Wizara ya Afya Z’bar kuwekwa kiti moto Pemba leo

Rais wa Zanzibar na Mwwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipokea Cheti cha shukurani,kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya watu wa zanzibar na mshauri wa Rais uwezeshaji wananchi kiuchumi,Mhe, Abrahmani Mwinyijumbe,wakati wa uzinduzi wa Tawi la Bnki ya Watu wa Zanzibar,PBZ Pemba jan. (31/10/2011)

 

RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein leo atakuwa na ziara ya siku moja kisiwani Pemba ambako pamoja na mambo mengi atafungua jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na mkutano mkuu wa mwaka wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya.

Dk Shein atawasili kisiwani humo asubuhi na kulakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Chake na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba , Juma Kassim Tindwa.

Juu ya ufunguzi wa tawi la PBZ, Mkurugenzi Mtenbdaji wa benki hiyo, Juma Amour Mohammed alisema jengo jipya litakalofunguliwa na Rais Shein lipo katika tawi la Chake Chake na kwamba uzinduzi wa tawi hilo utafanyika saa tatu asubuhi.

Alisema ufunguzi wa jengo hilo la tawi la Chake Chake utafuatiwa na uzinduzi wa huduma zinazotolewa na PBZ kwa kutumia mfumo wa benki za Kiislamu.

Juma alisema tawi la Chake Chake ni la pili kwa upande wa Zanzibar kuwa na huduma za aina hiyo na kwamba PBZ pia imo katika hatua ya mwisho ya maandalizi ya kuanza kutoa huduma kama hiyo katika tawi lake lililopo Dar es Salaam kuanzia mwezi ujao.

Alisema kwa upande wa huduma za mfumo wa kawaida, PBZ ina matawi matano Zanzibar na moja Tanzania bara, yote kwa pamoja yakiwa na jumla ya wateja 135,000.

Juu ya hatua nyingine ya ziara ya Rais Shein kisiwani Pemba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Saleh Mohamed Jidawi atafungua mkutano wa mwaka wa wafanyakazi wa wizara hiyo utakaowashirikisha wadau 130 wa sekta ya afya.

Alisema wadau hao ni wawakilishi wa nchi kadhaa na mashirika mbali mbali yanayochangia gharama za maendeleo ya sekta ya afya visiwani humo ambayo ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa kawaida miongoni mwa kazi kubwa za mkutano huo ni kutathimini mafanikio na matatizo yanayoikabili sekta hiyo katika ngazi mbali mbali ya utoaji huduma ya afya kwa jamii.

Mkutano wa mwaka huu unafanyika wakati hospitali nyingi na baadhi ya zahanati na vituo vya afya visiwani vinakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa na vifaa muhimu pamoja na upungufu mkubwa wa wafanyakazi, hasa madaktari bingwa.

Mbali na upungufu wa madaktari bingwa, Hospitali ya Rufaa ya Mnazimoja pia haina wataalamu wa kusoma na kujua matokeo ya vipimo vinavofanyika kwa kutumia mashine aina ya CT Scan.

Ukosefu wa wataalam hao na mpango wa wagonjwa kuchangia gharama za vipimo hivyo, kuuziwa vichupa vya kuwekea mkojo kwa ajili ya kupima, ni miongoni mwa matatizo yanayotarajiwa kuibua mjadala mkali wakati wa mkutano huo.

Na Charles Mwankenja

SMZ kuepusha vifo kwa watoto na wajawazito

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein amesema Serikali itahakikisha inapambana na maradhi yote hatari ambayo yamekuwa yakisababisha vifo ikiwemo vya watoto na wajawazito. Dk. Shein alisema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wizara ya Afya kisiwani Pemba na kusema mikakati ya Serikali kuwapatia afya na matibabu kinamama na watoto ipo pale pale.

“Tumejizatiti kuwapatia wananchi wetu afya bora ya uhakika ikiwemo ya kinamama na watoto kwa ajili ya kuepukana na vifo,” alisema Dk. Shein.

Alisema Zanzibar imo miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya akinamama na watoto kwa asilimia 25 na kusema lengo hilo litafikiwa zaidi ifikapo mwaka 2020.

Dk. Shein alisema mpango wa kupunguza vifo vya kinamama na watoto uliozinduliwa miaka miwili iliyopita, umepata mafanikio ambapo sasa kinamama wanajifungua katika vituo vya afya vinavyotambuliwa na Serikali.

Aidha, Dk. Shein alichukua nafasi hiyo kuwapongeza washiriki wa maendeleo ambao wamekuwa wakisaidia huduma za afya nchini mjini na vijijini. Alisema juhudi hizo zimekuwa chachu ya mafanikio makubwa katika tiba ya wananchi wengi na kuondokana na tatizo la maradhi pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.

“Tunawapongeza kwa dhati washirika wa maendeleo ambao wamekuwa nasi bega kwa bega katika kutupatia matibabu na ushauri katika sekta za afya Unguja na Pemba,” alisema.

Aliupongeza uongozi wa Wizara ya Afya kwa kufanya mkutano huo katika Kisiwa cha Pemba, hatua ambayo inaonesha wazi kwamba sasa wizara imedhamiria kushughulikia na kupeleka maendeleo sehemu zote.

Mapema Waziri wa Afya, Juma Duni Haji alisema wizara ipo katika mikakati ya kupambana na kuzuia maradhi yote ambayo yamekuwa yakisababisha vifo ikiwemo malaria.

Alisema kwa mfano, ugonjwa wa malaria sasa umepungua kwa asilimia 1.8 huku baadhi ya hospitali za Unguja na Pemba zikikosa wagonjwa wa aina hiyo.

Kuhusu ugonjwa hatari wa Ukimwi, Duni aliitaka jamii kubadilika na kuachana na kufanya vitendo vya ngono ambavyo ndiyo chanzo kikubwa cha maambukizi ya maradhi hayo.

Mkutano huo wa siku tatu lengo lake kubwa ni kufanya tathmini ya maendeleo ya sekta ya afya kwa kuwashirikisha washirika wa maendeleo wanaosaidia sekta ya afya.

CHANZO: HABARI LEO
Advertisements

One response to “Wizara ya Afya Z’bar kuwekwa kiti moto Pemba leo

 1. post ya ukatibu mkuu jidawi haiwezi kwa sababu uwezo wake wa health management ni finyu hata kama ni daktari bingwa.

  unazungumzia madaktari bingwa zanzibar??????????? mshangao kwangu kwani zanzibar haitimizi madaktari 10 { 10 MD holders }
  Anyway twende hivyo hivyo.
  ali shein pia hana uwezo wa kuwa rais ni ile tu kwamba utulivu wa kisiasa na ccm ilitaka rais wa zanzibar atoke kisiwa cha pili
  bahati yake; lakini angalia ana fikra gani dhidi ya maendeleo ya zanzibar; kila kitu kaacha vile vile.
  vijana wenye elimu na new vision hawapewi nafasi. mawaziri ,wakuu wa mikoa ni wale wale.
  shein hana confidence wala thoughts in zanzibar’s future plan in development especially in education, health and agriculture.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s