Tanzania inasimama wapi kuhusu Libya?


Na Ally Saleh

Mwanzoni mwa mwaka huu wakati vuguvugu la mabadiliko nchini Libya
linaanza niliwandika makala katika safu hii juu ya hali hiyo kwa kuwa
nilijaribu kuona mbali katika suala hilo.Serikali yetu na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe ikanyamaza kimya na hadi juzi ndipo ilipoibuka na kutoa msimamo kwa niaba yetu kuwa Tanzania haitaitambua Serikali ya Mpito ya nchi hiyo.

Napenda kurudia makala nilioiandika wakati huo ili wananchi wetu waone
ni jinsi gani Serikali yetu inavyoendeshwa na ni namna gani mtindo wa
kuahirisha maamuzi unavyoweza kuwa gharama kwetu, lakini muhimu zaidi
ni vipi tunaogopa kufanya maamuzi magumu wakati kesho na keshokutwa
tutaitambua Serikali ijayo ambayo imechukuliwa kwa nguvu na wananchi,
kama ambavyo tunaendelea kutambua Zimbabwe ya Robert Mugabe na wababe
wengine mbali mbali:

Kwa hakika inasikitisha kuona nchi yangu Tanzania, na hasa Waziri wa
Mambo ya Nje na Uhshirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe walivyokaa
kimya kuhusiana na suala la Libya. Inasikitisha kwa mambo mengi.

Najiuliza iwapo Tanzania ingekuwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa wakati huu ingekuwa na msimamo gani kuhusiana na suala hilo
wakati lilipopiga kura yake ya hivi karibuni kuamua kusiktisha madhila
ya kionogozi wa Libya juu ya watu wake.

Kabla ya Libya sote tunajua ilikuwa ni vuguvugu la Tunisia, kisha
likatambaa hadi Misri, likarambaramba Algeria kidogo lakini baadae
likatuwama huko Libya, pembe ya Kaskazini kabisa ya Bara la Arika.

Kote kwa kiasi kikubwa utawala au Marais wa nchi hizo waliheshimu haki
ya raia wao kujikusanya na kujieleza ijapokuwa walijikusanya kupinga
utawala wao na walitoa maoni yao kupinga pia utawala huo.

Kitendo cha Misri kuendelea kuruhusu watu kufika na kukusanyika katika
Uwanja wa Tahriri kwa siku 18 kiliwashangaza wengi, maana kwa kwetu
kisingewezekana kabisa na ndicho kilichotoa shindikizo kwa Mubarak
kuondoka madarakani.

Kwa maneno mengine hata katika dhiki ya kupingwa na wananchi wake,
lakini Rais Hosni Mubarak hakufanya ambayo yamefanywa na Muamar
Ghadafi wa Libya ya kukataa kabisa wananchi wake kuomyesha dalili
yoyote ya kupinga na kuchoka na utawala wake.

Hali kadhalika huko Tunisia, cheche iliyowashwa na kijana aliyejichoma
moto haikzimika mpaka Rias Zein Abideen Bi Ali alipoondoka na sababu
kubwa ni watawala hawakufanya kama alivyofanya Muamar Ghadafi wa
Libya.

Kwa kuona kilichotokea Misri na Tunisia, mara yalipooanza maandamano
nchini mwake kwa wananchi wake kumchoka baada ya utawala wa miaka 40
Ghadafi alisema kuwa nchini mwake hakuna risasi za mpira ila ziliopo
ni risasi za moto tu na akaapa atazitumia.

Kwa kuamini kuwa hangeweza kutokea mtu wa kumpinga hadharani kwa vile
yeye Ghadafi amefanyia wema mno wananchi wake kwa kuwapa nyumba,
elimu, mfumo bora wa miundombinu basi yeye alistahiki sio tu kupendwa
lakini hasa kuabudiwa, kongozi huyo hakustahamilia kabisa maandamano
hayo.

Hata Waafrika wengi tunalitizama suala la Libya katika jicho hilo
hilo. Kwamba Ghadafi kiongozi aliyejali maslahi ya watu wake inakuwaje
leo wananchi wake wamsusuike na kumuadhiri kiasi hiki? Lakini wengi
hatajuwi kabisa thamani ya kukosa uhuru ambayo Ghadafi aliwanyima
wananchi wake.

Kukosa uhuru na amani yua moyo ni suala zito sana na mifano ya karibu
ambayo naweza kuitoa ni ya hapa hapa kwetu. Wakati wa mwanzo mwanzo wa
Mapinduzi ya Zanzibar Rais Abeid Karume alifanyia mema mengi wananchi
wake, lakini uhuru na amani ya moyo ilikosekana kwa sababu ya
ukandamizi wa utawala wake na yakatokea yalitokea ingawa wengine
watasimama vilikuwa ni kitendo cha kupinga mapinuzi na cha
kitimbakwiri ( reactionaries).

Pili, ilikuwa ni rahisi kwa Julisu Nyerere kuwateka Wazanzibari
alipokuja na wazo lake la kuunganisha vyama 1977, kwa sababu pamoja na
mema ambayo Afro Shirazi Party iliyokuwa ikifanyia watu, lakini umma
ulikuwa kama umo ndani ya jela, na kwa hivyo walichoka na chama hicho,
na wakachagua kukiiondosha katika dunia.

Wengi tunamtizama Ghadafi kwa picha yake ya nje. Muafrika halisi,
mpenda maen delea, mpenda umoja, msadizi wa harakati za ukombozi
lakini pia msaidizi wa nchi za Kiafrika ambazo nyingi ama zimekula
fedha zake au zimetumia mafuta yake.

Ni wachache ambao wanajua kilichokuwa kikitokea Libya siku kwa siku.
Wanaojua utawala wa kipolisi ulivyoweza kuzima fikra yoyote ile
isyokuwa ya Ghadafi, utawala kandamizi ilivyoweza kuzima upinzani wa
aina yoyote ile lakini pia utawala chuma ulivyoweza kufung watu kwa
miaka mingi bila hata kupelekwa mahakamani.

Ni wachache pia wanaojua juu ya lawama dhidi ya Ghadafi kuuunga mkono
vitendo vya kigaidi au vyengine vya vikundi vinavyopigana katika nchi
zao na mfano tunaujua ule wa askari wa Libya kuonekana wkiisaidia
Uganda wakati Tanzania ilipoingia vitani kwenye vile baadae
vilivyoitwa Vita vya Kagera.

Baadhi ya watu wanaona uhalali wa Ghadafi na Serikali yake kuchukua
hatua ya kupiga na kupambana na wale wanaoitwa waasi kwa sababu waasi
hao wamechukua silaha kupambana na dola na kwa hivyo Serikali haiwezi
kukaa kimya wakati kitu kama hicho kinatokea.

Ni kweli waandamanaji na maandamano ya Libya yameelekea kuingia kwenye
uasi na kuingia kwenye majimbo kujitenga, lakini jee kabla ya uasi na
kujitenga si kulikuwa na maandamano na waandamanaji ambao walikuwa na
uhalili kabisa kutoa maoni yao na Ghadafi akakataa kuwapa angalau haki
yao hiyo?

Jee si kweli kuwa hadi kufikia kuasi na kujitenga haikuwa kwamba
utawala wa Ghadafi uliyatenga baadhi ya makabila ya nchi hiyo na watu
wake na kutoa fursa za kazi, elimu kwa misingi ya kibaguzi? Jee si
kweli kuwa chuki ya Ghadafi ni ya mkusanyiko wa ghamidha ya ndani kwa
ndani ya muda mrefu?

Hoja zimetolewa kuwa kinachotokea Libya ni chuki ya nchi za magharibi
kwa Uislamu, au kwamba suala la Libya limekuzwa kwa sababu ya nchi
hizo kugombea raslimali ya mafuta ya Libya. Hoja hizo naziwe sahihi
lakini jee si kweli pia utawala wa Ghadafi umefanya matendo
yakukirihisha dhidi ya amani na utulivu wa kidunia na ikastahamiliwa
na hata ikasamehewa kwa kufutiwa dhambi zake na hizo hizo nchi za
magharibi?

Kwa fikra zangu ni kwamba Ghadafi alikuwa amefikia ukiongoni na hakuwa
tayari kukubali hilo na si hasha alikuwa akiwaandaa wanawe Saad na
Seif al Islam washike madaraka kama ambavyo Hosni Mubarak alivyokuwa
akimuandaa mwanawe na viongozi wa aina hiyo wanavyofanya ili kulinda
maslahi yao daima dawamu.

Kwa sababu ya hofu Waafrika tuliojijengea na hofu hiyo kutiwa ndani ya
Katiba ya Umoja wa Afrika (AU) nchi moja moja ya Afrika huogopa kutoa
kauli dhidi ya nyengine. Utamaduni huu unaaanza kutuchosha na hata
kutukirihisha sisi wananchi wa nchi moja moja za Afrika.

Maana haiwi na kwangu haiingii akilini kabisa kuwa tukio kama la Libya
ambalo tayari hivi sasa limepelekea kufa watu zaidi ya 10,000 iwe ni
watu wasio na hatia au raia na nchi yangu Tanzania ikanyamaza kimya.
Haiwi na haiingii akilini kwangu kwamba Umoja wa Mataifa umepitisha
azimio la kulinda watu wa Libya na azimio hilo linatekelezwa na nchi
yangu Tanzania imenyamaza kimya.

Siafiki hata kidogo sera ya kukaa kimya na kutizama upepo utaenda
upande gani ndipo tutoe sauti yetu hasa pale jambo linalohusika ni la
haki na maisha ya raia wa Bara hili. Nataraji au ningetaraji kuwa nchi
yangu ingechukua uongozi au kama si hivyo basi angalau ingekuwa iko
mbele kutoa msimamo wake.

Kwa fikra zangu Waziri Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Serikali
kunyamaza kabisa kuhusu suala la Libya kunaleta tafsiri nyingi ambazo
sioni ulazima wa kuzitaja kwa kuwa naamini zinaeleweka, lakini pia
kuna athari kubwa katika hadhi ya Tanzania na kama nchi inayotizamwa
kuongoza Afrika.

Haiwezekani tukio kama hili linatokea Afrika, la ndege na manowari za
nchi za magharibi zimo ndani ya ardhi yetu ya Afrika kwa kilichoelezwa
kutulindia watu wetu ambao Rais na Utawala wa Libya umekuwa
ukiwahujumu, na sisi tunyamaze kimya kama hakuna kitu kinachotokea.

Hivi Membe, Wizara na Serekali hawaoni kuwa Watanzania wanataka
maelezo ili wajue nchi yao inasimama wapi? Hatuishi tena katika dunia
ya kizamani ambapo watu wetu mpaka waambiwe ndio wasikie au waonyeshwe
ndipo waone, la, dunia imebadilika sana.

Taifa madhubuti ni lile linachokua msimamo wa maslahi yake ya muda
mrefu si ya muda mfupi. Jee sisi hatuna maslahi, hatuna msimamo wetu,
hatuna misingi yetu juu ya haki na maisha ya raia? Kama tunavyo vyote
hivyo kwa nini tusisemee kuhusu Libya?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s