Magendo hayakubaliki

Ras wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kamati Maalum Task Force,ambayo itasimamia zoezi zima la uchumwaji wa karafuu katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo,kisiwani Pemba leo,alipoizindua rasmi.

 

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetenga jumla ya shilingi billion 36 kwa Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) kwa ajili ya wakulima wa zao la karafuu katika msimu huu wa mavuno ya zao hilo.

Shirika la ZSTC katika kipindi cha wiki tatu zilizopita tayari limeshanunua tani 24.16 za karafuu kutoka kwa wakulima huku sshirika hilo likitumia zaidi ya millioni 288 kuwalipa wakulima wa zao hilo.

 

Wakati serikali ikijidhatiti kutenga kiasi hicho cha fedha tayari jumla ya magunia 170 yamevushwa na baadhi ya wajanja ambao huendesha biashara hiyo kwa njia za magendo idadi ambayo imeikosesha serikali na wakulima zaidi ya  shilingi millioni 200 katika kipindi kifupi cha mavuno kilichoanza mwezi huu.   

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein jana aliwataka wananchi wa kuacha tabia ya kufanya magendo na kuitia hasara serikali wakati akizungumza na wakulima na wazalishaji wa zao hilo katika ukumbi wa Kiwanda Cha Makonyo Wawi Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.

‘Nasisitiza kuwa wakulima wa karafuu kuuza karafuu zao kupitia shirika la taifa la biashara…..tutahakikisha tunaondowa urasimu wote uliokuwa ukikwamisha wakulima kuuza karafuu zao kupitia ZSTC’ alisema Dk Shein na kuongeza kwamba.

‘Nao watendaji wa ZSTC wawe waadilifu maana wapo baadhi yao sio waadilifu na pia wafanyakazi wajitahidi sana wawe na lugha nzuri maana kuna malalamiko kwamba wapo baadhi yao wanawatolea lugha mbaya wakulima …mjirekesishe’ ‘alisisitiza Dk Shein.
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepandisha bei ya karafuu kwa asilimia mia moja kutoka shilingi 5,000 hadi kufikia shilingi 10,000 huku mkulima akipata asilimia 80% ya bei ya karafuu anayouza serikalini na asilimia 20% ya serikali.

Aidha wakulima wa zao la karafuu wametakiwa kukata tamaa juu ya ubinafsishwaji wa zao hilo na badala yake wametakiwa kuongeza nguvu katika kushirikiana na serikali ya umoja wa kitaifa ili kudhibiti magendo ya karafuu nchini.

 

Dk Shein amesema serikali haina mpango kabisa wa kulibinafsisha zao la karafuu kwa kuwa uamuzi wa kubinafsisha zao hilo ni hatari kwa wananchi kutokana na kuwa hakutakuwa na udhibiti kwa wanunuzi wa zao hilo jambo ambalo litapelekea wananchi kupata shida kama ilivyotokea kwa zao la mwani ambalo wananchi wanakosa kufaidi matunda yao.

 

Akitoa mfano kwa wakulima hao alisema serikali iliamua kuwaachia wakulima kuuza mwani wao wanapotaka lakini matokeo yake kinachotokea wananchi wanakamuliwa na wanaonufaika ni wale wanunuzi na sio wakulima wenyewe.

Alisema katika zao la karafuu serikali imeamua kuweka mkazo katika kudhibiti magendo ya karafuu na kuwataka wananchi wabadilike na wafanye kazi kwa mashirikiano na kuiamini serikali yao kwani lengo ni kumsaidia mwananchi wa kawaida katika kuimarisha kilimo cha zao hilo

Alisema baraza la mapinduzi katika maamuzi yake limeona hakuna sababu ya kubinafsisha zao la karafuu kwani bado umuhimu wake kwa taifa na wakulima kwa ujumla ni mkubwa sana.
 

‘Tumekubaliana kwamba hatuna sababu za kubinafsisha zao la karafuu lakini mpango wetu mkubwa ni kulifufua zao la karafuu kwa sababu faida za zao hili ni kubwa katika uchumi wetu na mikakati yetu sasa ni kuimarisha kilimo cha zao la karafuu na kudhibiti magendo kwa hali ya juu ili kilimo hiki kitusaidie na wakulima wetu wanufaike…hatutaki kufanya kama ilivyotokea kwenye zao la mwani ambalo halimnufaishi mwananchi ..serikali imebinafsisha zao la mwani matokeo yake wananchi wanalalamika sana’ amesema Dk Shein.

 

 Alitoa tahadhari kwa wafanyabiashara wanaojishungulisha na usafirishaji wa magendo ya karafuu kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watu wote watakaojishungulisha na magendo hayo ambapo aliwataka vikosi vya ulinzi na usalama kufanya kazi zao kwa umakini pamoja na wananchi kuacha kuwafuga watu hao ambao wataisababishia hasara serikali.

Alisema haoni sababu ya wakulima kujishungulisha na biashara ya magendo ya karafuu zaidi baada ya serikali kuchukuwa maamuzi ya msingi ya kuongeza bei ya karafuu kwa asilimia mia moja ambapo bei ya karafuu hivi sasa ni shilingi 12,000 kwa kilo.
 
‘Mtu ambaye atasafirisha karafuu kwa magendo msimfiche kwa sababu huyu ni mtu mbaya lazima afichuliwe na nikuulizeni kweli hamuwajui wanaofanya magendo? Alihoji Dk Shein na wakulima kumjibu ‘tunawajua’.

Awali Dk Shein alizindua kikosi kazi cha mipango ya kuzuwia magendo, kushajiisha wakulima wa zao hilo, kuwasikiliza matatizo ya wakulima na kuchukua hatua, kusaidia serikali katika kupatikana kwa viwango vya karafuu, na kusaidia wakulima kupata mahitaji muhimu ya zao hilo ikiwemo majamvi, kamba, karabai, vibatari na vifaa nyengine.

Aidha alizinduwa msimu wa uvunaji wa zao la karafuu na na kusisitiza kwamba serikali itajitahidi kuwaelimisha wananchi waweze kuuza karafuu zao kwa shirika la taifa la biashara (ZSTC) ambalo limepewa uwezo mkubwa wa kununuwa karafuu zote za wakulima.
 
Alisema hakuna mkulima atakayekopwa karafuu zake kutoka serikalini kwa sababu shirika hilo limejiandaa vya kutosha kununuwa karafuu zote katika msimu huu.
 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s