Marekani yafurahishwa na vijana znz

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso wakati alipofika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Ferej ofisini kwake Migombani na baadae kutembelea sober house ya mwanzo iliyoko Tomondo iliyoanzishwa 13/01/2009.

MAREKANI imefurahishwa na dhamira ya vijana kujiunga na vituo vya huduma kwa vijana walioachana na madawa ya kulevya visiwani Zanzibar na kusema hatua hiyo ni mafanikio ya vita dhidi ya biashara ya madawa hayo.

Msimamo huo ulionyeshwa jana na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt alipotembelea kituo cha Tomondo Sober House, kinachotoa huduma kwa vijana walioachana na utumiaji wa madawa ya kulevya katika eneo la Tomondo, mjini hapa.

“Uamuzi wenu wa kijiunga na vituo hivi, ni njia sahihi zaidi katika vita vya kupambana na bishara ya madawa ya kulevya duniani, kwa sababu hatimaye bishara hiyo itakosa soko,” alisema Balozi Lenhardt.

Aliambiwa kuwa zaidi ya vijana 300 walioachana na tabia ya kutumia madawa ya kulevya wamepitia katika kituo cha Tomondo Sober House na kupatiwa huduma mbali mbali na kwamba asilimia 30 kati ya hao sio mateja tena baada ya kurejea katika maisha ya kawaida.

Tomondo Sober Haouse ni miongoni mwa vituo vitano vinavyotoa huduma ya aina mbali mbali ikiwemo elimu kwa vijana waliachana na madawa ya kulevya katika visiwa wa vya Unguja na Pemba .

Akifafanua msimamo wa Marekani katika vita dhidi ya biashara ya kulevya Balozi Lenhardt alisema nchi yake inaamini kuwa njia sahihi ya kufanikisha vita hiyo ni kuua soko la madawa ya kulevya kwa watumiaji kuachana na tabia hiyo.

“Tunahitaji vijana zaidi kama ninyi, wanaume na wanawake kujitokeza kuachana na madawa ya kulevya, sisi kama nchi tutasaidia kuwaelimisha wasitumie madawa, na wauzaji pia wataacha kuleta madawa Zanzibar ,” alisema Balozi Lenhardt.

Alisema ingwa uamuzi wa kuachana na madawa ya kulevya ni mgumu, lakini kwa dhamira inawezekana na kutoa mfano wa kaka yake kwamba alifanikiwa kuachana na tabia hiyo baada ya kutumia madawa ya kulevya kwa zaidi miaka 35 na sasa sio mwathirika tena.

Alisema anaamini inawezekana kwa vijana wengi zaidi Zanzibar kuachana na tabia hiyo kwa sababu: “Mnajua namna kulinda maisha yenu, lakini madawa ya kulevya hayana uwezo wa kukulazimisheni kuyatumia ikiwa mumeamua kuacha.”

Mapema Balozi lenhardt alikuwa na mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Zanzibar , Fatma Abdulhabib Fereji huko Migombani nje kidogo kutoka mjini hapa.

Katika mazungumzo yake na Balozi Lenhardt, Waziri Fatma alisema serikali inakusudia kujenga kituo kikubwa katika eneo la Tunguu ili kuondoa msongamano wa vijana wanaoachana na madawa ya kulevya katika vituo vinavyoendesha shughuli katika majengo ya kukodi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s