Jenereta ni mzigo kwa zeco

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Gulioni ambapo pamoja na mambo mengine alikanusha maneno ya baadhi ya wawakilishi kwamba majenereta yalionunuliwa na shirika lake kuwa mabovu

SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO), limesema genereta za umeme wa dharura
zilizonunuliwa na serikali hazifanyikazi kutokana na gharama kubwa za uendeshaji
na sio kuharibika.

Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Ali Mbarouk alieleza hayo jana alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ofisini wake Gulioni mjini Zanzibar.

Alisema tofauti na inavyodaiwa, ukweli ni kwamba genereta hizo zimeshindwa
kufanyakazi ya kuzalisha umeme kutokana na gharama za uendeshaji ambapo kwa siku
hutumia lita 8,000 kwa siku.

Alisema shirika hilo limesitiza kuzitumia katika kuzalishia umeme kwani
zinahitaji gharama kubwa ambapo kuanzi mwezi Agosti mwaka jana hadi Machi mwaka
huu jenereta hizo zimetumia kiasi cha sjilingi milioni 900.

“Ukweli ni kwamba genereta zetu zote nzima hakuna mbovu hata moja, ila tatizo ni
gharama za uzalishaji”, alisema Meneha huyo.

Alifahamisha kuwa uzalishaji wa umeme unagharama ya shilingi 394 kwa uniti moja
ikilinganishwa na bei ya shilingi 120 wanayouziliwa wateja wa Zanzibar.

Jenereta hizo 32 zilinuliwa na ili kuupunguzia mzigo waya wa umeme unaotoka
Tanzania bara ambao umechaa na hauna uwezo wa kuchukua zaidi ya megawati 40,
huku matumizi kwa kisiwa cha Unguja kikikiwa kinatumia zaidi ya megawati 55.

Akizungumzia deni la TANESCO ambapo hivi karibuni walikaririwa wakisema kuwa
wanalidai shirika hilo bilioni 50, Meneja huyo alisema shirika lake
halikubaliani na deni hilo kwani kuna utata mkubwa uliojitokeza.

“Tanesco wanatudai lakini sio deni bilioni 50, hili ni deni
lililoengezwa”,alisema Meneja huyo.

Meneja huyo alilishutumu EWURA kwa kuongeza bei ya umeme Zanzibar ambapo wateja
wamepandishiwa kwa zaidi ya asilimia 168 jambo ambalo alisema sio sahihi na
linawaumiza sana wananchi.

Advertisements

One response to “Jenereta ni mzigo kwa zeco

  1. Vipi kitu cha gharama kama hichi kinanunuliwa bila kwanza kuhakikisha uendeshaji wake na gharama
    zitazohitajika? Hata mutukari ya kwaida unapewa kwanza kuijaribu, kwanza uhakikishe umadhbuti wake
    na uwezo wake kwa ujumla na kujuwa gharama za spareparts zake na pia utumiaji wake wake wa petroli
    na pia dhamana zake. Usitie miguu yako yote miwili kutaka kukijuwa kina cha maji, ni heri kutia mguu
    mmoja na kuubagisha wapili nje ili kina kikiwa kikubwa uwe mguu uliouwacha nje ndio wa kukutoa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s