Futari nzuri sana hii

. Bi Mayasa kutoka Manispaa ya Singida akimuonyesha Boga Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad katika maonyesho ya nane nane Mjini Dodoma.

 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais waZanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali za mitaa nchini, zinakabiliwa na kazi kubwa ya kusimamia maendeleo ya wananchi kwa kuzingatia kuwa Watanzania walio wengi ni wakulima.

 

Maalim  Seif amesema hayo leo katika viwanja vya nane nane mjiniDodoma, alikofika kuangalia maonyesho ya wakulima, yanayokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Amesema Serikali za mitaa ndio chombo kilicho karibu zaidi na wananchi na kufahamu matatizo na kero mbali mbali zinazowakabili.

 

Akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo, waandaji wa maonyesho hayo pamoja an waandishi wa habari, Maalim Seif alisema iwapo serikali hizo zitafanya kazi zake ipasavyo na kuhakikisha kila senti  inayotolewa na serikali inatumika ipasavyo, ni wazi kuwa maendeleo ya haraka katika kilimo yatafikiwa.

 

Alisema taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini, zinaonyesha kuwepo kasoro kubwa ya upotevu wa fedha unaotokana na usimamizi mbovu wa serikali za mitaa.

 

Aliwataka watendaji katika Serikali hizo kuondokana na ufisadi katika ununuzi wa pembejeo za kilimo na kuwaomba wananchi kuwa macho dhidi ya watu wachache wanaokwamisha maendeleoyaokwa maslahi binafsi.

Maalim Seif ambae katika ziara hiyo alipata fursa ya kutembelea mabanda na taasisi mbali mbali, alishauri taasisi zinazohusika kuyatangaza yale yote yanayofanyika katika kuimarisha kilimo ili Watanzania wayajue.

 

Alisema tayari nchi imepiga hatua kubwa na maonyesho hayo yanathibitisha jinsiTanzaniailivyofanikiwa, lakini tatizo lililopo ni kuwa Watanzania hawafahamishwi juu ya yale yanayofanyika.

 

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa mafanikio yaliokwisha kupatikana katika uimarishaji wa kilimo kutafisriwa moja kwa moja kwa wakulima.

Aidha aliishauri Serikali na taasisi zinazosimamia uingizaji wa pembejeo nchini kupunguza gharama za ununuzi ili wakulima wa kawaida waweze kuzimudu.

 

Katika ziara hiyo Maalim Seif alipata fursa ya kuyatembelea mabanda na taasisi mbali mbali ikiwemo, CRDB, Manispaa ya Singida,Wizara yaMaliasili, Polisi, BoT, VETA na Wizara ya Afya, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kilimo kwanza – Tumethubutu na tumeweza na tunazidi kusonga mbele”.  Habari hii imeandikwa na Abdi Shamna

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s