mwaka 1 wa serikali ya umoja wa kitaifa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiongea katika kongamano la kumbukumbu ya siku ya umoja wa kitaifa mjini kulia ni Bi Maryam Hamdan mwenyekiti wa kongamano hilo na Rashid Omar mjumbe wa Jumuiya ya waandishi wa habari za maendeleo zanzibar (WAHAMAZA).

SERIKALI visiwani Zanzibar imsema inajiandaa muswada wa kuunda sheria ya kusimamia vita dhidi ya rushwa visiwani humo.

Hayo yalisema jana na makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad katika kongamano la kumbukumbu ya siku ya umoja wa kitaifa mjini hapa.

Maalim Seif Sharrif Hamad alisema anaamini baada ya mandalizi kukamilika, muswada huo utapelekwa katika kikao kijacho cha Baraza la Wawakilishi.

Kongamano hilo liliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mandeleo Zanzibar (WAHAMAZA) kukumbuka siku ya kutangazwa kwa matokeo ya kura ya maoni Agosti Mosi, mwaka jana yaliyofanikisha kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo.

Walioshiriki katika kongamano hilo la siku moja ni pamoja na wajumbe wa iliyokuwa kamati ya kuratibu mchakato wa kura ya maoni, wanasiasa mbali mbali, wakiwemo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na waandisahi wa habari.

Kwa sasa vita dhidi ya rushwa visiwani Zanzibar vinasimamiwa na polisi wanaofanyakazi chini ya kitengo maalum kilichoanzishwa chini ya Jeshi la Polisi huko kwa sababu kisheria, Takukuru hairuhusiwi kufanya shughuli zake Zanzibar .

Hata hivyo, akifafanua juu ya muswada ambao uko mbioni kuandaliwa, Maalim Seif alisema chini ya uongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa hakuna kiongozi atakayevumiliwa kwa vitendo vya rushwa na kwamba sheria itakayoanundwa kutokana na muswada huo itakuwa ndio silaha ya kupambana na mwenendo huo.

Maalim Seif alitoa tamko hilo baada ya mshiriki moja wa kongamano hilo , Muhammad Yussuf kulalamaika serikali ya umoja wa kitaifa imesaidia kuleta mfumo wakuvumiliana katika siasa, lakini bado haijaingia katika kupambana vitendo vya ufisadi na rushwa

“ Zanzibar hivi sasa watu wengi wana mali nyingi za kifahari, nyumba na magari, hii ni dalili ya kuwepo ufisadi na rushwa, lakini pamoja na matatizo hayo Zanzibar hakuna anti-corruption commission,” alisema Muhammad.

Alisema mbali na matatizo ya ufisadi na rushwa, serikali ya umoja wa kitaifa pia inajiendesha kwa gharama kubwa ambazo hazilingani na kiwango cha maendeleo ya uchumi wake.

Alisema wakati Waziri Mkuu wa Sweden na Katibu Mkuu wa Umoja wa Ban Ki – moon anatumia gari aina ya Volvo ambalo thamani yake ni Dola za Marekani 40,000, mawaziri na viongozi wengine wa serikali ya umoja wa kitaifa wanatumia magari aina ya Prado ambayo gharama yake ni Dola za Marekani 70,000.

“Bila Sweden , Zanzibar hakuna elimu, lakini Waziri Mkuu wake anatumia gari aina ya Volvo,” alisema.

Salim Said Salim, mshauri wa masuala ya habari alisema ukubwa wa bajeti ya safari za viongozi na huduma kwa viongozi wastaafu pamoja na kuwepo kwa mawaziri wasiokuwa na wizara maalum ni mzigo kwa serikali ya umoija wa kitaifa.

“Mawaziri wasiokuwa na wizara maalum wa nini?,” aliuliza Salim bila kutaja ukubwa wa bajeti na baraza la mawaziri, lakini katika kikao cha bajeti cha Baraza la Wawakilishi kilichomalizika juzi, Waziri wa Fedha, Omar Yusuf Mzee alisema serikali imetenga shilingi bilioni 9.7 kwa kazi hiyo.

Akichangia mjadala katika kongamano hilo , Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ali Vuai alisema kuna umuhimu wa kuwa na chombo huru cha kusimamia mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa na kuijengea mfumo ulio endelevu.

Salma Said, mmoja wa viongozi wa WAHAMAZA, alisema chama hicho kinapendekeza Agosti Mosi ya kila mwaka iwe “Siku ya Umoja wa Kitaifa, kwani ndio siku yalipotangazwa matokeo ya kura ya maoni na hatimaye kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo.

Advertisements

2 responses to “mwaka 1 wa serikali ya umoja wa kitaifa

  1. Aslam aleikum,
    Unajua mimi sielewi ni vipi lakini kutokana na kauli zake Maalim Seif kwenye kampeni aliahidi kuwa na Serikali fupi yenye mawaziri kidogo na kubana matumizi lakini chakushangaza nikama alivyosema mchangiaji Mohamed kwamba katibu mkuu wa umoja wa mataifa na waziri mkuu wa swiden ambayo ndio inayoisaidia Zanzibar kielimu wanatumia magari yenye thamani ya 40,000 doller lakini mawaziri wa Zanzibar magari yao ni 70,000 doller.
    Sasa sijui tuseme vipi au nikama ilivyo kwakua Serikali inaendeshwa na viongozi wa CCM ndio Maalim ameshindo kukemea hilo au kutoa ushauri kwa Rais Sheni au ndio kama Shein alivyo sima kuwa yeye ana washauri wawili kalin anahiyari yake kukubali au kukataa ushauri?

  2. Hongera wa-zenj, kwa kuadhimisha mwaka mmoja tangu serikali ya umoja wa kitaifa kuasisiwa. Dumisheni huo kwa masilahi ya Zanzibar na wazanzibari wote. POSTED BY MAKERESIA PAWA. Mbarali, MBEYA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s