Hoja binafsi ya mikopo ya elimu ya juu yawasilishwa

Mwakilishi wa viti maalumu vya wanawake (CCM) Mgeni Hassan Juma

MWAKILISHI wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma amewasilisha hoja binafsi inayoitaka Serikali kulifanyia kazi suala la ukosefu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wanafunzi wa Zanzibar.Zaidi ya wanafunzi 3,000 wa Zanzibar walioomba mikopo elimu ya juu mwaka huu wamekosa kupata na hivyo kushindwa kuendelea na masomo yao hali ambayo imezusha malalamiko makubwa miongoni mwa wanafunzi hao na wazazi wao.

Juma aliwaeleza wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba ukosefu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wanafunzi kutoka Zanzibar ni tatizo kubwa ikiwa ni kero kwa wanafunzi pamoja na wazazi wao..

Alisema wakati umefika sasa kwa Serikali kulishungulikia suala hilo kwa kutafuta vyanzo vya fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma elimu ya juu.

‘Hili tatizo sasa limekuwa la kitaifa kwa sababu wanafunzi wengi sasa wamekosa mikopo ya elimu ya juu huku wakiwa hawana la kufanya, familia maskini zinakosa kuwasomesha watoto wao kwa sababu wanakosa mikopo serikalini ‘alisema Mwakilishi huyo ambaye ameanza kupata umaarufu kutokana na misimamo yake dhidi ya serikali.

Aidha Juma aliibana Serikali na kuitaka kupunguza matumizi yake yaliopo katika bajeti ya Serikali ikiwemo mafungu ya safari za viongozi wakuu wa kiserikali ambapo zaidi ya shilingi bilioni 24 zimetengwa kwa ajili ya safari hizo wakati wanafunzi wakikosa kuendelea na masomo yao.

Mwakilishi huyo pia ameitaka serikali kufanya harambee (michango) ambayo itakusanya fedha kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi wa elimu ya juu mikopo na kuendelea na masomo yao na kuondokana na tatizo hilo.

Alisema zipo taasisi kubwa za fedha ikiwemo mfuko wa hifadhi ya jamii wa Zanzibar (ZSSF) ambao unahitaji kushirikishwa katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo la wanafunzi na kwa maoni yake haoni sababu ya kutofanyika michango na taasisi hizo kutoshirikishwa.

Wakichangia hoja hiyo Mwakilishi wa viti maalumu kutoka (CCM) Mgeni Hassan Juma alisema kwamba Serikali bado haijawa makini kiasi kikubwa katika kukabiliana na tatizo la ukosefu wa wanafunzi kupata mikopo ya elimu ya juu wakati kila mmoja anafahamu umuhimu wa suala hilo la kupata elimu kwa wanafunzi.

‘Mheshimiwa Spika bado Serikali haijajipanga vizuri kukabiliana na tatizo hilo ambalo limekuwa kero majumbani mwetu kwa watoto wetu pamoja na wazazi kwa ujumla, kwani kila mara unasikia watoto wakilalamikia suala hilo huku siku zikisonga mbele watoto wetu wanakosa elimu wakati wengine wanaendelea na masomo yao’ alisema Mwakilishi huyo.

Mgeni alisema wanafunzi wengi wanakosa mikopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu lakini wanazo sifa zote za kufanya hivyo ikiwemo wanafunzi wanawake, ambao wangepeswa kupatiwa kipaumbele ili waweze kuendelea na masomo yao kwani kuwaacha ni kuwanyima haki ya msingi ya kupata elimu.

Aidha aliitaka Serikali kufanya mawasiliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na nafasi ya wanafunzi wa Zanzibar kupata mikopo hiyo zaidi wale wenye sifa za kuendelea na masomo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s