Dk Shein ahimiza uadilifu

Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Idd el Fitri huko katika Ukumbi wa Salama hall Bwawani mjini zanzibar,wakimskiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akisoma hutuba yake katika mkutano huo wa baraza la Idd

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza suala la uadilifu katika sehemu za kazi na kusema ndiyo kipimo cha imani ya mtu na kumfanya kuwa raia mwema.Akilihutubia baraza la Eid El Fitri katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani, alisema mfanyakazi mwaminifu hutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo kwenda kazini kwa wakati na kuondoka kazini.

Alisema uaminifu na utiifu ndio unaomfanya hata mfanyabiashara kuacha kukwepa kodi pamoja na kufanya vitendo vya rushwa.

‘Hiyo ndiyo misingi ya uadilifu kama mfanyabiashara basi hawezi kughushi bidhaa zake kwa ajili ya kukwepa kulipa kodi’alisema Shein.

Akitangaza mikakati ya serikali yake katika kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi wa Unguja na Pemba. amesema Serikali inataajiri watu wapatao 2,476 katika ajira rasmi na zisizo rasmi katika mwaka huu wa fedha kulingana na mahitaji na uwezo uliopo..

Alisema suala la ajira rasmin na isiyokuwa rasmin limepewa kipaumbele na serikali yake ikiwa ni sehemu ya kuondokana na tatizo la kazi kwa wananchi wa Unguja na Pemba licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali.

alisema serikali itashajihisha wananchi kujiunga katika vikundi vya ushirika ili waweze kunufaika na huduma za mafunzo na mikopo iliyotayarishwa.

Sheni alisema mkazo umewekwa katika kuvisaidia vikundi vya ushirika wa akinamama vya uzalishaji ili kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kujiongezea kipato na kupunguza umasikini.

Aidha alisema juhudi za kuwawezesha wakulima wa Unguja na Pemba kupiga hatua kubwa za kilimo unaendelea ikiwemo kulima kwa kutumia pembejeo ikiwemo mboleya.

‘Sote tunafahamu kwamba kilimo kinayo mchango mkubwa ikiwemo kutoa ajira kwa wananchi mbali mbali….ndiyo maana tumeamuwa kupunguza bei ya pembejeo za kilimo na huduma mbali mbali za matrekta ilikwemo kusafisha mashamba’alisema Shein.

Mapema Shein aliwapongeza wananchi mbali mbali ikiwemo wale wasiokuwa waislamu kwa kuonesha ushirikiano mzuri ikiwemo kuheshimu mfungo wa mwezi mtukufu.

Aliwataka wananchi kuendelea kutekeleza na kufanya ibada zao katika kipindi chote ili kuepuka kufanya vitendo vichafu ambavyo vitarudisha nyuma juhudi zao walizofanya ibada katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

Viongozi mbali mbali walihudhuria baraza la Idd akiwemo makamo wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharif Hamad, makamo wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi pamoja na rais mstaafu wa zanzibar awamu ya tano Amani Abeid Karume na viongozi wa vyama vya siasa, mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wastaafu na waumini kadhaa.

Baraza la Eid limefanyika baada ya waislamu wote duniani kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Katika hatua nyengine wazanzibari wametakiwa kuitunza amani na mshikaamano uliopo sasa katika serikali ya umoja wa kitaifa na kamwe wasiruhusu mtu kuichezea kwani umewaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja na kuondosha siasa za chuki na uhasama.

Hayo yalisemwa na Imamu mkuu aliyeongoza sala ya Iddi sheikh Fadhili Suleiman Soraga na kusema amani hiyo ni matokeo ya fadhila kutoka kwa Mwenyeenzi Mungu na watu wanapaswa kuishukuru.

Sheikh Soraga alikuwa akitoa hotuba katika sala ya iddi iliyofanyika hapo katika viwanja vya Maisara na kuhudhuriwa na viongozi wote wa ngazi za kitaifa akiwemo rais dk.Ali Mohamed Shein na makamu wa kwanza na wa pili, mawaziri, viongozi wastaafu na waumini mbali mbali. Hii ni mara ya kwanza kwa sala hiyo ya kitaifa kusaliwa uwanjani.

Lengo la serikali kutangaza sala ya Eid El Fitri kusaliwa uwanjani ni kutoa nafasi kwa waumini wengi kujumuika pamoja na ni hatua moja wapo ya kuendeleza umoja na mshikamano uliopo miongoni kwa wananchi wa zanzibar. Awali sala ya Eid kitaifa ilikuwa ikisaliwa msikitini wa Muembe shauri huko Rahaleo.

Sheikh Soraga alisema umoja na mshikamano uliopo sasa ni matokeo ya serikali ya umoja wa kitaifa ambayo imewaunganisha tena wananchi wa visiwani kuwa kitu kimoja na kusahau tofauti zao za kisiasa.

‘Gharama za kuvuruga amani na kuileta tena ni kubwa sana…jamani naomba umoja na mshikamano uliopo kamwe tusikubali kuubomoa.

Aidha sheikh Soraga aliwaonya viongozi wa dini wakiwemo mashekhe kuacha kuwapotosha wafuasi wa dini hiyo kwa kuingiza ushabiki na matakwa yao binafsi.

Alisema kitendo cha viongozi wa dini kuwatangazia waislamu wengine kufunguwa kwa sababu mwezi wa kimataifa umeonekana ni kinyume na sheria za nchi na hakikubaliki.

‘Ipo sheria nambari 9 ambayo inasema mtu mwenye mamlaka ya kutangaza kuandama kwa mwezi ni mufti tu’ alisema Soraga na kuongeza kwamba kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za nchi. Aidha aliwataka masheikh kuwa makini sana na kufuata maamrisho ya dini inavyosema na sio matakwa yao binafsi yanavyowaelekeza.

Alisema waislamu waliofunguwa juzi kwa kula mchana na kusali sala ya idd wajuwe wazi kwamba wamepotoshwa na masheikh wao ambao wameficha ukweli. ‘Hawa masheikh ni watu wa ajabu sana huu mwezi wameuona wapi wakati katika nchi zote za kiarabu haukuonekana….eti wanasema umeonekana Chile’ alisema Soraga.

Aliwataka viongozi wa dini kujenga tabia ya kupendana na kushirikiana katika mambo yenye kuleta tofauti,huku akisema viongozi wa kisiasa waliohitilafiana kwa muda wa miaka mingi sasa wamekuwa wamekuwa kitu kimoja.

Baadhi ya waislamu zanzibar jana walifunguwa na kusali sala ya Iddi katika viwanja mbali mbali ikiwemo Lumumba na Maisara wakisema kwamba mwezi umeandama katika nchi nyengine ikiwemo Uganda, baadhi ya nchi hizo ni mashariki ya mbali za Indonesia na Malaysia.

Advertisements

2 responses to “Dk Shein ahimiza uadilifu

  1. Na raisi muadilifu haibi kura. Vipi mnataka raia wawe waadilifu na watiifu lakini nyie hamfanyi hivyo. Munaamrisha watu kufanya mema munazisahau nafsi zenu

  2. AHSANTE USEMAYO MWIZI KUMTAKA MWENZIE ASIIBE ALIKUA YEYE AWE MFANO WA UADILIFU SERIKALI YAKE HAITOFANIKIWA KWASABABU HIO HIO……………….

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s