Mianya ya Magendo ya Karafuu kuzibwa

Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini Unguja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ali Vuai pembeni ni Bi Kidawa Mbunge wa kuteuliwa na afisa wa sekreteriat ya CCM Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kufanya mawasiliano na ofisi za ubalozi wa Tanzania ziliopo katika nchi za Malaysia, India na Mombasa nchini Kenya kufuatilia mwenendo wa biashara ya karafuu unaofanywa na wafanyabiashara kwa njia ya magendo.Kauli hiyo imetolewa na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati alipokutana na watendaji wa Shirika la Taifa la Biashara la (ZSTC) huko Pemba wakati wa ziara yake kwa ajili ya kuangalia shunguli za uchumaji wa zao la karafuu.

Alisema hali ya magendo ya karafuu yanayofanywa na wafanyabiashara wa nchi jirani ya Kenya inatisha ambapo, karafuu zinazovunwa Pemba zinasafirishwa huko na kulikosesha taifa fedha nyingi za kigeni.

‘Tunakusudia kuwaagiza maofisa wa ubalozi wetu waliopo Mombasa, India pamoja na Malaysia kufuatilia kwa kina mwenendo wa uingiaji wa karafuu katika nchi hizo na kujuwa zinatoka wapi’ alisema balozi.

Alisema magendo ya karafuu kwa kiasi kikubwa yanadhoofisha uchumi wa nchi, zaidi katika kipindi hichi ambapo zao la karafuu mavuno yake ni mazuri sana kisiwani Pemba,pamoja na bei yake kupanda katika soko la dunia.

Balozi alitembelea mashamba mbali mbali ya wakulima wa karafuu kisiwani Pemba na kujionea mwenyewe shunguli za uchumaji wa zao la karafuu.

Mkuu wa wilaya ya Mkoani, Jabu Khamis Mbwana alimuambia makamo wa rais kwamba jumla ya magunia ya karafuu 141 zimekamatwa zikiwa katika mpango wa kusafirishwa nje ya nchi kwa njia za magendo.

Alisema karafuu hizo zilikamatwa kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa wapiganaji wa vikosi vya serikali pamoja na polisi jamii Pemba.

‘Mheshimiwa makamo wa pili wa rais magendo kisiwani Pemba bado yapo na yanaendelea….lakini na sisi tunapambana nao’alisema Jabu.

Jabu aliwataka wakulima wa zao la karafuu kuuza karafuu zao kupitia shirika la taifa la biashara na kuacha tabia ya kuweka karafuu majumbani, kwa kisingizo cha kusubiri hadi kupanda kwa bei mpya katika soko la dunia.

Advertisements

One response to “Mianya ya Magendo ya Karafuu kuzibwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s