Serikali nilipeni haki yangu

Hii ndo gari la katibu mkuu iliyoshambuliwa na mawe na mtu ambaye kwa miaka mingi anaidai serikali million 104 za tanzania. licha ya mahakam kutoka hukumu mwaka 2007, bado seriklai inapiga danadana kumlipa mmnyonge huyo hadi kufikia kupata hasira za kushambulia gari la katibu mku. kwa mujibu wa unchunguzi mtu huyo Ali Said alijenga rest House ya rais Micheweni, Kaskazini Pemba. na baada ya karibu na kumaliza, anakorofishana na serikali juu ya malizpo na kufikishana mahakamani. Serikali ya karume na sasa ya Dk Shein bado haitaki kulipa deni.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUSHAMBULIWA KWA GARI LA KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA ZANZIBAR

 

Gari la Katibu Mkuu  Wizara wa Fedha, Uchumi na Maendeleo ya Mipango wa Zanzibar limeshambuliwa kwa mawe na  Ali Salim Ali(49) Mkazi wa Fuoni Mjini Unguja  ambaye anaidai Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kufanya kazi ya ujenzi wa jengo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.

 

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi wa Wizara hiyo, Ramadhan Senga amesema mtu huyu awali, alikwenda Ofisi ya Katibu Mkuu Khamis Mussa kutaka kumuona,lakini hakuwepo Ofisini,lakini wanadhani alikuwa na dhamira ya kutaka kumfanyia jambo baya.

 

Senga amesema baada ya kumkosa Katibu Mkuu, alianza kulishambulia kwa mawe gari analotumia Katibu Mkuu Khamis Mussa lenye namba za usajili SMZ 6460 aina ya Toyota Pradomaliya Wizara ya Fedha,Uchumi na Maendeleo ya mipangoZanzibar.

 

Mkurugenzi huyo amesema garihilolilishambuliwa sehemu za vioo kabla ya mtuhumiwa kukamatwa na Polisi.

 

Akizungumzia kadhia hiyo, Mkurugenzi Senga amesema Wizara yake sio muhusika mkuu wa madai ya mtuhumiwa huyo ambapo Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ndio wanaohusika na madai ya mtuhumiwa ambaye alifanya kazi ya ujenzi katika Mkoa wa KaskaziniPemba.

 

Amesema kazi aliyofanya ni kujenga jengo la Serikali katika Wilaya ya Micheweni karibu miaka mitatu iliyopita ambapo hakuweza kulipwa fedha zake kwa wakati na ndipo alipofungua kesi Mahakamani.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kamishna Msaidizi, Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukiohiloambapo amesema upelelezi wa tukiohilounaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

 

IMETOLEWA NA:

IDARA YA HABARI(MAELEZO)ZANZIBAR

05/09/2011

3 responses to “Serikali nilipeni haki yangu

  1. Serikali jaman kuwen makini watu mkiwapa kazi jaman walipe kwan hat wao wanahitaji matumizi ili kuepusha hatia kama hiyo ambayo.

  2. Kwa hakika huyu jamaa ana makosa lakini serikali ina makosa zaidi na ndio ya kwanza kuanza kuyafanya makosa
    hivyo haina budi kujibu mashtaka ya kutokumlipa kama walivyokubaliana na kumdhalilisha yeye na familia yake kwa
    kipindi chote walichokaa bila ya kumlipa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s