Sala maalum kuwaombea maiti wetu wa Mv Spice Islander

Kutoka kushoto: Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, katika dua maalum kwa ajili ya wahanga wa mkasa wa meli ya Mv Spice Islander iliyofanyika leo Jumatatu ya 12 Septemba 2011, Maisara mjini Unguja

 

Baadhi ya viongozi wa kidini na wa kiserikali waliohudhuria kwenye sala maalum ya kuwaombea wahanga wa mkasa wa kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander. Sala hiyo ilifanyika leo katika viwanja vya Maisara.

Baadhi ya Waislamu wa Zanzibar katika sala ya kuwaombea ndugu na jamaa zao waliokufa kutokana na ajali ya meli ya Mv Spice Islander. Sala ilifanyika leo Jumatatu katika viwanja vya Maisara, mjini Unguja

 

Miongoni mwa makaburi 46 yaliyochimbwa na serikali huko Kama kwa ajili ya kuwazika baadhi ya watu waliokufa kwenye ajali ya meli ya Mv Spice.

 

Mkono wa Pole kutoka kwa Wanafunzi wa Tanzania nchini Urusi

UMOJA  WA  WANAFUNZI  WA  KITANZANIA  WASOMAO  KATIKA  CHUO  KIKUU  CHA  URAFIKI  (LUMUMBA) MJI  WA  MOSCOW  NCHINI  URUSI,  UNAPENDA  KUTOA  SALAMU  ZA  POLE KWA  WATANZANIA  WENZAO  KUFUATIA  AJALI  YA  MELI  ILIYOPINDUKA  NA  KUZAMA   KATIKA  VISIWA VYA  ZANZIBAR  MNAMO  SIKU  YA  JUMAMOSI  MAJIRA YA USIKU WA MANANE  NA  KUSABABISHA  VIFO  KADHAA VYA   ABIRIA WALIOKUWEMO  KATIKA  MELI  HIYO  WAKIWA SAFARINI KUTOKA UNGUJA  KUELEKEA PEMBA.

KWA  PAMOJA  TUNASEMA  MSIBA  HUU  NI  WETU  SOTE  NA  TUNAMUOMBA   MWENYEZI   MUNGU AWALAZE  MAREHEMU  MAHALA PEMA PEPONI,AWAPE SUBIRA WAFIWA NA AWAPE SHIFAA NA TAHAFIFU MAJERUHI NA WOTE WALIONUSURIKA NA KADHIA HIYO.

KWAKE  TUMETOKA  NA  KWAKE  NI  MAREJEO.

AMEEN!!!!!!
UONGOZI WA  WANAFUNZI-UWATA

Advertisements

One response to “Sala maalum kuwaombea maiti wetu wa Mv Spice Islander

  1. Mungu aziweke Roho zao mahali pema peponi ameni mbele yao nyuma yetu ni kazi ya mungu hiyo aina makosa si njama za mtu wala nini tuwe na moyo wa subra kwani kila afanyalo mungu ni yeye amepanga si mkono wa mtu Inshallah Allah atatupa mioyo ya subra sote twatakiwa tuseme Inna Lilah wa Inna Illah raj unn!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s