Dk Shein apongezwa na CCM

Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar; Issa Haji Ussi akizungumza na waandishi wa habari Kisiwandui.

CCM yampongeza Dk Sheni mwaka mmoja madarakani.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimempongeza rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kwa kutimiza mwaka mmoja kuwepo madarakani huku akifanikiwa kwa asilimia kubwa kutekeleza ilani ya chama hicho.Kauli hiyo imetolewa na katibu wa idara ya itikadi na uenezi ya chama cha Mapinduzi Zanzibar, Issa Haji Ussi wakati akizungumza na waandishi wa habari hapo ofisi kuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa.

Dk.Shein alikula kiapo cha utii na uaminifu Novembar 3 mwaka jana na kuwa rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mfumo wa umoja wa kitaifa, ambapo ni mara ya kwanza toka kurejeshwa kwa mfumo wa vyama nchini Zanzibar kuunda serikali iliyovishirikisha vyama vya upinzani. 

 Ussi alisema rais Dk.Shein aligombea nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi na hatimaye kuibuka kwa ushindi kwa asilimia 50.1 na kuapishwa kushika madaraka katika Serikali ya kwanza ya mfumo wa umoja wa kitaifa.

Lakini alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kushika madaraka hayo,amefanya kazi kubwa katika kutekeleza ahadi zote ziliomo katika ilani ya uchaguzi ambazo alizinadi katika kipindi cha kampeni cha chaguzi mkuu mwaka jana.

‘Ndiyo maana chama cha Mapinduzi kimepanga kufanya sherehe kubwa za kutimia mwaka mmoja tangu mgombea wake kushika madaraka ya dola na kutekeleza ahadi ziliomo katika ilani ya uchaguzi mkuu’ alisema Ussi mbele ya waandishi wa habari.

Alizitaja baadhi ya ahadi alizofanikiwa kuzitekeleza ikiwemo kulipandisha hadhi zao la Karafuu na kuwafanya wakulima kupata faida asilimia 80% ya bei ya karafuu inayouzwa. ‘Wakati Dk.Shein anaingia madarakani zao la karafuu lilidharauliwa na wakulima wenyewe huku mikarafuu ikikatwa na kufanywa kuni…..sasa bei ya karafuu imepanda na wakulima kujipatia fedha nyingi’ alisema Ussi.

Aidha Alisema Dk,Shein alipoingia madarakani alitangaza mapinduzi ya kilimo na kufanikiwa kwa asilimia kubwa ikiwemo kupunguza bei ya pembejeo kwa wakulima katika mazao muhimu ikiwemo ya mpunga. Lakini Ussi alisema kwamba Dk Shein tangu kushika madaraka mwaka mmoja sasa amekuwa muaminifu kwa kutekeleza ahadi za kiapo chake cha kuunda serikali yenye sura ya umoja wa kitaifa, ambayo ipo madarakani ikiwatumikia wananchi.

‘Ndiyo maana Chama cha Mapinduzi kimeona ipo haja yakufanya sherehe kubwa ya kumpongeza kwa kipindi cha mwaka mmoja kuwepo madarakani na kuongoza dola lakini pia mafanikio yaliopatikana katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja ‘alitamba Ussi.

Habari hii kwa hisani ya Khatib Suleiman

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s