Wajibu wa waandishi katika jamii

Picha ya pamoja na washiriki wa semina ya siku mbili ya waandishi wa habari na asasi za kiraia hoteli ya bwawani

VYOMBO vya habari vinawajibu wa kuwaunganisha wananchi Zanzibar, umuhimu wa kuwa na serikali ya Umoja wa Kitaifa, hasa baada ya wananchi hao kupita katika kipindi kigumu na cha muda mrefu cha hitilafu za maelewano zilizotokana na hali ya siasa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alieleza hayo jana lipokuwa akitoa mada kwenye warsha ya siku mbili inayoelezea nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha serikali ya Umoja wa kitaifa.

Mhadhiri huyo alisema kihistoa Zanzibar imepitia katika mkondo mrefu wa kihistoria wa kuhitilafiana kisiasa hali ambayo imezikwa na maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa baina ya vyama vya CUF na CCM.

Alifahamisha kuwa baada ya kupatikana kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo imekuwa msingi imara wa utengamano baina ya Wazanzibari hivi sasa umefika wakati wa kuzienzi na kuzitunza tunu za taifa.

Alizitaja tunu hizo ambazo haziwawekwa katika utaratibu mzuri na aadhi yao zinahitaji kufanyiwa mapotio ni pamoja na amani, umoja,, uzalendo, mashikamano, usawa, haki, muungano, uvumilivu katika dini, rangi na siasa.

Muwezeshaji huyo alisema jamii ipaswa kuelimishwa kwa undani umuhimu wa tunu hizo ambazo zina umuhimu mkubwa katika kujiletea maendeleo, na kueleza kuwa kazi hiyo inaweza kufanywa kwa usahihi na vyombo vya habari.

Kwa upande wake Rashid Omar Kombo ambaye ni Muhadhiri wa Chuo cha Habari Zanzibar, akiwasilisha mada katika warsha hiyo alisema vyombo vya habari vinawajibu wa kuitathmini hali ya utawala bora kwa kutumia viashria vilivyopo hasa wakati huu ambapo Zanzibar ina serikali ya umoja wa Kitaifa.

Alisema utawala bora unamchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya nchi yoyote sambamba na upatikanaji wa haki za msingi ambazo kila mwanadamu anatarajiwa kuzipata bila ya kuwepo mizengwe yeyote.

Wakichangia washiriki wa warsha hiyo walipendekeza uwepo uwajibikaji wa vyombo vya habari katika kutoa taarifa sahihi kwa wasikilizaji, wasomaji na watazamaji wa vyombo vyao na kutaka uweledi utumike ili kuepusha kuandika habari zinazoweza kusababisha mifarakano katika jamii.

Awali akifungua warsha hiyo waziri wa Bishara na Viwanda, Nassor Ahmed Mazrui, kwa niaba ya waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo, Abdillahi jihad Hassan, alivitaka vyombo vya habari viandike habari zao kwa misingi ya uweledi ili kuepuka kuwa msingi wa mitafaruku katika jamii.

Waziri huyo alisema umefika wakati wananchi kuelimishwa na kuzielewa tunu za taifa ikiwemo Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964, ambayo ndiyo yaliyomkomboa kila Mzanzibari.

Waziri Jihad Hassan alivitaka vyombo hivyo viandike habari zao kwa misingi ya uweledi ili kuepuka kuwa msingi wa mitafaruku katika jamii.

Warsha hiyo ya siku mbili inawashirikisha waandishi wa habari, watendaji wa vyama vya siasa pamoja na taasisi za kiraia, na imeandaliwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s