Dk Shein atetea kiapo chake

Waandishi wa Habari na Wahariri wa vyombo mbali mbali Bara na Visiwani wakimskiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipozungumza na Waandishi wa Habari wa Bara na visiwani,kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja tokea kushika nafsi ya Urais wa Zanzibar,Ikulu Mjini Zanzibar.

Dk Shein atoboa siri ya kula kiapo Baraza la Mawaziri

Theophil Makunga, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mohamed Shein, amesema aliapa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano kwa kuheshimu Katiba na kuimarisha Muungano.

Dk Shein aliwaambia hayo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye mkutano aliouitisha mjini Zanzibar kuadhimisha mwaka mmoja tangu aingie madarakani baada ya uchaguzi uliofanyika nchini Oktoba 30, mwaka jana

“Nilipoapishwa kuwa Rais wa Zanzibar, niliapa kuilinda katiba na nitailinda kwa nguvu zangu zote nikiwa kiongozi,” alisema Dk Shein.

Rais huyo wa Zanzibar alisema Rais wa Zanzibar anaingia kwenye baraza hilo kulinda maslahi ya Zanzibar katika Serikali ya Muungano na kwamba hata akiwa humo anabaki kuwa Rais wa Zanzibar na si kama waziri asiye na wizara maalumu kama inavyodaiwa na watu wanaopinga hatua hiyo.

Kifungu cha 54 (1) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinasema: …kutakuwa na baraza la mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na mawaziri na kwamba kifungu kidogo (b) cha katiba hiyo kinasema Rais wa Jamhuri ya Muungano ataongoza baraza hilo.

Dk Shein alisema anawashangaa Wazanzibari wanaopinga yeye kuapa kujiunga na baraza hilo kwa sababu yeye si Rais wa kwanza wa Zanzibar kufanya hivyo baada ya katika iliyoruhusu vyama vingi kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

“Mbona mimi siyo wa kwanza kuapa…(rais mstaafu) Karume alifanya hivyo tena mara mbili na mara ya pili ilikuwa mwaka 2006 mimi nilishuhudia na hakukuwa na malalamiko iweje kwangu miye?” alihoji Dk Shein.

Akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja ya serikali yake, Dk Shein alisema amevutiwa sana na moyo wa ushirikiano wa Wazanzibari baada ya kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa na kwamba ana imani kubwa Wazanzibari wakiacha kuendeleza malumbano aliyoyaita yasiyo na tiza, Zanzibar itafika mbali.

“Katika mwaka mmoja tumefaulu kujenga Zanzibar moja, yenye amani na utulivu kinyume na wasiwasi waliokuwa nao baadhi ya Wazanzibari, majirani wetu na watu wengine ambao walikuwa na mashaka makubwa ya utekelezaji wa serikali ya umoja wa kitaifa,” alisema..

Dk Shein aliwaambia wahariri hao kuwa ingawaje serikali yake inaonekana na watu kuwa kubwa yenye makamu wa rais wawili na mawaziri katika wizara 16, alisema gharama ya kudumisha amani katika nchi haiwezi kulinganishwa na kiasi cha fedha kinachotimika kuendesha serikali.

Akitoa tathmini ya utawala wake katika kipindi cha mwaka mmoja, Dk Shein alisema kuwa, alitembelea wilaya zote kumi na mikoa mitano katika visiwa vya Unguja na Pemba na kufanya mikutano na wizara zake zote ili kujiridhisha na mipango ya utekelezaji wa shughuli zao na kubaini kwamba, kuna matumaini makubwa ya visiwa hivyo kusonga mbele.

“Malengo yetu katika miaka mitatu ijayo, Zanzibar itapunguza kwa asilimia 50 uagizaji wa mchele toka nje,” alisema Dk Shein.

Zanzibar yenye idadi ya watu 1.3 milioni sasa inahitaji tani 80,000 za mchele kukidhi mahitaji ya nafaka hiyo kwa ajili ya matumizi yake na kwamba wakati kipindi hiki kinamalizika, anaona kuna uwezekano mkubwa wa kufikia lengo hilo kwa sababu ameanza kuona dalili. Idadi ya Wazanzibari baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 ilikuwa watu 320,000.

Inakisiwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Zanzibar wanategemea moja kwa moja kuununua chakula ili kukidhi mahitaji yao ya chakula ya kila siku, huku uzalishaji wa mchele ukiwa ni tani 16,000 ambayo ni sawa na asilimia 16 tu ya mahitaji ya nafaka hiyo.

Akizungumzia jitihada za Serikali yake katika kuimarisha sekta ya uchumi, Dk Shein alisema wameanza kuimarisha vyama vya ushirika kwa kutoka mikopo kwa vyama hivyo, vyama vya kuweka na kukopa (saccos) na wajasiriamali mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja, tumewafikia watu 6803 ambao ni wanachama wa Saccos 11, huku Saccos nane ziko katika visiwa vya Unguja na tatu visiwani Pemba…hii ni mbali na kuongeza ajira kwa vijana,” alisema.

Kuhusu afya, Dk Shein alisema kama alivyoahidi katika kampeni zake alipokuwa akigombea nafasi hiyo, ahadi yake ya kuipandisha daraja hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa iko palepale na kwamba mipango iko tayari kutekeleza ahadi hiyo. Hivi sasa Zanzibar haina hospitali ya rufaa.

Kuhusu elimu tayari serikali yake imejenga shule 16 za wilaya kama alivyoahidi kuwa angejenga shule 21za aina hiyo ili kuinua kiwango cha elimu visiwani hapa kwa kutilia mkazo masomo ya sayansi na kwamba, shule hizo zinatarajiwa kumalizika ifikapo mwaka ujao.

Dk Shein ameahidi kuzungumza na wahariri kila baada ya miezi mitatu ili kuwafahamisha wananchi Serikali yake inafanya nini kila inapowezekana.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements

2 responses to “Dk Shein atetea kiapo chake

  1. a alaykum kwanza napenda kutowa pole kwa kifo cha mzee wetu kwa jina la kwetu tunamwita ka badawy na huyu ni na mm ni kwangu ni mjomba yangu yeye na mama yangu ni ndugu mungu amlaze pahali pema amin na nawpa pole ndugu zangu naninao wajuwa na nisowajuwa kwani sababu mm nipo mbali nawao naomba mungu inshaallah tutakuja kuonana kwakaribu amin mungu amuweke pahali pema peponi amin

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s