Balozi wa Oman aagwa

Balozi Mdogo wa Oman, Majid Abdullah Al Abbaad akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad aliyefika ofisini kwake Migombani kwenda kuaga rasmi kutokana na muda wake kumalizika pembeni ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Dk Omar Dadi Shajaak

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim seif Sharif Hamad amesema kuwa ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman umeimairika sana katika kipindi cha miaka sita, kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na Balozi mdogo wa nchi hiyo hapa nchini, Majid Abdulla Al –Abbad, ambae amemaliza muda wake.

Maalim Seif amesema hayo leo ofisini kwake Migombani alipokutana na Balozi huyo anaerudi nyumbani baada ya kuitumikia nchi yake kwa kipindi cha miaka sita.

Amesema Balozi Majid alikuwa mfano mzuri wa kukuza mashirikiano kati ya nchi mbili hizi, kutokana na juhudi zake binafsi za kusukuma mbele miradi kadhaa ya kijamii na kimaendeleo, ikiwemo uimarishaji wa Chuo cha Afya Mbweni.

Alisema pia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa uliowezesha Serikali ya Oman kuliruhusu Shirika la Ndege la nchi hiyo ‘Oman Air’ kuanza tena safari zake kati ya Oman na Zanzibar, mbali na mapungufu yaliopo katika uwanja wa Ndege wa Zanzibar, hatua iliopunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la usafiri.

Alisema katika kipindi cha utumishi wake hapa nchini, Balozi Madjid alikuwa mtu wa karibu na wananchi, alieonyesha mshikamano na kushiriki katika shughuli mbali mbali za Kitaifa.

Maalim Seif alimshukuru Balozi huyo kwa kufanikisha ziara yake nchini Oman mapema mwaka huu, na kueleza imani ya Serikali ya Zanzibar juu ya utekelezaji wa masuala mbali mbali yaliokubaliwa.

Alisema Serikali ya Zanzibar, kwa msaada wa Oman, inaendelea na matayarisho ya kuandaa mkutano wa wafadhili (donors conference) utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Alimtakia maisha mema Balozi huyo na kuahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa Balozi mwengine atakaekuja kuchukua nafasi yake.
Nae Balozi Madjid alisema Serikali ya Oman itaendeleza mahusiano na mashirikiano yake na Zanzibar, ili kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumzia juu ya ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais nchini Oman, Balozi Madjid alimhakikishia kiongozi huyo, kuwa mbali na kuchelewa utekelezaji wa baadhi ya mambo yaliokubaliwa, kuna matarajiio makubwa ya kupatikana mafanikio.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s