Raza atamba kuwa na uwezo

Mfanyabiashara maarufu na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Mohammed Raza akizungumza na waandishi wa habari

Raza atamba kuwa na uwezo wa kumaliza kero katika muungano.

Mfanyabiashara na kada wa CCM maarufu Zanzibar Mohamed Raza ametangaza kuomba kazi ya ubunge, mshauri, au, mjumbe wa tume ya marekebisho ya katiba ya Muungano kwa rais Jakaya Kikwete ili aweze kumaliza kero zote ndani ya muungano.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar Raza alisema kuwa ana uwezo wa kumaliza kero zote ndani ya mwezi mmoja mpaka miezi sita, na kutamka kwamba viongozi wote waliyotanguliwa na wa sasa wameshindwa kumaliza kero za muungano.

Alisema kuwepo kwa nafasi maoni ya katiba mpya ya muungano ni neema kubwa kwa wazanzibari, na kwamba ni fursa pekee ya Zanzibar kujikomboa kiuchumi na utamaduni ambao umekuwa ukivurugwa.

Alisema rais Kikwete akiunda tume ya kusimamia utafutaji kura ya maoni juu ya katiba ya muungano, ni lazima azingatie uwiano sawa wajumbe kutoka Zanzibar na wajumbe kutoka Tanzania bara.

Raza aliwalaumu baadhi ya viongozi na watendaji serikalini kwa kutokuwa wakweli juu ya maswali ya taifa mfano kero za muungano, na pia kuwa wezi wa mali za umma huku akimtaka rais kikwete awafukuze kazi maramoja watuhumiwa wote wa ufisadi.

“Si lazima kupata ushadihi, mtu akituhumiwa na wengi, bora kumuondosha katika serikali au chama. Namuomba rais Kikwete awe mkali na watuhumiwa,”Raza alisema.

Advertisements

8 responses to “Raza atamba kuwa na uwezo

  1. utawala wako ushapitwa na wakati huna moja hufai hata mjumbe wa nyumba kumi sembuse leo kikwete akuchaguwe raisi ukazidi kuiba mana yake nyie ndio mlochagia kuiwa zanzibar kwa kuleta vitu vibovu na kudai pesa nyingi hazina mambo yenu yote yanajulikana bora nyamaza usitiriwe

    • Wewe mbuzi RAza wacha upuuzi wako sasa unamaanisha nini, hata umefika muda unaomba uongozi kuku mmoja weee, nenda katufute unga ukauze, mmh! wewe huna hata haya nenda bata mzinga weee !
      Mimi nakushangaa tumekuwa na makongamano ya katiba huna ulicho kisema namwisho unaanza kusifu sera za chama kwa serikali 2, weeeee punda usojijua wweee kwenda hatutaki kelele za kipuuzi kama hizo WAZAZIBARI hawataki watu kama wewe wasokuwa wazalendo.

  2. Mheshimiwa Raza ni kweli kuwa msema pweke hakosei. Kero za Muungano hazitatuliwi kwa nia njema zinahitaji mamlaka ya kisheria. Muungano huu ni shida kuondosha kero zake kwa wenyewe ni kero, msingi wake ni kero, ujenzi wake ni kero na kila chake ni kero. Nafurahi kuwa akina Ali Vuai karibbuni wameitaka SMZ itoe tamko lake juu ya Muungano na pia Ali kwa kusoma ishara za wakati amekiri kuwa Muungano una kero zinahitaji kushughulikiwa. Wewe moja huwezi nudugu kuzitatua. Njia moja ya kutatua kero hizi ni kutafuta msingi wake. Katiba mpya kama ikiandikwa na watu inaweza kusaidia ingawa si dhani kwa kuwa tayari tume imepewa hadidu rejea. Strategies zako ni zipi?

  3. Raza uwezo wako ni kutengeza ugali wako tu. Chukuwa chako mamema sisi hatuutaki muungano na inshallah Mungu atatuongoza kwa hilo. Kero za muungano tutazimaliza sisi wenyewe chini ya usimamizi wa UAMSHO UKISIMAMIWA NA MWENYEWE MUUMBA WA VITU VYOTE(ALLAH) RAZA USIDANGANYE WATU SISI SI WATOTO WACHANGA AU UMETUMWA NA HAO. SISI HATUUTAKI MUUNGANO NA HUO MCHAKATO WA KATIBA SISI WAZANZIBARI TUMESHAONA KUWA HAUNA MASLAHI MEMA KWA KWETU. HIZO NI DANGANYA TOTO TU. TUNACHATAKA NI KURA YA MAONI PEKEE NDIO SULUHISHO KAMA UNA UWEZO WAMBIE HAO WENZIO SISI TUKO MAKINI NA HATURUDI NYUMA NA KWA UWEZO WA ALLAH TUTASHINDA. HATUUTAKI MUUNGANO KWA FAIDA YA WAZINZIBAR NA VIZAZI VIJAVYO. MUSITULAZIMISHE.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s