Rambirambi kwa msiba wa Zanzibar

Msiba! Msiba! Msiba!

Uongozi wa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo pamoja na wafanyakazi wake wote unaungana na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wazanzibari wote kutokana na msiba mkubwa uliyoikumba nchi kutokana na kuzama kwa meli ya Spice Islanders tarehe 10/09/2011 wakati ikisafiri kwenda Pemba kutokea Unguja.

Ofisi inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ndugu na jamaa wa wafiwa wote. Aidha, Ofisi inawaombea subira na kupona haraka wale wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Tunamuomba Mwenyezimungu mkarimu azilaze roho za marehemu waliotangulia mbele ya haki mahali pema peponi, Amin.

Inshallah familia zote zilopatwa na msiba huu nazo ziwe na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu.

INNA LILLAH WAINNA ILAIHI RA’AJIUN.

Imetolewa na;
Afisa mawasiliano
Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo
Skina Hamad Salum

Advertisements

One response to “Rambirambi kwa msiba wa Zanzibar

  1. Kwa hakika sisi sote ni wa M/Mungu kwake tumetoka na kwake ndio marejeo yetu. Ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki ni kuwa M/Mungu aliwapenda zaid kilichobakia kwetu ni kuwaombea dua M/Mungu awapumzishe mahali pema peponi na sisi tuliobakia tuvute subra katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi kwani wao wametangulia nasi tunawafuatia kwani hatujui ni lini wala muda gani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s