Danny Mwakiteleko afariki dunia

Danny Mwakiteleko wakati wa uhai wake akipokea cheti chake ambacho bila ya shaka yoyote kilikuwa ni cheti chake cha mwisho kupokea hapa duniani na aliyebahatika kumkabidhi cheti hicho ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa Serengeti Breweries, Teddy Mapunda baada ya mkutano wa jukwaa la wahariri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kukutana kwa siku mbili wakijadiliana kuhusu 'Responsible Journalism' huko Kibo Palace Arusha.

JANA vyombo vya habari kadhaa viliripoti habari za ajali mbili mbaya za barabarani zilizotokea Dar es Salaam na Morogoro ambapo ya Dar es Salaam ilijeruhi huku ya Morogoro ikiua.

Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari Limited (NHL), Danny Mwakiteleko, alijeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea kwenye barabara ya Nelson Mandela usiku wa kuamkia juzi na kulazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).

Ajali ya Morogoro ilihusisha basi na lori la mafuta ya kula kugongana uso kwa uso na kuwaka moto ambapo watu kadhaa ambao idadi kamili hadi jana haikuwa imefahamika, walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Mwakiteleko ambaye alikiwa akiendesha gari lake saa za usiku, inasemekana alipamia tela la lori lililokuwa limeegesha barabarani, wakati lori na basi yaligongana kutokana na moshi uliotanda barabarani uliotokana na kuchomwa majani karibu na barabara.

Ajali zote hizo zilitokana na kutokuwapo hadhari barabarani ya kuonesha kuwa kuna tela limeegesha, hivyo madereva wa magari mengine wawe waangalifu, ina maana hakukuwa na kibao cha kuakisi mwanga usiku.

Morogoro moto uliowashwa barabarani ni dhahiri ulisababisha moshi uliozuia madereva kuona mbele na kujikuta wakigongana na kusababisha maafa hayo ambayo kwa mara nyingine yametupora ndugu zetu, lakini pia nguvukazi ya Taifa na wengine kuwaachia vilema.

Siku zote kelele za kuzingatia usalama barabarani zimekuwa zikipigwa, lakini bado kuna watu wanaona ni kama nyimbo na hivyo hawataki kuzifuata, mathalan Mwakiteleko, ingawa hajaweza kuzungumza, angeona alama inayomwashiria kuwapo tela mbele yake kweli angepata ajali hiyo?

Kama moto usingewashwa karibu na barabara ya Mikumi, Morogoro, madereva wa lori na basi wangegongana na kujikuta katika maafa hayo?

Bila shaka ni hapana, lakini kutokana na udhaifu huo uliopo miongoni mwa watumiaji wa barabara, hayo yametokea.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda huko nyuma alipata kuonya dhidi ya madereva wa malori mabovu kuegesha barabarani bila kuweka alama zozote na kusababisha ajali nyingi, lakini ikaonekana kama yanaingilia sikio moja na kutokea lingine.

Madereva wengi wa malori na hata wakati mwingine mabasi, hawana alama za pembetatu zinazoakisi mwanga, ambazo ni muhimu kuwekwa barabarani ili kutoa tahadhari kwa madereva wengine, kwamba kuna tatizo mbele ili nao waamue nini cha kufanya.

Sana sana wanaoona kuwapo umuhimu baadhi yao nao wamekuwa wakitumia matawi ya miti kutandaza barabarani na hata baada ya kutengeneza magari yao na kutengemaa, wamekuwa wakiyaacha hapo, wakidhani kuna watu maalumu wa kuyaondoa!

Kama hata Waziri Mkuu ameagiza na askari wa Usalama Barabarani wanalijua hilo, iweje sasa haya hayafanyiki?

Tunamtaka nani alisemee hili na hasa tukijua kuwa ni kwa usalama wetu wenyewe? Kinachotakiwa ni kila mmoja wetu kuwajibika ili kuondokana na hali hii.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s