Ajali ya Spice Islander: Waafrika ya Kusini waondoka, Rais Shein ateua Tume

Mkuu wa kikosi cha wazamiaji kutoka Afrika ya Kusini iliyokuja kusaidia kuizamua meli ya Mv Spice Islander (kulia) akimuaga Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, baada ya kushindwa kuizamua meli hiyo kutokana na kina kirefu iliyozama

 

Na Talib Ussi, Zanzibar

Wakati wapiga mbizi wa Afrika ya Kusini wakiaga na kurudi nyumbani baada ya kushindwa kuifikia meli ya Mv Spice Islander iliyozama usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kamati ambayo itafanya uchunguzi wa ajali ya meli hiyo iliyotokea  ikiwa safarini kutoka Unguja kueleka Pemba na kusababisha vifo vya watu 203.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, ameteua tume hiyo kwa kuutmia uwezo aliopewa chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 33 ya Sheria ya Zanzibar.

Tume hiyo ambayo ina wajumbe 10 itakuwa chini ya uwenyekiti wa Jaji Abdulhakim Ameir Issa ambaye ni mwanasheria mzoefu na kwa sasa ni jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar.

Wengine ni Jenerali S. S. Omar ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Wanamaji katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Komadoo Hasan Mussa Mzee, ambaye ni mkuu wa Kikosi cha Wanamaji wa KMKM na Kapteni Abdulla Yusuf Jumbe, ambaye ni nahodha mzoefu katika meli za kitaifa na kimataifa ambapo pia aliwahi kuwa nahodha wa Mv Mapinduzi iliyokuwa inamilikiwa na Serikali ya Zanzibar.

Vile vile, kwenye kamati hiyo yumo Kapteni Abdaulla Juma Abdulla, mwanamaji mstaafu na sasa ni naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Idara Maalum za SMZ), Salum Taufik Ali ni mwanasheria mzoefu pia ana uzoefu wa Sheria za Bahari kwa sasa ni mwanasheria wa Zantel.

Wengine ni Kapteni Hatibu Katandula ni Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Baharia cha Dar es Salaam na Bi Mkakili Fauster Ngowi, ambaye ni wakili katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanajeshi mstaafu Ali Omari Chengo ambaye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Naibu Waziri wa Mawasiliano katika awamu zilizopita.

Na wa mwisho ni Katibu wa tume hiyo Shaabani Ramadhani Abdulla, ambaye ni mtaalamu wa sheria za bahari na hivi sasa ni mwanasheria katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP).

Tume hiyo imeundwa ili kujuwa ukweli kuhusu kutambuwa chanzo cha ajali ya meli hiyo iliyosababisha maafa makubwa na simanzi kubwa katika visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Advertisements

2 responses to “Ajali ya Spice Islander: Waafrika ya Kusini waondoka, Rais Shein ateua Tume

  1. Jamani sasa huyu Abdulla Yusuf Jumbe ambaye ni mjumbe na Mustafa Aboud Jumbe (cousin) ambaye ni mmoja wa wachunguzwa, jee inakuwaje? Ataweza kweli kumtosa nduguye?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s