Grand Malt watoa vifaa vya michezo

Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt Consolata Adam akitowa maelezo ya Kampuni yake kuhusu vifaa vya michezo kwa timu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa timu hiyo.

TIMU ya soka ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imefanikiwa kupata mdhamini katika bonanza linalotarajiwa kufanyika Septemba 8 mwaka huu huko Mkoani Arusha.Watunga sheria hao wa Zanzibar wamepata udhamini huo kutoka kwa watengenezaji wa kinywaji baridi cha Grand Malt ambapo kampuni hiyo ilikabidhi vifanaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.

Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa kinywaji hicho Consolata Adam, huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani visiwani Zanzibar,amesema kuwa wamefurahishwa sana kupata nafasi ya kuidhamini timu hiyo ingawa udhamini huo umekuja kwa haraka haraka.

Consolata amesema kuwa ni matumaini kuwa bonanza hilo litatoa burudani ya kutosha kwa wale wote watakaohudhuria shughuli hiyo,lakini pia kwa wazee wanaotoka kenye kazi nzito ya kuwakilisha bajeti.

Udhamini huo ambao umetokana na vifaa vya michezo ambavyo ni viatu,soksi,jezi, na track sut vilikabidhiwa kwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Abdilah Jihad Hassan

“Kampuni ya kinywaji baridi ya Grand Malt,imefurahi sana kupata nafasi ya kuidhamini timu hii na tunatarajia kwamba bonanza hilo litatoa burudani kwa wataofika,”alisema.

Nae Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo,Abdilah Jihad Hassan,ameishukuru kampuni hiyo kutokana na kuona umuhimu wa kuisaidia timu hiyo.

Alisema kuwa msaada walioutoa wanauthamini kwa wali na mali na kuutaka uongozi wa kampuni hiyo uwe unatoa mashirikiano ya mara kwa mara katika kusaidia nyanja mbali mbali za kijamii visiwani humu.

“Natoa shukurani zangu za dhati kwa Garand Malt kutokana na msaada wenu mlioutoa kwetu,hivyo naomba mara hii isiwe mwisho kwenu bali muwe mnaendelea kutusaidia katika nyajnja mbali mbali,”alifahamisha Jihad.

Nae Katibu wa Wawakilishi Sports Club,Haji Omar Kheir amesema kuwa msaada walioupata watautumia kama ilivyokusudiwa kutokana na hivi sasa wapo katika mazoezi makali ya kujifua kushiriki katika bonanza hilo.

Kheir alifahamisha kwamba huu ni mwanzo na timu hiyo inatarajia kuwa na Grand Malt bega kwa bega kila wakati kwa ajili ya kusaidia timu hiyo.

Viongozi mbali mbali wakiwemo Wawakilishi,Mawaziri na Manaibu Mawaziri walishiriki katikahafla hiyo ya ukabidhiwaji wa vifaa hivyo vya michezo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s