Taarifa ya kamati ya kusimamia viongozi

WAZIRI Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee akimsiliza Waziri wa Maji Ujenzi Ardhi na Maendeleo ya Makazi Ali Juma Shamuhuna, wakiwa nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi liliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

TAARIFA YA KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA KUSIMAMIA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA JUU YA TUKIO LA KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDERS I ILIYOTOKEA TAREHE

10.09.2011 KATIKA ENEO LA MKONDO WA BAHARI YA NUNGWI, ZANZIBAR

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kukutana tena mbele ya Baraza lako tukufu tukiwa wazima wa afya ili kujadili mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Pia napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Serikali kwa kuwasilisha taarifa inayohusiana na tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islanders I iliyotokea katika mkondo wa bahari ya Nungwi, Zanzibar, mnamo tarehe 10.09.2011. ni mwezi mmoja hivi sasa lakini bado tunakumbuka tukio hilo la kihistoria ambalo hatutoweza kulisahau maishani mwetu. Wazanzibari sote.

Mheshimiwa Spika, Aidha kwa niaba ya kamati nakushukuru wewe binafsi kwa kuniruhusu kusimama mbele ya Baraza lako tukufu ili niwasilishe taarifa ya kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa juu ya tukio hilo la maafa.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya kamati, nachukua fursa hii kumuomba Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi wale wote waliofariki kutokana na ajali hiyo, na pia kuwataka kuwa na subira wale wote waliopoteza ndugu na jamaa zao. Pia wale walionusurika katika ajali hiyo na kuwatakia afya njema na pia waliopata matatizo ya mshituko kutokana na tukiou kiafya tunawaombea Mwenyezi Mungu awape afueni ili tuweze kujumuika nao na kuweza kuendelea na majukumu ya kujenga Taifa letu.

Mheshimiwa Spika,Sisi Wajumbe wako wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wewe mwenyewe binafsi tulipata mshtuko mkubwa usiku wa manane wa kuamkia tarehe 10.9.2011 wakati tuko safarini kikazi huko mjini Arusha. Baada ya kupokea simu kutoka kwa watu mbali mbali kuhusu tukio hilo kubwa la aina yake kwa hapa Zanzibar kwa kweli hakuna aliyeamini taarifa hizo na tulianza kupiga simu huku Zanzibar kwa watu tofauti ili kupata uthibitisho huo.

Baada ya kupata uthibitisho wa ajali hiyo tulipigiana simu katika mahoteli mbali mbali tuliofikia ukiwemo wewe mwenyewe ili kujuulishana yaliyotokea Zanzibar na baadae kwa busara zako ukaamua tuahirishe safari na turudi Unguja alfajiri hiyo hiyo.

Mheshimiwa Spika,Baada ya Waheshimiwa Wajumbe kuanza kupata taarifa Kwenye mahoteli tofauti tuliofikia vilio vilitawala kwenye mahoteli yetu na hata aliyekuwa sagu machozi yalimtoka,waliorudi kwa mabasi vilio vilitawala kutoka Arusha hadi Dar es Salam kwani kila mmoja alikuwa na fikra tofauti hajui nani alikuemo kwenye meli hiyo ama ndugu,jamaa au rafiki, Mheshimiwa Spika,sisi wengine nikiwemo mimi mwenyewe binafsi pia nilipata simu kutoka kwa ndugu zangu kwamba ndani ya meli hiyo alikuwemo mtoto wa shangazi yangu yeye pamoja na watoto wake watatu walikuwemo katika meli hiyo wakitokea Unguja kurudi nyumbani kwao Pemba na hadi leo hatukuwaona kama wako hai au wamefariki.

Lakini isitoshe kutokana na ukubwa wa ajali hiyo hata kama mtu hakuna ndugu au jamaa yako basi lazima machozi yangekutoka kutokana na kuwafikiria ni hali gani iliyokuwemo kwenye meli hiyo wakati kila mmoja aliyekuwemo alikuwa akiona hivi hivi kuwa wakati wake wa kuaga dunia umefika.

Mheshimiwa Spika,kifo si kitu cha mchezo hata kidogo na wala sio kitu cha masihara na ndio mana hata Mwenyezi Mungu akakiekea pazia akakifanya kuwa ni siri yake peke yake,hakutoa nafuu kwa mtu yoyote kujua ni lini au wakati gani ataaga dunia.Na alifanya hivyo kwa makusudi kwani kwa binaadamu yoyote kama angelikuwa anashauriwa kufa basi hakuna angelikubali kama tajiri basi angelikubali kutoa mali yake yote ili abaki hai duniani,jee Mheshimiwa Spika,hebu tufumbe macho na tuvute fikra jee wakati meli inazama wenzetu walikuwa katika hali gani. Kwani wao walipata bahati ya kushuhudia vifo vyao.

Mheshimiwa Spika,tuwafikirie wanawake waliokuwa na watoto wao ndani ya meli hiyo walikuwa katika hali gani,tuwafikirie waliokuwa na wake zao ndani ya meli hiyo walikuwa na hali gani,tuwafirie waliokuwa na wazee wao ndani ya meli hiyo walikuwa na hali gani,halikadhalika waliokuwa na ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wamefuatana pamoja ndani ya meli hiyo walikuwa katika hali gani.

Mheshimiwa Spika,bilashaka fadhaa ilikuwa kubwa ndani ya meli hiyo kwani hakuna angelikuwa na uwezo wa kumuokoa mwenziwe isipokuwa Allah (S.W).Mheshimiwa kwa taarifa meli haikuzama ghafla ilianza kujaa maji kwa upande wa nyuma na katika mkondo mkubwa Nungwi wenye kina kirefu cha maji na mawimbi makali ambapo wakati wote meli hata ikiwa na ukubwa gani basi hupata tabu kupita katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, usiku huo wa manane wakati wengi wa abiria hao walikuwa wamelala ghafla waliamshwa na mawimbi ya maji yaliyoanza kuingia ndani ya meli pamoja na vilio vya wenzao pia na wao kupata mfadhaiko na kushuhudia meli waliokuwemo ndani ikianza kuzama na kusshuhudia kwa macho yao kuwa ndio wanaaga dunia.

Mheshimiwa Spika,hebu tufikirie mfano humu ndani ya ukumbi wa Baraza kama ingekuwa ndio meli hiyo na sisi ndo abiria jee hali ingekuaje.

Mheshimiwa Spika,hili ni tukio la kweli na wala si mchezo wa kuigiza,huu ni msiba mkubwa wa kitaifa na hatuwezi kuusahau milele,tukitaka tusitake kifo walichokufa wenzetu ni kibaya sana ingawa ni uwezo wa Mwenyezi Mungu lakini ukweli kinauma sana.

Mheshimiwa Spika, sisi tukiwa Wawakilishi wa Wananchi tunaitaka Serikali ichukue hatua kali sana za kinidhamu kutokana na uzembe mkubwa uliosababisha ajali hiyo ambayo haiwezi kusahaulika. Ambayo imepoteza roho nyingi za ndugu zetu pamoja na mali.

Mheshimiwa Spika, kamati yangu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais juu ya tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islanders imekutana na kujadili kwa kina na kuja na maoni yafuatayo kuhusiana na taarifa hiyo.

Mheshimiwa Spika, Kwanza ripoti imeeleza kuwa meli hiyo imesajiliwa kubeba abiria 610 ambapo ikiwa itatokea ajali hao kungekuwa na life jacket 610 na ingekuwa wepesi wa kuokolewa kutokana na vifaa vilivyopaswa kuwemo kwenye meli hiyo, lakini uhalisia meli hiyo ilipakia abiria wengi sana zaidi ya 2,764 mara tano zaidi ya uwezo wa meli hiyo, hii inadhihirisha uzembe wa makusudi uliofanywa na wahusika mbali mbali wanaohudumia na kusimamia idadi na usalama wa abiria wanapo safiri kwenye meli. Mhe Spika ndani ya baraza lako tukufu tumekuwa yukipiga kelele siku zote namna ya udhibiti wa idadi uingiaji melini lakini Waziri amekuwa akitoa jawabu za kubahatisha asizokuwa na uhakika nazo pia dharau ya kutokujali taarifa mbalimbali zinazotolewa na wananchi kupitia vyombo mbalmbali vya habari ikiwemo magazeti na Redio na matokeo yake ndio kama hayo. Kwa mfano ( TAARIFA YA WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO JUU YA HITILAFU KWA VYOMBO VYA BAHARINI SIKU ZA HIVI KARIBUNI):= Mhe Spika naomba kunukuu baadhi ya maneno yake kama ifuatavyo:-

“Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu kupitia mamlaka yake ya Usafiri baharini imekuwa ikpokea taarifa mbalimbali kuhusiana na usafiri na mwenendo mzima wa vyombo vya Baharini, anaendelea :- taarifa hizi zimekuwa zikifuatiliwa na wizara yangu kupitia Redio ,Magazeti n.k hata hivyo wizara yangu imekuwa ikizifuatilia kwa karibu na kujitahidi kuzihakiki na kugundua nyingi ya taarifa hizo zinazotolewa zinautata hivyo inapelekea kuleta tafsiri nyingine kwa jamii, tafsiri zinazoleta taharuki kwa jamii.” Mwisho wa kunukuu.

Mhe Spika pia Waziri huyo akalidanganya Baraza lako tukufu kwa kusema naomba kunukuu tena “Mhe Spika, waziri naomba kutoa pole kwa wale wote waliopta athari na usumbufu kutokana na taarifa hizo, Aidha nalihakikishia baraza lako tukufu na wananchi wetu wa Zanzibar wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kupitia malaka ya usafiri Baharini wanachukua hatua zote za kiusalama wa vyombo vya Usafiri Baharini kabla ya vyombo kuondoka kufanya safari zake. Aidha tutaendelea kuchukua hatua zote za kiusalama kwa vyombo vyote vinavyofanya safari hizo na kufanya huduma hizo za kusafirisha wananchi ikiwemo kuvikagua na kuvithibitisha juu ya safari zake hizo. Mwisho wa kunukuu, Je Mhe Spika, katika meli hiyo hili lilifanyika?

Ndio maana kamati yangu ikabaini kwamba kunaubabaishaji mkubwa wa kiutendaji katika wizara hii na kukaa ofisini na kutuletea taarifa za kujifurahisha wao tu, na sio uhalisia.

Mhe Spika, kutokana na uzembe huo uliofanywa na wizara imeonyesha wazi wazi kuwa Waziri ameshindwa kusimamia ipasavyo majukumu yake aliyopewa na mhe Rais na kwa kuwa kwa mujibu wa Sheria na Regulation zinazoongoza mamlaka ya usafiri wa baharini kuna kupengele kinachomtaka Waziri kuunda tume linapotokea jambo kama hilo lakini mhe Rais ameamua kuchukua jukumu yeye mwenyewe kuunda tume ni wazi ameona waziri naye amehusika ndio maana hakumsubiri akaunda yake, kwa maana hiyo Hapa tunamtaka Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano ajiuzulu kwa hiari yake ili kuonyesha uwajibikaji na asisubiri kuwajibishwa na Rais kwa uzembe wa kutokusimamia majukumu aliyopewa na tunaamini akifanya hivyo itakuwa ni kweli Serikali yetu inawajibika kwa wananchi na hata M.Mungu amesema kwamba( kila mchunga ataulizwa kwa anachokichunga ) Hiyo ndio Demokrasia na utawala bora unavyotaka, kwani Demokrasia ni gharama. Tusione taabu kuwajibika pale inapobidi, hasa kutokana na uzito wa jambo lenyewe.

Mhe Spika, kama kweli tunataka tuendelee lazima tubadilike kama anvyosema mhe Rais wetu tusifanye kazi kama tulivyozoea ( BUSSINESS AS USSUAL) tubadilike ili tufike tunakotaka, kuna mifano mingi ya Serikali kuwajibika Duniani tangu kuchaguliwa Rais mwanamke huko Brazil Bi ROSHELINA kuanzia mwezi January mwaka huu hadi sasa ni Mawaziri wane wamejiuzulu kwa hiari yao, kutokana na makosa mbali mbali ya taasisi zao, Japan kwa miaka mitano ni Mawaziri wakuu watano wamejizulu, Iraq n.k na kwa hapa Tanzania Rais mstaafu wa ZNZ na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu kutokana na vifo vya wafungwa gerezani alipokuwa Waziri wa Mambo ya ndani na sio mkuu wa Magereza aliyewajibika, wakati wa utawala wa Mwalim Nyerere, kwa hiyo hilo sio jambo geni hata kwa Tanzania. Bado kuna haja ya Serikali yetu kuonyesha uwajibikaji kwa wananchi.

Mhe Spika, bado kamati yangu imeona kulitokea uzembe mkubwa kutoka kwa keptein wa meli hiyo kwa kushindwa kutoa taarifa mapema wakati meli ilpoanza kuingia maji hadi hapo abiria wenyewe kuanza kupiga sim wakiwa juu ya meli tunaamini kama Keptain angelitoa taarifa mapema basi abiria wengi sana wangeliokolewa wakiwa hai nadhani kwa kuwa ulikuwa usiku wangelipiga fataki kurusha angani ingelisaidia kujulisha waokoaji kujua chombo kiko wapi, kwani abiria walikaa baharini karibu masaa 5 wakiwa hawajapata msaada wowote, wakati tukio limetokea pahala pa kufika kwa muda wa saa moja tu. Tunaamini waokozi wangelifika mapema hali isingekuwa hivyo.

Kamati inashauri meli zote ziwe na fataki za kupiga angani pindipo ikitokea janga kama hilo, kwani ajali wakati wowote hutokea.

Mhe Spika, suala la uzembe wa kutojua idadi ya abiria waliopanda kwenye chombo umekuwa na kitu cha kawaida kwa wenye vyombo na watendaji wa Serikali wanashuhudia lakini hakuna anaejali mfano ,baada ya kuzama meli ya MV ,FATIH waziri aliahidi kuwa sasa mtu yeyote akitaka kusafiri ni lazima aende na kitambulisho je hilo linafanyika au wajumbe wako wanaondolewa njiani tu? Kama suala hilo lingeli simamiwa basi tayari wtu wote waliokuwemo wangelikwisha julikana lakini kutokana na uzembe huo hakuna kinachofanyika, hii inaonyesha ni namna gani baadhi ya viongozi wanavyoshindwa kusimamia majukumu yao, pia kutojua thamani ya Raia wetu, hata akifa bado watu uchungu hawana.

Mhe Spika kamati yangu haijaridhika na sehemu ya taarifa ya Serikali inayosema kwamba kuna majina yamepokelewa mara mbili sisi tunaamini kwa kushirikiana na wakuu wa Mikoa majina yanaweza kukusanywa na yakaangaliwa yote kwa pamoja na kuangalia yaliyofanana kufuatiliwa na marekebisho yakafanywa haraka ni aibu katika karne hii ya 21 tunashindwa kulinganisha vitu kama hivi,

Mhe Spika, pia kamati yangu haikuridhika na taarifa ilyotolewa na Serikali kuhusu kushindwa kwa kazi wazamiaji kutoka Afrika ya kusini eti kwa sababu ya kina kirefu cha maji kwani hapo mwanzo walipoitwa kwani hawakupewa taarifa kamili kuhsu eneo la tukio na kima cha maji kilichopo? Kwani tulipata taarifa za awali kutoka kwa wazmiaji wetu wa hapa ZNZ kwamba wamejaribu kuzamia na wakagundua kima cha maji hapo ni kiasi metre 300 kabla ya kuja hao ndugu zetu kutoka Afrika ya kusini, kwa hiyo tunaitaka Serikali tujifunze kutokana na makosa yetu wakati na siku yeyote tutakapohitaji msaada kutoka kwa wenzetu basi tuwape taarifa za kutosha kwa kazi watakayokuja kuifanya ili kuweza na na wao kujitayarisha na vifaa na zana zinazostahili na kama uwezo wao utakuwa ni mdogo basi kutujuulisha mapema, lakini pamoja na kasoro hizo za kiutendaji tunawashukuru ndugu zetu wa Damu kutoka Afrika ya kusini tunaamini walikuja kutusaidia lakini hawakupata taarifa sahihi zilizokamilika, tunawaomba na mara nyingine tukiwahitaji basi wasisite kuja kutusaidia ingawa hatuombi maafa mengine yatokee.

Kamati kwa niaba ya wananchi wote tunaomba serikali itupelekee pongezi hizo. Kwa Serikali ya Afrika ya kusini.

Mhe Spika, pamoja na kuchelewa kufika kwenye tukio kutokana na kutojua chombo mahala kilipokuwepo, lakini tunatoa pongezi zetu za Dhati hasa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kask, Unguja, pamoja na wavuvi na wananchi wa kijiji cha Nungwi bila ya kujali itikadi za kisiasa au Dini wala jisia wakiwemo kinamama waliosadia kuwapokea majeruhi na maiti zilizopokelewa Nungwi, pia kikosi cha Kmkm kilichotokea Mkoani Pemba kwa kuwa wa mwanzo kufika kwenye ajali wakitokea Pemba, pia Helikopta ilyokuja kugundua na kutoa ishara ya mahala meli ilipokuwepo, wenye vyombo binafsi vya Speed Boat pamoja na wawekezaji wa Mahotelini waliotumia Speed Boat zao kusaidia kuokoa maiti na majeruhi waliokuwemo kwenye meli hiyo. Kamati yangu inawaombea kuendelea na moyo huohuo wa kusaida popote na wakati wowote kwenye matukio kama hayo sisi hatuna cha kuwapa isipokuwa M,Mungu atawalipa fungu lao.

Mhe Spika tunaiomba Serikali kama tulivyoshauri kwenye ripoti yetu ya kamati kwa afisi ya Rais mnamo mwezi wa April mwaka huu serikali iko haja maalum ya kukiboresha kikosi chetu cha uokozo KMKM pamoja na Zimamoto kwa kuvipatia vifaa vya kisasa ili pale yanapotokea maafa basi wawe na uwezo mkubwa wa kukabiliana nayo.kwani hivi sasa KMKM wanaukosefu mkubwa wa nguo za kuzamia ukosefu wa chupa za gesi, na chombo cha kumuandaa mzamiaji kabla kwenda kwenye kina kirefu cha maji bila chombo hicho basi kuhatarisha hata usalama wa afya ya muokozi hyo, baya zaidi kwa upande wa Pemba hakuna hata kitengo cha uzamiaji je M.Mungu tena atuepushie mbali ajali ikitokea Pemba basi itabidi waokoaji wachukuliwe kutoka unguja.

Mhe Spika leo hii Pemba kuna Fibre Boat za KMKM karibu sita lakini ingine iliyoko na moja tu wakati thamani ya engie hizo na shs 3milioni kila moja je hapa kweli tuko Serios katika kuokoa maisha ya wananchi wetu? hii ni hatari kubwa na inabidi kamati yangu inashauri Serikali kulifanyia kazi mara moja.

Mhe Spika, kutokana na funzo tulilolipata hivi sasa ni lazima Serikali ifanye jitihada zozote za kununua meli kwa njia yeyote na kama hakuna pesa basi ifunguliwe account maalum ya kuomba msaada wa kununuliwa meli naamini kuna wasmaria wema wengi watatusaidia.

Mhe Spika, kamati yangu intoa tahadhari nyengine kwa Serikali kwamba yanaweza yakatokea maafa mengine Makubwa sana kama hatua za haraka hazijachukuliwa na Serikali kuangalia athari itakayokuja kutokea iwapo Hoteli ya Misali Beach Resort iliyoko wesha iwapo ikija kuripuka na kuwaka kama mahoteli mengi yanavyowaka maeneo mbali mbali hapa Zanzaibar kutokana na pale ilpo basi Matenki ya Maufuta yaliopo wesha yataripuka ,pia kama kama kuna Meli inateremsha Mafuta itawaka na wananchi wanaoishi wesha watateketea, sasa bora mtu aliepata maafa akafa kuliko mtu alieungua kwa moto sijui viongozi tutaenda tena kuwafariji kwa zamu au vipi.kwani hoteli hii imejengwa kiubabe haikufuata taratibu zozote Idara ya Mazingira ilizuia, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba alizuia lakini nguvu ya Pesa ilitumika ilitumika na Hoteli ikajengwa na hivi sasa inatumika likitokea la kutokea kamati inasema Serikali itawajibika.

Mhe spika, tunashauri Serikali hiyo tume iliyoundwa na SMZ ije na taarifa zitakazowaridhisha wananchi, mfano Wamiliki wa meli, Bima, mwaka ilokaguliwa meli hiyo,vifaa vya uokoaji vilivyokuwemo, Ruhusa ya kuondoka bandarini, hatua kwa wasimamizi waliokuwepo siku ya tukio, na msaada gani kwa familia hasa mayatima waliobaki.

Mhe Spika, pia tunatoa pongezi kwa Serikali kupitia kamati yake ya maafa kwa mipango mizuri ilyoipanga na kuweza kuweka utaratibu wa kuzitambua maiti pamoja majeruhi pamoja na maandalizi ya mazishi kwa wale waliokuwa hawakuonekna na jamaa zao. Pia kutoa huduma chakula na usafiri kwa wale waliotaka kurejeshwa makwao. Pia tunatoa pongezi kwa madaktari na wahudumu wote wa Hospitali ya KIVUNGE, JESHINI BUBUBU NA MNAZIMMOJA kwa kazi kubwa walioifanya kuokoa maisha ya waliopelekwa Hospitalini huzo.

Tunatoa pongezi za dhati kwa vyombo vyote vya Habari kuanzia Radio Nur walionza kutoa taarifa ,TVZ, Radio znz Znz Cable TV N.k kwa kuwapasha habari wananchi kwa wakati wote wa tukio.

Mhe Spika pia tunatoa pongezi kwa viongozi wetu wote wa kitaifa Kuanzia Rais mwenyewe Makamo wake wa kwanza na wa Pili, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Waziri mkuu, Viongozi wa Dini na wengine wote wakiwemo Vikosi vyetu vuyote vya ulinzi kwa kujumuika kwa pamoja kwa kila mmoja kwa nafasi yake katika kutoa msaada uliohiohitajika hii inaonyesha mashikamano mkubwa kwa nchi yetu hasa kwenye kusaidiana kwenye dhiki na faraja.

Mhe Spika mwisho kabisa tunatoa shukrani kwa wananchi wote wa Zanzibar kwa mashirikiano waliyoyatoa wakati wote wa tukio na kutoa msaada wa hali na mali tunawaomba waendelee na moyo huo huo na sisi tuko nyuma yao.

TUNAMUOMBA M.MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEM MAHALI PEMA PEPONI AMIN .

Ahsante

…………………

MHE: HAMZA HASSAN JUMA

KAMATI YA KUSIMAMIA OFISI ZA VIOGOZI WAKUU WA KITAIFA

BARAZA LA WAWAKILISHI

ZANZIBAR.

Advertisements

One response to “Taarifa ya kamati ya kusimamia viongozi

  1. Yah, its true, Mh. Hamad you better resigned. Umeshindwa kazi, bora upumzike. Unafanya kazi kimazoea na kutoa majibu ya kisiasa bila ya kujali adha ya usafiri tunazopata jamaa zako wa kipemba! Na leo umekuwa sababu ya mauti ya ndugu zetu! Umeshindwa kuonyesha mabadiliko yeyote ktk wizara unayoiongoza na kuyaacha madudu yakiendelea bandarini!

    Mustafa jumbe should be next to resign!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s