Wazanzibari wa Uingereza walilia wenzao

Makamo wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akimpa mkono wa ta'azia Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kufuatia ajali ya meli iliyogharimu maisha ya watu zaidi ya 200

Viongozi na wanachama wa Zanzibar For Democracy (UK) tumezipokea habari za kuzama kwa meli ya Spice Islaners kwa huzuni, masikitiko na unyonge sana. Aidha, tumepata maumivu sana kwa vifo vya wananchi wengi ambao walikuwemo katika meli hiyo.

Tunaomba kuchukua nafasi hii ili kutoa salamu zetu za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo.Vile vile tunaiomba serikali kuchukua hatua zifuatazo ili kunusuru maisha ya wananchi wanaosafiri kwa kutumia vyombo vya baharini.

(a) Kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya baharini vinavyosafirisha abiria vinakaguliwa kwa kutumia viwango vya kimataifa;

(b) Vyombo hivyo vinapakia idadi halisi iliyokubaliwa kisheria;

(c) Vyombo vyote vilivyochakaa visiruhusiwe kuingizwa nchini na vile vilivyopo visiruhusiwe kusafiri;

(d) Serikali ichukue juhudi za makusudi za kuwapatia wananchi vyombo vya kisasa katika vivuko vyote vyenye kutumiwa na wananchi wengi, isiwache jukumu hili mikononi mwa watu binafsi;

(e)Serikali ifanye uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo, na mapendekezo yatakayotolewa yafanyiwe kazi kwa lengo la kuimarisha na kudumisha usafiri wa uhakika na usalama kwa wananchi.

Tunaungana na wananchi wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa uliotokea.

Inshallah Mwenyezi Mungu awape wafiwa wote subira, stahmala uvumilivu kwa msiba huo na awalaze marehemu wote peponi (Amin).

Ahsante,
Abdulla A. Abdulla,
Katibu,
Zanzibar For Democracy (UK)
(07853180339)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s