
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Ally Amour wakati alipofika kumjulia hali mtoto Said Gerald (6) aliyenusurika katika ajali ya Meli eneo la Nungwi usiku wa kuamkia leo, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar. Aliyempakata ni mama yake mzazi, Mariam Hemed. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
MUWAZA IMESIKITISHWA NA AJALI YA MELI YA SPICE ISLANDER ILIOKUWA SAFARINI KUELEKEA PEMBA. AJALI HIO ILITOKEA ALFAJIRI YA LEO TAREHE 10.09.2011 SEHEMU ZA BAHARI KARIBU YA NUNGWI KASKAZINI YA UNGUJA.
MUWAZA INAWAOMBEA WALE WALIOPOTEZA ROHO ZAO: KAULI THABIT, WAONDOSHEWE ADABU, WASAMEHEWE MAKOSA YAO, WAPOKEWE KAMA MASHAHIDI NA WALAZWE PEPONI AMIIN!!
MUWAZA INATOWA MKONO WA RAMBI RAMBI KWA JAMAA, WEMA NA MARAFIKI WA WAFIWA NA KUWAOMBEA SUBRA.
INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJIUUN
MUWAZA INAIOMBA SEREKALI IANZISHE UCHUNGUZI WA HARAKA NA WA KINA ILI KUJUA KIINI CHA SABABU ILI KUEPUKA AJALI KAMA HIZO SIKU ZA MBELE NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WALE WALIOSABABISHA AJALI HIO
Dr. Yussuf S. Salim
Mwenyekiti wa MUWAZA