Wafanyabiashara wadogo wasaidiwe

Wafanyabiashara wadogo wadogo (wajasiriamali) wa Zanzibar wakiuza bidhaa zao katika maonesho ya sabasaba yaliofanyika jijini Dar es salaam

NCHI za Afrika kwa sasa zinakabiliwa na changamoto ya kutafuta njia za kuondoa urasimu unaosababisha sekta binafsi ya biashara kushindwa kuchangia juhudi ya kuongeza ajira kwa vijana.

Mtaalam mmoja katika masuala ya biashara ndogo ndogo na za kati (SME’s), Rajeev Aggarwal, alisema jana mjini hapa kuwa nchi hizo lazima zianze sasa kuelekeze juhudi katika kujengea mazingira yanayoruhusu sekta binafsi kuendesha shughuli za biashara na viwanda vya kati bila vikwazo.

Aggarwal ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (KIST), iliyopo Kigali, Rwanda alisema mazingira bora kwa maendeleo ya sekta hiyo yatapatikana kwa kuondoa urasimu katika utoaji wa leseni za biashara ndogo ndogo na kuanzisha utaratibu wa msamaha wa kodi kwa watu wanaoanzisha miradi ya viwanda vya kati.

Alisema katika mazingira ya sasa ni vugumu, kwa vijana wanaotafuta maendeleo kwa kujiajiri katika nchi nyingi, zikiwemo za Afrika mashariki, kupata leseni za vitega uchumi wanavyokusudia kuanzisha.

Aggarwal ambaye alikuwa anazungumza na maofisa wa ngazi ya juu serikalini visiwani Zanzibar , alisema vijana wanaokwamishwa na urasimu huo ni pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni sehemu kubwa ya vijana waathirika wa tatizo la ajira, barani Afrika.

Akitoa mfano, ofisa huyo alisema inasikitisha karibu katika nchi zote za Afrika Mashariki, ikiwemo Rwanda , kuona vijana wanasota kwa muda mrefu kutafuta leseni bila mafanikio. “Mtu anatumia zaidi ya miezi sita hadi mwaka kutafuta leseni na hafanikiwi.”

Alisema mbali na vikwazo katika upatikanaji wa leseni za biashara na miradi ya mingine ya viwanda vya kati, pia anashangaa kwanini nchi za Afrika hazina utaratibu wa msamaha wa kodi kwa sekta ya SME’s.

“Hakuna utaratibu wa msamaha kwa kodi kwa sekta ya SME’s barani Afrika,” alisema Aggarwal na kuwashauri wataalam wa masuala ya sera na wasomi kukaa pamoja kutafakari sababu zinazochangia Afrika kukwama kimaendeleo.

Kuhusu Zanzibar, Aggarwal alisema visiwa alisema visiwa hivyo vinaweza kuwa mfano katika maendeleo kupitia SME’s iwapo vijana watajengewa mazingira ya kuanzisha vikundi vya uzalishaji bidhaa zitokanazo na mazao ya nazi na karafuu.

“Kuna taasisi nyingi za fedha ambazo ziko tayari kugharamia maendeleo ya sekta ya SME’s, iwapo serikali itatuma watendaji wake kujifunza maendeleo ya sekta hiyo katika nchi zilizofanikiwa, ikiwemo India .

Aliongeza kuwa miongoni mwa mambo ambayo watajifunza kutoka nchi zilizofanikiwa, ni pamoja na namna ya kuweka utaratibu mzuri wa kuratibu shughuli za sekta hiyo kwa ufanisi ikiwa ni hatua ya kuwavutia vijana wengi kuwa washiriki.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Zanzibar, Mwinyihaji Makame Mwadini alisema njia ya kuondokana na urasimu katika kusimamia shughuli za SME’s ni kujifunzo kutoka nchi zilizofanikiwa katika uendeshaji wa sekta hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s