Bei ya chakula yatangazwa

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui ametangaza bei mpya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Zanzibar

BEI Mpya ya Chakula zanzibar

Katika kudhibiti Mfumko wa bei serikalini, Serikali ya Zanzibar imetangaza kuanza udhibiti wa bei za bidhaa muhimu hasa vyakula kuanzia leo (jumapili), na kuonya kuwa mfanyabiashara yoyote atakayekwenda kinyume na hilo ataadhibiwa.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui alisema katika mkutnao na waandishi wa habari kuwa bei mpya zitakazotumika kununuwa Mchele, Sukari, na Unga wa ngano, ni matokeo ya mikutano mbali mbali kati wizara yake na wafanyabiashara wanaoagizia bidhaa hizo nchini.

Alisema kuwa bei hizo ni kwa Mchele, Sukari, na Unga wa Ngano kutoka nje tu, “bidhaa zinazolimwa nchini mfano mpunga, mkulima atauuza bei atakayopanga mwenyewe. Tumetizama mchele wa gredi ya chini kwa sababu wananchi wengi ndo uweo wao.”

Mazrui alitangaza bei hizo kuwa kipolo kimoja cha mchele au Sukari, au Unga, , kilo 50 ni 52,650/=; 80,680/=; ana  51,855/= bei ya jumla, wakati bei ya rejareja ni 1,100/=; 1,660/=; ana 1,090/=. Bei hizi ni kwa ajili ya Pemba mjini tu.

Pemba vijini bei zake ni 56,150/=; 84,180/=, ana 55,355/= kwa jumla, wakati, bei ya rejareja ni 1,120; 1,680/=; na 1,110/=.

Unguja afadhali kidogo kwa bei, ambapo Mchele, Sukari, na unga wa ngano ni 49,350/=; 77,400/=; 48,560/= Zanzibar mjini, na vijini mfano Nungwi ni 50,350/= 78,400/=; 49,560/=. Na bei za rejareja mjini Zanzibar ni 1,060/=; 1,620/=; na 1,050, vijijini 1,070/=, 1,640/=; na 1,060/=. Atakaevunja kanuni hiyo atashitakiwa na kuchukuliwa hatua imeelezwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s