Kichaka cha Mfumo Kristo

Maalim Seif na Dk Shein

Kichaka cha Mfumo Kristo, kupigwa kiberiti Zanzibar,*Maridhiano yafungua mlango wa kheri,*Rais Shein, Seif wapewa changamoto

Muungano umetajwa kama kichaka unakojificha mfumo kristo kuiburura Zanzibar katika idhilali kwa kuipora nguvu zake za kisiasa na kiuchumi na kubwa zaidi kuhujumu Uislamu na Waislamu.Ni kutokana na sababu hiyo imeelezwa kuwa ndio sababu muungano limefanywa jambo nyeti sana na mwiko kuuhoji.

Hayo yamebainishwa katika kongamano lililofanyika katika eneo la Markaz Tabligh, Ole Kianga, Pemba Jumapili Oktoba 2, 2011.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za Pemba, lilijadili hatari ya mfumo kristo kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Awali mtoa mada Sheikh Ilunga Hassan Kapungu alisema kuwa, inaweza kuwa jambo lisiloeleweka ukizungumzia mfumo kristo kwa vile takriban viongozi wote wa serikali na taasisi muhimu ni Waislamu, Wapemba na Waunguja.

Hata hivyo akasema kuwa, ile kuwa inaitwa ni serikali ya Zanzibar haina maana kuwa serikali hiyo ni serikali inayoongoza dola kwani mamlaka yote ya kisiasa yapo katika serikali ya muungano.

Na hivyo, kwa vile serikali ya muungano imeshikwa na Wakristo kwa takribani asilimia 89, na kwa vile imeshathibiti kwamba nchini kuna mfumo kristo unaopendelea Wakristo na kuhujumu Uislamu, basi mfumo huo unaihujumu pia Zanzibar kupitia muungano.

Akifafanua alisema kuwa yapo mambo ambayo Wazanzibari wangetaka kufanya au kuamua kwa masilahi ya nchi yao, lakini hawawezi kuyafanya kwa vile muungano umewapora nguvu za kisiasia.

Na kwamba, yale mamlaka ya kidola na kisiasa ya Zanzibar yalizikwa na kusomewa talakini siku ASP ilipoungana na TANU ambapo CCM ilishika hatamu na maamuzi yote muhimu kuwa yanafanyika Dodoma.

Akitoa mfano alitaja uchaguzi mkuu ambapo jina linalopitishwa kugombea Urais laweza kuwa lile ambalo halikupata ridhaa ya Wazanzibari.

Na hata kuondoka madarakani, kiongozi anaweza kuondolewa bila ya Wazanzibari wenyewe waliompigia kura au vyombo vyao vya uwakilishi kama Baraza la Wawakilishi kuhusishwa.

Ukatajwa mfano wa Mzee Aboud Jumbe aliyekwenda mkutanoni Dodoma akiwa Rais akarudi Urais akiwa ameuacha Dodoma.

Sheikh Ilunga kwa kutoa mfano huo alisema kuwa Alhaj Aboud Jumbe, yalimfika kwa sababu alihoji muungano na kuhoji kwenyewe si kutaka kuuvunja, bali kutaka uwe wa haki.

“Yalimfika.” “Kwa nini?” “Kwa nini imefanywa kuwa mwiko kuhoji muungano?” Alisema na kuhoji Ilunga.

Kabla ya kutoa jawabu, Sheikh Ilunga alirejea pia hali ilivyokuwa wakati wa Mzee Abeid Aman Karume ambaye alishaonesha kuwa koti la muungano linambana, lakini mauti yakamfika muda mfupi kabla ya kutimiza nia yake ya kulivua.

Aligusia pia yaliyomfikia Maalim Seif Shariff Hamad, hata hivyo hakutaka kufafanua bali akawataka Wazanzibari wenyewe wamuulize Maalim nini kilimkuta na kwa nini.

Katika kukamilisha hoja yake akasema kuwa muungano umefanywa jambo nyeti na mwiko kujadiliwa kwa sababu ndio uchochoro na kichaka mfumo kristo unakopitia kuiua Zanzibar na kuuwa Uislamu.

Katika hali hiyo akasema kuwa, Wazanzibari watakuwa wakiwalaumu na pengine hata kuwachukia bure viongozi wao, lakini nao wanashindwa kufanya yanayotakiwa na Wazanzibar kwa sababu inabidi kwanza watizame Dodoma inasema nini.

Kwa maana kuwa jambo kama halijapata ridhaa ya mfumo kristo, haliwezi kuwa kama ambavyo haikuweza Zanzibar kujiunga na OIC na hivi sasa Tanzania haiwezi kujiunga na jumuiya hiyo kwa sababu maaskofu hawataki, mfumo kristo hautaki.

Pamoja na hali hiyo, Sheikh Ilunga aliwataka Wazanzibari kutokukata tamaa, bali watumie fursa zilizopo kurejesha hadhi yao.

Kwanza hadhi ya Uislamu na pili hadhi ya nchi yao na dola yao ambayo awali ilikuwa na kiti Umoja wa Mataifa.

Alisema kuwa, Wazanzibar ni lazima watumie maridhiano ya kisiasa yaliyopo kuleta maridhiano ya Kiislamu.

Kwamba amani iliyopo itumike kuimarisha udugu wa Kiislamu, watu wajitambue kwamba wao ni Waislamu kwanza kabla ya jambo jingine, ni Waislamu kabla ya CUF na CCM na ni Waislamu kabla ya kuwepo Tanzania na muungano wake.

Akasema hilo linahitaji Da’wah ya kutosha na watu warejee katika Qur’an waone na kutafakari jinsi Mwenyezi Mungu anavyowaonya juu ya kuwafanya Mayahudi na Manasara kuwa marafiki na wasiri wao.

Akawakumbusha pia kuwa Qur’an imesema wazi kwamba chuki iliyofichwa na Manasara ndani ya vifua vyao ni kubwa mno kuliko wanayoidhihirisha na kwamba hawataridhia mpaka wawaritadishe Waislamu, japo wabakie Waislamu wa majina lakini makafiri kwa kauli, vitendo na maadili.

Ukiacha fursa ya kuwepo maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa, Ilunga ametaja fursa nyingine kuwa ni mabadiliko ya katiba yanayokuja.

Akasema, ni lazima fursa hiyo itumike vizuri kuhakikisha kuwa kichaka kinachoficha mfumo kristo kinapigwa moto.

Na hiyo itafanyika kwa kuwa na muungano wa haki ambapo pande mbili za muungano, Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na haki sawa, sio huu wa serikali ya Tanganyika kujivika joho la serikali ya Tanzania.

Muungano ambao utairejeshea Zanzibar nguvu zake za kisiasa, kiuchumi, nguvu kazi na ulinzi.

Ilunga akamalizia kwa kuwapa changamoto viongozi wa serikali ya Zanzibar, Rais Ali Mohammed Shein, na Makamo wake wawili, Maalim Seif Shariff Hamad na Balozi Seif Ali Iddi kwamba wao wametoka katika migongo ya wazee wa Kiislamu na hivyo, hawawezi kukwepa jukumu la kuona hadhi ya Uislamu inarudi kama ilivyokuwa wakati wakilelewa na wazee wao.

MWISHO

Zanzibar inaadhibiwa; *Salama yake irudi katika Qur’an

 

Imeelezwa kuwa madhila yaliyowakuta Wazanzibari toka mapinduzi, muungano na kuingia mfumo wa vyama vingi, yaweza kuwa ni adhabu na matokeo ya kutupa Uislamu.Adhabu hiyo ndiyo inawakuta pia Waislamu wa Tanzania Bara ambao kama ilivyokuwa Waislamu wa Zanzibar waliweka uzalendo mbele wakaweka Uislamu nyuma wakati wenzao walioshikilia Mfumo Kristo, Biblia mbele Utanzania baadae.

Hayo yamebainishwa katika kongamano la Ole Kianga ambapo mtoa mada amesema kuwa heshima ya Waislamu haiwezi kurudi mpaka warejee kule kule walikojikwaa na kujirekebisha.

Akitoa mada katika kongamano hilo lililofanyika Jumapili iliyopita Oktoba 2, Sheikh Ilunga amesema kuwa Zanzibar ilikuwa Dola iliyosambaa pwani yote ya Afrika Mashariki, lakini imebomolewa na Mfumo Kristo na kubaki visiwa vya Pemba na Unguja.

Amesema, hata hiyo Pemba na Unguja yenyewe, imehujumiwa na kupoteza kabisa nguvu zake za uchumi, siasa na maadili yake.

Amekumbusha kuwa wakati toka ujio wa akina Vasco da Gama ilikuwa Ukristo mbele, Waislamu walipambana kuondoa ukoloni wakiweka uzalendo mbele na kutupa mafundisho ya Qur’an kwa hiyo baada ya kupata uhuru wakawa wameruhusu kudhibitiwa na Mfumo Kristo.

Mifano ilitolewa jinsi Waislamu walivyojitolea kupigania uhuru, lakini wakighafilika na mafundisho ya Qur’an yaliyowataka kuchukua hadhari zao juu ya Mayahudi na Manasara.

Katika kughafilika huko, walimwamini kila mtu hata wale waliokuwa maadui wao wa wazi.

Sheikh Ilunga alisema kuwa hata pale ambapo maadui wa Uislamu walijitokeza wazi wazi na kuonesha makucha yao, walioparurwa hawakupata watetezi kutoka kwa Waislamu.

Alitaja masaibu yaliyomkuta Sheikh Suleiman Takadiri, Sheikh Hassan Bin Ameir, Chifu Saidi Abdallah Fundikira na Profesa Kighoma Ali Malima.

Alisema, wakati ilijitokeza wazi kuwa mikasa iliyowakuta Waislamu hao ni kutokana na kuhoji kwao mfumo kristo, Waislamu hawakuzinduka na kuwatetea.

Alisema hali ni hiyo hiyo kwa Zanzibar ambapo kwa kutupa Uislamu waliruhusu kugawanywa kwa ufuasi wa kivyama na kujengewa chuki.

Katika hali hiyo wamekuwa wakiishi katika hofu na uadui ambapo maadui nao walitumia mwanya huo kuzidi kuwadhuru.

Ilitajwa hali ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita ambapo kutokana na hali ilivyotengenezwa ionekane ya hatari, askari wengi walikuwa wakimwagwa Pemba na Unguja, wengi wakitoka bara.

Ilunga alisema kuwa askari wenyewe walifanywa kuamini kwamba Wapemba ni watu hatari kwa hiyo walikuwa na silaha zao tayari tayari mkononi kujihami na kushambulia, matokeo yake ni kuuliwa watu na kujeruhiwa hasa kila unapofika wakati wa uchaguzi.

Kutokana na hali hiyo, Waislamu na Wazanzibari wametakiwa kurejea mwongozo wa Qur’an unasemaje juu ya Mayahudi na Manasara.

Aidha, wametakiwa kurudi katika Uislamu na ni kwa kupitia Uislamu wanaweza pia kuondoa uchafu uliokwisha kuingia kupitia utalii.

HABARI HIZI NI KWA HISANI YA GAZETI LA ANNUUR
Advertisements

2 responses to “Kichaka cha Mfumo Kristo

 1. Nimeipitia tena historia ya biashara ya watumwa, nikaona ilikuwa inaendeshwa na mtandao au mfumo ulioenea kutoka Congo na Malawi kupigia Bagamoyo na Zanzibar, hadi Arabuni na nchi za Ghuba. Waliouunda na waliokuwa wanaendesha mfumo huo ni waArabu, wote wakiwa ni waIslam. Je, tuseme kuwa biashara ya watumwa ilikuwa ni ya mfumo Islam?

  Halafu, huko Visiwani kulikuwa na utawala wa masultani, kwa miaka mingi. Hao walioendesha utawala ule walikuwa ni waIslam. Je, tuseme kuwa usultani ulikuwa ni mfumo Islam?

  Nauliza masuali haya kwa sababu nimewahi kupinga dhana ya mfumo Kristo, kwa msingi kwamba kama tunaongelea maovu au mfumo wa maovu, hauwezi kuwa mfumo Kristo, kwani ni mfumo unaokiuka maadili ya dini ya u-Kristo. Makala niliyoandika ni hii hapa. Lakini watu wameng’ang’ania tu kutumia neno mfumo Kristo.

  Kutokana hilo, napaswa kuuliza kama nilivyouliza hapa juu: Je tuseme kuwa biashara ya watumwa ilikuwa ni kazi ya mfumo Islam? Na je, usultani Visiwani ulikuwa ni mfumo Islam?

  Mimi ninavyoamini ni kuwa dhana ya mfumo Kristo ni lazima iwa na maana ya mfumo ambao kweli unafuata maadili ya dini ya u-Kristo, si vingine. Na ukisema mfumo Islam, ni lazima uwe ni mfumo unaofuata maadili ya u-Islam. Si vingine. Huwezi ukakuta mtandao wa majambazi au wahujumu wa haki za wengine, halafu mtandao huo ukauita mfumo Kristo, au mfumo Islam.

  Nangojea majibu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s