China yamnusuru Duni kujiuzulu

Balozi Mdogo wa China Zanzibar Chen Qinman na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee, kutowa mafunzo ya Uwezesheji Viongozi Nchini China., utiaji wa saini huo umefanyika Wizara ya Fedha Vuga.

China yamnusuru Duni kujiuzulu

CHUMBA cha wagonjwa mahututi (ICU) cha Hospitali ya Rufaa ya Mnazimoja kitafanyiwa upembuzi yakinifu, chini ya mpago wa kukijenga upya utakaogharamiwa na serikali ya China.

Balozi mdogo wa nchi hiyo, huko Zanzibar, Chen Qiman amesema kazi ya upembuzi yakinifu juu ya hali ya chumba hicho, itafanyika sambamba na kazi nyingine juu ya mfumo wa huduma ya maji na umeme katika hospitali hiyo.

Alitoa ahadi hiyo baada ya serikali yake kutoa msaada kwa Zanzibar wa shilingi milioni 82.5 kwa ajili ya kugharamia mpango wa kujenga uwezo wa watendaji serikalini huko katika ofisi za wizara ya fedha Zanzibar.

Msaada huo ulikabidhiwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee na Balozi Chen mjini hapa jana.

Akifafanua juu ya ahadi ya kujenga chumba cha wagonjwa mahututi, Balozi Chen alisema lengo ni kuimarisha huduma kwa wagonjwa na kwamba mpango huo utaambatana na wa mafunzo kwa madaktari.

Balozi Chen alimueleza Waziri wa fedha kwamba China inakusudia
kuijenga upya ICU ya hospitali kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na kuwapatia madaktari
mafunzo kwa ajili ya kuiendesha, sambamba na kuleta vifaa ili iweze kufafanana
na za kimataifa.

“Tutakifanyia tathimini kwa lengo la kujua hali ya sasa ya chumba hicho, nia ni kujenga ICU mpya,” alisema Balozi Chen.

Alisema kazi ya awali ya upembuzi yakinifu wa chumba hicho na mfumo wa maji na umeme itatekelezwa na serikali yake kwa ushirikiano na Wizara ya afya na Wizara ya Fedha ya Zanzibar .

Chumba cha wagonjwa mahututi cha Hospitali ya Mnazimoja, hakina vitendea kazi kwa muda wa mwaka moja sasa, baada ya mashine tano zinazowaongoza madktari kujua mwenendo wa afya ya mgonjwa mahututi, kuharibika kabisa.

Mapema mwezi huu, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji, alitishia kujiuzulu iwapo ahadi ya kuipatia hospitali hiyo vifaa hivyo haitatekelezwa na serikali katika muda wa miezi sita kwanzia mwezi huu.

Hii ilikuwa ni baada ya kubanwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kupitisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, wakipinga hatua ya serikali kushindwa kutenga kasma kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya ICU na dawa.

Hata hivyo, wakati Balozi Chen anatoa ahadi juu ya mpango wa kuboresha huduma za Hospitali ya Mnazimoja kwa jumla, Waziri Duni hakuwepo, lakini baadaye alisema amefurahishwa na uamuzi wa serikali ya China kuisaidia Zanzibar katika suala hilo .

Alisema hata katika hatua fulani, baada ya kutishia kujiuzulu serikali alipobanwa na wawakilishi barazani, alipata fursa ya kuonana na maofisa wa ubalozi huo na wakamnong’oneza juu ya mpango wa kujenga upya kitengo hicho.

“Hata uamuzi wangu wa kujiuzulu, waliniuliza nikawaambia, I am serious – sifanyi utani, siogopi kuwa nje ya utumishi wa serikali,” alisema Duna katika mahojiano kwa njia ya simu kiganjani akiwa Chukwani nje ya baraza la wawakilishi.

Akiipongeza serikali ya China baada ya kupokea msaada huo, Waziri Omar alisema utaondoa ukosefu wa mashine za kupima mwenendo wa afya za wagonjwa, kwa sababu ujenzi upya wa chumba hicho, utakuwa ni pamoja na kukiwekea vifaa vya kisasa.

“Hali ni mbaya, hakuna duniani mtu anakwenda na mitungi ya gesi ICU,” alisema Waziri Omar baada ya waandishi wa habari kutaka ufafanuzi zaidi iwapo mpango wa kujenga upya chumba za ICU utawezesha chumba hicho kupata mashine mpya.

Waziri huyo wa Fedha alisema msaada huo ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kimafunzo watendaji wa Serikali, ambapo watakwenda nchini China kwa awamu tofauti kuanzia mwezi Augosti, Novemba na kundi la mwisho Februari mwakani.

Alieleza mafunzo hayo yatayochukuwa karibu siku tisa hadi 10 nchini China
yatawajumuisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa SMZ, Wenyeviti wa Kamati wa
Baraza la Wawakilishi, baadhi ya wakuu wa wilaya, baadhi ya watendaji wa
Halmashauri na maofisa Wadhamini.

Alifahamisha kuwa, programu za mafunzo hayo yatajumuisha mapinduzi ya uvuvi,
ambao utajumuisha mafunzo katika ufugaji wa samaki baharini, ufugaji wa chanza,
kamba, kilimo cha umwagiliaji maji, elimu na miundombinu na mawasiliano.

Nae Waziri Omar alishukuru kwa hatua hiyo Serikali ya China kutaka kuleta
wataalamu wake ili waje kufanya tathmini katika ICU na baadae kujengwa upya,
ambapo aliwataka wananchi kuwa wastahamilivu maendeleo makubwa yatafanyika
nchini katika huduma za kiafya na kukuza uchumi na kupunguza umasikini

Juu ya msaada wa shilingi milioni 82.5 wa kujenga uwezo wa watendaji serikalini, Waziri Omar alisema fedha hizo zitagharamia mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi wa SMZ, wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, watendaji wa serikali za mitaa na wenyeviti wa kamati za Baraza la Wawakilishi.

Alisema mafunzo hayo yatafanyika nchini China na kwamba washiriki watakwenda katika awamu tatu katika kipindi cha miezi mitatu, kuanzia mwezi ujao, Novemba mwaka huu na Februari mwakani na kwamba jumla ya viongozi 80 watanufaika na mafunzo hayo.

Alisema mafunzo hayo yatagusa nyanja mbali mbali za maendeleo, zikiweno za kilimo, elimu, uvuvi na sekta ya maji.

Advertisements

One response to “China yamnusuru Duni kujiuzulu

  1. Asante Bi Salma kwa nakala hii. Naona jambo lakutia moyo kuwaona akina Maalim Juma Duni kuweka presha ya hali ya juu kwa manufaa ya wananchi. Wizara yake inauzito mkubwa sana kwa jamii yetu na ikiwa hakuwa namna hii basi mambo yatalegea zaidi. Mwenyezi Mungu atamzidishia imani na mapenzi kwa wenzake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s