika eneo hilo.

Mirza alisema viongozi wengine waliomo kwenye ujumbe wa Zanzibar katika maonyesho hayo ni pamoja na Mshauri wa Rais wa Zanzibar wa masuala ya Utalii, Issa Ahmed Othman.

Alisema Zanzibar ni mshiriki wa muda mrefu katika maonyesho hayo ya kila mwaka na ya pili kwa ukubwa duniani katika shughuli za utalii.

Juu ya rasilimali za Zanzibar zitakazotiliwa mkazo kuonyeshwa katika maonyesho hayo, Mirza alisema fukwe, utamaduni na amani ni baadhi ya mambo muhimu katika maendeleo ya biashara ya utalii.

Alipoulizwa athari za matukio ya uchomaji moto zaidi ya baa saba kisiwani Unguja katikati mwaka huu na sababu za kamisheni yake kushindwa kutoa tamko, Mirza alisema hayakuleta madhara yoyote kwa mwenendo wa shughuli za utalii.

Hata hivyo, alisema kamisheni ilifuatilia mwenendo huo kujua kama una madhara kwa shughuli za utalii, lakini ilibaini ni msuguano baina ya wenye baa za kawaida mitaani na wakazi wa maeneo hayo wanaopinga biashara hiyo kufanyika katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo.

Mgogoro ulikuwa na sura mbili, jamii haifurahishwi na uwepo wa baa karibu na makazi ya watu, kelele na matendo mengine ambayo ni matokeo ya shughuli za baa, yamesababisha watu kutofurahishwa na biashara hiyo,” alisema Mirza.

Alisema watalii kwa upande mwingine, wanajua mambo ambayo ni tishio kwa usalama wao, ndio maana matukio ya uchomaji moto baa hayakuleta madhara kwa mwenendo wa watalii kutembelea Zanzibar mwaka huu.

Alisema badala yake, idadi ya watalii kutembelea Zanzibar iliongezeka kufikia 125 katika kipindi cha Januari na Septemba, mwaka huu, kulinganisha na 97 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

CHANZO: NIPASHE

Advertisements

One response to “Zanzibar kushiriki maonyesho ya utalii London

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s