Msiiogope CUF

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi wanachama wa CUF kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar kadi za uanachama katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Bwawani ambapo alisema bado lengo la CUF kukamata khatamu za uongozi na kumtaka Dk Shein ajiweke sana ifikapo 2015

Maalim Seif awaambia wasomi wasiogope kujiunga na CUF

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad jana aliwataka wananfunzi wa vyuo vikuu visiwani Zanzibar kuondokana na tabia ya kuogopa kujiunga na chama hicho kwa hofu ya kunyimwa ajira baada ya kuhitimu masomo.

 

Alisema  tabia yao ya kuongopa kujiunga na chama hicho wakiwa bado vyuoni imesababisha  ukame wa wasomi ndani ya chama, ambao utendaji wao unahitaji kwa ajili ya kazi za utafiti wa kuboresha sera za chama.

 

Maalimu Seif alitoa wito huo baada ya kuwakadhi kadi wanachama wapya 555, wakiwa ni wanafunzi  waliojiunga na chama hicho katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu visiwani Zanzibar .

 

Alisema mazingira ya sasa visiwa humo yanapitia hatua ya mabadiliko makubwa, hivyo ni dhana potofu kwa wananfunzi wa ngazi hizo za elimu kuogopa kushiriki katika shughuli za kijamii, ikiwa ni pamoja na siasa.

 

“Mazingira yamebadilika Zanzibar , jiungeni bila hofu, iliyokuwepo awali kwa watu waliokuwa na hamu ya kushiriki katika harakati za mageuzi kwa kujiunga na upinzani, hasa CUF,” alisema Maalim Seif.

 

Alionya kuwa uoga ni ugonjwa na kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana wengine kuwa wajasiri, huku akitoa mfano kwamba Nelson Mandelea angekuwa mwoga mpaka leo, ubaguzi usingeondolewa Afrika Kusini.

 

Alisema uongozi ni sawa na mchezo wa kupokezana vijiti na kwamba vijana wakiogopa siasa wakiwa bado vyuoni na taasisi nyingne za elimu ya juu, taifa halitakuwa na wanasiasa wenye ujasiri.

 

Akiwaondoa hofu ya kunyimwa ajira kwa misingi ya kisiasa, Maalim Seif alisema  chini ya sheria mpya ya utumishi katika serikali ya umoja kitaifa, hakuana mtu atakayepewa ajira kupitia mgongo wa siasa.

 

“”Sheria mpya ya utumishi ya Zanzibar inaeleza kuwa ajira zote ni lazima zitangazwe, kila moja atapimwa na kuajiriwa kwa uwezo, sio kwa itikadi ya chama,” alisema Maalim Seif.

 

Alisema kwa sasa ajira ni haki ya kila mtu na kwamba, suala hilo hata Rais wa Zanzibar Dk  Ali Mohamed Shein juu ya suala la kila Mzanzibari kupata haki, ikiwemo ya kuajiriwa.

 

Wanafunzi 555 waliokabidhiwa kadi za uanachama wa CUF, ni pamoja na wanaosoma katika Chuo Kukuu cha Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha Chukwani,  Chuo Cha Afya Mbweni, Chuo cha Kiislam Cha Mazizini na na Chuo Cha Mtakatifu Clement.

 

Wito wa Maalim Seif kwa vijana kuondokana na tabia ya kuogopa kujiuna na CUF ilikuja baada ya viongozi wa kamati ya Jumuiya ya Vijana wa CUF wa Vyuo Vikuu na taasisi za elimu ya juu Zanzibar,  kumweleza kwamba vijana wengi wanapenda siasa vyuoni, lakini wanaogopa kukosa ajira baada ya kumaliza masomo.

 

Hata hivyo akitoa maelezo hayo, mmoja wa viongozi hao Goma Gora Khamis alisema kwa upande wake haogopi na kwamba anamaliza chuo mwaka huu na ana uhakika wa kupata kazi ya kujiajiri mwenyewe iwapo atawekewa mizengwe kwa kujikiunga na CUF.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s