tuwe makini katika ibada

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akifungua mkutano wa tatu wa Baraza la Afrika elimu masafa katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam

 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amezitaka taasisi za dini nchini, kuendeleza kazi ya kuinganisha na kuielimisha jamii juu ya haja ya kujenga tabia njema, maadili na uadilifu.

Maalim Seif ametoa changamoto hiyo jana huko Ole Kianga, Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ufunguzi wa Ijitmai ya kimataifa inayowashirikisha waislamu kutoka Mataifa mbali mbali ya Afrika Mashariki na Kati na Mikoa kadhaa ya Tanzania Bara.

Ijitimai hiyo itakayodumu kwa kipindi cha siku tatu, ina lengo la kuwakumbusha na kuwaamrisha waislamu mambo ya heri, pamoja na kuwakatazana maovu,sambamba na kupata fursa ya kufahamiana ili kuongeza mshikamano wao.

Amesema wakati huu nchi ikiwa imekabiliwa na changamoto ya kuporomoka kwa maadili, ni muhimu kwa taasisi hizo kuuelimisha umma haja ya kurejesha maadili mema na kujenga uadilifu ikiwa njia moja wapo ya kupiga vita maovu.

Alisema kazi ilioanza kuonyeshwa na taasisi hizo, hasa wakati ule nchi ilipokumbwa na mifarakano iliotokana na sababu za kisiasa ni ya kupongezwa, na inayohitaji kuendelezwa kwa faida ya kizazi kijacho.Aidha alizipongeza taasisi hizo kwa kuchangia maendeleo ya nchi kuchumi na kijamii, sambamba na hatua za kuanzishwa Vyuo vikuu, ujenzi wa shule, hospitali an vituo vya Afya.

Katika hatua nyingine Maalim Seif alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waumini wa dini ya kiislamu umuhimu wa kukabiliana na majanga mbali mbali yanayolikabili Taifa hivi sasa, ikiwemo maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwi, madawa ya kulevya na uharibifu wa mazingira.Alisema ukimwi ni ugonjwa unaoiathiri sana jamii, kiasi ambacho hakuna familia ambayo haijaguswa na athari za maradhi hayo.

Alisema sababu kubwa ya kuongezeka kwa mamabukizo mapya ni kutokana na kuporomoka kwa maadili, huku suala la zinaa likichukua nafasi kubwa kama chanzo kikuu cha ugonjwa huo.Aidha alisema wakati waislamu wamezungukwa na nuru kubwa kutoka kila pembe ya maisha yao, kuna baadhi ya watu wanaowapeleka gizani kwa kujishughulisha na biashara au matumizi ya madawa ya kulevya.

Alisema vita dhidi ya madawa ya kulevya sio lelemama kwa kuzingatia kuwa wale wanaofanya biashara hiyo ni watu wenye fedha nyingi,wajanja na wasiokamatika kirahisi.

Aliwataka Masheikh, Maulamaa na waumini wote wa dini hiyo kuielimisha jamii ili iachane na matumizi ya madawa hayo na kuanisha kuwa ikifika mahala pakiwa hakuna mtumiaji basi itakuwa ndio mwisho wa biashara hiyo.
Aidha Maalim Seif aliitaka jamii ya Wazanzibari kukabiliana vilivyo na changamoto ya uharibifu wa mazingira, unaotokana na shughuli na maendeleo ya kila siku ya binadamuza, ikiwemo ukataji miti, uchimbaji mchanga na ukataji wa miamba kwa ajili ya matofali.

Aliwataka waislamu kufuata mafunzo yalioletwa na Mtume Muhammad katika uhifadhi wa mazingira, akinukuu aya ya Quraan inayosema “Ikikufikia baragumu la kiyama limepigwa na ukiwa na mche wa Mtende mkononi mwako, basi upande kwanza.”

Vile vile aliwaomba waislamu kujiunga na Jumuiya ya wachangia Damu kwa hiari, ili kunusuru maisha ya bianaadamu pale wanapokutwa na maradhi au majanga mbali mbali.
Aliwataka waumini walioshiriki katika Ijitmai hiyo kuweka azma ya kuyatumia ipasavyo mafunzo watakayoyapata na kuyatumia kama maandalizi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani, sambamba na ibada ya Hijja.

Advertisements

One response to “tuwe makini katika ibada

  1. Maneno ni yakusisimua yaliyojaa hekima. Tunaomba duwa Unguja ineemeke chini ya uongozi wa busara
    wa Maalim. Neema na amani ya visiwa ambavyo vilitoweka Inshalla tuishuhudie tena. Yaa Rabi Amin

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s