Dk shein afanya uteuzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa nafasi mbali mbali.

Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika uteuzi huo, Rais Dk Shein amemteua Profesa Idris Ahmada Rai kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA). Profesa Rai ni Profesa wa Sayansi aliwahi kusomesha Chuo Kikuu cha Makerere Uganda.

Rais Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 9(1) cha sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar namba 8 ya mwaka 1999. Uteuzi huo unaanza Septemba 6 mwaka huu.

Katika uteuzi mwengine Rais Dk Shein amemteua Kombo Hassan Juma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar. Kombo aliwahi kuwa Mkurugenzi katika Wizara ya Elimu Zanzibar ambaye ana Shahada ya Uzamili katika Elimu.

Viongozi wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni pamoja na Idd Khamis Haji(Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar, uteuzi huo unaanza Septemba 6 mwaka huu.

Aidha, Rais Dk Shein amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika Taasisi mbalimbali za Serikali ambapo Salmin Senga Salmin anakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar, kabla ya hapo aliwahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, kitaaluma ni Mhandisi.

Mwalimu Haji Ameir ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri na ni mchumi.

Uteuzi mwengine ni Dk Issa Ziddy anayekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA ambaye ni daktari wa Falsafa(PhD).

Mariam Mohammed Hamdan ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya HakiMiliki. Mariam Hamdan aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda, kitaalum ana Stashahada ya Uzamili katika habari Uteuzi huo unaanza Septemba 6 mwaka huu.

Aidha, Rais Dk Shein amemteua Mohammed Faki Mohammed kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma. Kitaaluma ana Shahada ya Uzamili katika Uchumi. Amewahi kushika nafasi mbalimbali Serikalini ikiwemo Waziri.

Katika uteuzi huo, Rais Dk Shein amewateua watu sita kuwa Wajumbe wa Kamisheni hiyo ambao ni, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar,Hamid Mahmoud Hamid, Mabrouk Jabu Makame, Issa Mohammed Suleiman , Ali Rajab Juma, Balozi Hussein Said Khatib na Jecha Salim Jecha. Uteuzi huo unaanza Septemba 6 mwaka huu.

Rais Dk Shein amefanya uteuzi wa Makadhi wa Wilaya mbalimbali za Unguja. Walioteuliwa ni Sheikh Mustafa Hassan Mwinyi, Sheikh Ali Khamis Mussa, Sheikh Mansab Khamis Omar, Sheikh Mohammed Ali Hamad, Sheikh Nassor Khamis Mbwana na Sheikh Daud Khamis Salim. Uteuzi huo unaanza Septemba 6 mwaka huu.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
05/09/2011

Advertisements

One response to “Dk shein afanya uteuzi

  1. Thank God mwenyekiti Wa Bodi ya Mikopo keshateuliwa. Tuombe Mungu angie ofisini kwa ari mpya naatusaidie. Namkumbusha tu watoto waliokuwepo China wanahitaji kushughulikiwa haraka kabla ya tarehe 14 September kwasababu baada ya hio tarehe watatakiwa kulipa yuan 500 kwa kila siku watakayozidisha kukaa Nchini.je serikali iko tayari kulipa hizo un necessary expenses which we can easily avoid!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s