Zanzibar yaomba msaada wa nishati

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKA LA UWEKEZAJI VITEGA UCHUMI NCHINI MAREKANI (OPIC) BI MIMI ALEMAYEHOU; NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR DK. SIRA UBWA MAMBOYA NA KULIA NI WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR FATMA ABDUL-HABIB FEREJ.

ZANZIBAR imeshauriwa kulitumia vyema soko la Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza uchumi wake na kuondokana na kutegemea zao moja la karafuu kama mhimili mkuu wa Taifa.Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la uwekezaji Vitega Uchumi la Kimataifa Nchini Marekani (OPIC) Bi Mimi Alemayehou wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Washington DC Nchini Marekani.

Bi Mimi alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake ulioko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ya kuitangaza Zanzibar kwa wawekezaji kuwekeza Zanzibar kwamba Shirika hilo tayari limeshaandaa mpango wa kuwekeza ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki likilenga kusaidia eneo hilo Kiuchumi.

Alisema mpango huo una nia pia ya kuijumuisha Sudan ambayo imekuwa ikikabiliwa na ukame wa mara kwa mara licha ya kwamba haimo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ).

“Tumelenga zaidi kuisaidia Sekta Binafsi kwa vile jamii kubwa hasa ndani ya Bara la Afrika imekuwa ikikabiliwa na Uchumi duni, nadhani kwa kuwa na nia hiyo ya kusaidia bara la Afrika nchi hizo zitafaidika ”. Alisema Bi Mimi Alemayehou.

Bi Mimi alifahamisha kwamba huduma za Shirika hilo la OPIC mara kadhaa huelekezwa katika kutoa huduma za kijamii kwenye sekta binafsi kupitia Makampuni ya Kimarekani Chini ya Shirika la Misaada la Marekani USAid.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi ameuambia Uongozi wa Shirika hilo la Uwekezaji Vitega Uchumi la OPIC kwamba Zanzibar bado inaendelea kutegemea zao moja tu la Uchumi la karafuu.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko katika harakati za kuimarisha miundombinu ili kuyawezesha Makampuni ya Kigeni kupata fursa ya kuwekeza Zanzibar.

Alisema wawekezaji katika Sekta ya Utalii wana nafasi nzuri ya uwekezaji kwa vile miundombinu ya barabara, maji na umeme iko katika hatua nzuri hivi sasa.

Hata hivyo Balozi Seif ameuomba Uongozi wa OPIC kuangalia uwezekano wa kuanzisha mradi wa pamoja wa umeme kwa kutumia Nishati ya jua au Bahari ili Zanzibar iwe tayari kukabiliana na upungufu wa huduma ya umeme hasa wakati kinapopungua kina cha maji huko Tanzania Bara.

“Tumekuwa tukipokea huduma ya umeme kupitia gridi ya taifa huko Tanzania Bara, lakini wakati mwengine tunalazimika kupata umeme wa mgao kutokana na kupungua kwa kina cha maji. Hali hii huathiri utendaji kazi na kupunguza kasi ya Maendeleo ya Kiuchumi ”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Balozi Seif Iddi.

Balozi Seif Idd yupo ziarani kikazi Marekani akifuatana na ujumbe kutoka Zanzibar akiwemo Naibu waziri wa Afya, Dk Sira Ubwa na waziri wa ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej ambapo wameshatembea na kuonana na taasisi mbali mbali hivi sasa kwa lengo la kuitangaza Zanzibar kiuchumi.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
3/11/2011.

Advertisements

2 responses to “Zanzibar yaomba msaada wa nishati

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s