Vijana kujadili malaria

balozi wa Uingereza nchini Tanzania

 Mkutano wa Vijana juu ya Malaria kufanyika Dar es Salaam

19July 2011

 Taasisi ya Jumuiya ya Madola (Royal Commonwealth Society – RCS) itafanya Mkutano wa Vijana juu ya Malaria jijini Dar es Salaam kesho Jumatano, 20 Julai, 2011.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa British Council na kuhudhuriwa na wanafunzi kutoka shule 30 tofauti. Tukiohilolitajumuisha mjadala wa wazi utakaowakutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali yanayojishughulisha na mapambano dhidi ya Malaria nchiniTanzania, semina shirikishi kwa wanafunzi kupitia simulizi za hadithi ili kuhamasisha kampeni dhidi ya malaria kwa watoto wadogo, pamoja na onyesho la filamu yaTanzaniailiyochaguliwa, iitwayo Chumo. 

Mkutano huo umefadhiliwa na Ubalozi wa Uingereza, Idara ya Misaada ya Uingereza (DFID) pamoja na programu ya Wizara ya Afya NATNETS, Malaria No More, COMMIT na READ International.

Mkutano huo ni sehemu ya mradi wa “Me and My Net”, ambao ni shindano la kiubunifu linalowapa fursa vijana chini ya miaka 18 kutoa maoni yao juu ya changamoto za malaria duniani. “Me and My Net” inafadhiliwa na neti za Olyset za Sumitomo Chemical’s. Tembelea tovuti hii: www.meandmy.net kwa maelezo zaidi juu ya mradi huo.

Muhtasari kwa Mhariri:

 

Mkutano wa Vijana juu ya Malaria utafanyika katika ukumbi wa British Council, makutano ya mtaa wa Samora na Ohio, Dar es Salaam.

 

Waandishi wa habari wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo kuanzia saa 9:30 alasiri Jumatano tarehe 20 Julai. Tafadhari wasiliana na elaine.crisp@thercs.orgkama utahitaji kuhudhuria.

Me and My Net

“Me and My Net” ni shindano linaloratibiwa na The Royal Commonwealth Society na kudhaminiwa na Olyset Net. Shindano hilohuwapa watoto chini ya miaka 18 fursa ya kutoa mawazo yaojuu ya changamoto za malaria duniani. Kwa takwimu za maambukizi hadi kufikia watu milioni 500 kila mwaka, na pia kusababisha mamilioni ya vifo, tunaamini kwamba vijana wanaweza na hawanabudi kutoa tamko juu ya suala hili muhimu. Kuanzia Aprili hadi Septemba mwaka huu, watoto chini ya miaka 18 wanaweza kuwasilisha insha, mchoro, filamu au picha yenye maudhui ya neti za kuzuia mbu katika kinyang’anyiro kitakachowawezesha kujishindia zawadi hadi 100 – ikiwemo safari ya wiki moja jijini London. Kwa mawasiliano zaidi tembelea www.meandmy.net.

Taasisi ya Jumuiya ya Madola (RCS)

RCS ni asasi ya kiraia kubwa zaidi na kongwe inayofanya kazi kwa ustawi wa Jumuiya ya Madola. Ilizaliwa mwaka 1868, na inafanya na kusimamia matukio mbalimbali yanayolenga kukuza maelewano kati ya mataifa. Programu zake za elimu, vijana na kiutamaduni zinajumuisha mashindano ya uandishi wa insha mashuleni ya kihistoria na makubwa zaidi duniani pamoja na programu ya kimataifa ya uongozi kwa vijana. Ikiwa na makao yake makuu katika klabu ya Jumuiya ya Madola jijini London, RCS ina wajumbe wa kimataifa takribani 10,000 kupitia mtandao wa matawi. RCS imesajiliwa kama taasisi ya kiraia nchini Uingereza na Wales. (226748). thercs.org

Neti za Olyset

Neti za Olyset zinashikilia tuzo ya Sumitomo na ni nyenzo imara iliyothibitika kupambana na malaria. Neti ya Olyset huzuia mbu aina ya Anopheles kuwang’ata binadamu, na hivyo kupunguza kuenea kwa malaria. Anopheles ni aina ya mbu anayesambaza vijidudu vya malaria kutoka kwa mtu mmoja aliye na vimelea hivyo hadi mwingine kupitia damu. Neti za Olyset zinatengenezwa hapaTanzaniakwa ushirikiano baina ya Sumitomo Chemical na kiwanda cha A-Z Textiles kilichopo mkoani Arusha.

Neti za Olyset zina ‘kiuwa wadudu’, ambacho ni dawa inayotumika kuua wadudu wanaoweza kumdhuru binadamu. Neti hizi huimiri kutochanika na kufubaa, hivyo kuzifanya kudumu zaidi na endapo zitatunzwa vizuri, zinaweza kudumu hadi kwa muda wa miaka mitano. Neti za Olyset haziitaji kuongezewa tena kiuwa wadudu.

Kwa mawasiliano

Wasiliana na Jessica Smithwa The Royal Commonwealth Society: jessica.smith@thercs.org / +44 (0) 20 7766 9205

Mark Polatajko | Mkuu wa Idara ya Siasa, Habari na Miradi | Barua Pepe: mark.Polatajko@fco.gov.uk  | Tel: +255 (0) 22 2290000 | Mob: 0754 764276 |

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s