Elimu iimarishwe

Wanazuoni na wasomi kutoka nchi mbali mbali za Afrika walisohiriki katika mkutano huo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr. Ali Mohammed Shein, amezitaka nchi za Afrika kutambua umuhimu wa dhana ya elimu masafa kama kichocheo cha kukuza uchumi wa nchi zao na kuimarisha kasi ya maendeleo.

Dr. Shein amesema hayo leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakati alipofunga mkutano wa tatu wa Baraza la Afrika la Elimu masafa(African Council for Distance Education), ambao uliwashirikisha wanazuoni mbali mbali kutoka kila pembe ya Bara la Afrika, wakiwemo baadhi ya wanafunzi kutoka katika Vyuo vikuu huria nchini.

Katika hafla hiyo, hotuba ya Dr. Shein ilisomwa kwa niaba yake an Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.Amesema mbali na matatizo ya fedha yanayozikabili nchi za Bara hilo, kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo, kuna umuhimu wa kufanya juhudi ili kuwa na bajeti itakayotoa msukumo wa kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuweza kujisomea.

Alizitaka nchi hizo kutafsiri kwa vitendo dhana hiyo na kuwaelimisha wananchi wake ili waweze kutumia kikamilifu uwepo wa fursa hizo.
Alisema elimu masafa ni moja kati ya njia muhimu inayowawezesha wananchi wengi kujiendeleza kimasomo na kufikia viwango vya juu kabisa.

Alieleza kuwa ni vigumu kwa nchi hizo kuweza kupata maendeleo ya kweli bila ya watu wake kuelimika, na kuzitaja baadhi ya nchi ikiwemo Malaysia, China na India kuwa ziimefikia maendeleo makubwa baada ya wananchi wake walio wengi kuelimika.

Dr. Shein alitumia fursa hiyo kuitaka Tanzania kujenga mazingira bora kwa wananchi wake, ili waweze kutumia fursa hizo ipasavyo, kwa kuzingatia kuwa huu ni wakati wa Utandawazi ambapo matumizi ya IT yamechukuia nafasi kubwa.

Aidha alisema changamoto kubwa inayozikabili nchi za Bara la Afrika ni mkanganyiko wa matatizo mbali mbali, huku rasilimali zilizopo zikiwa haziwezi kukidhi utatuzi wa matatizo yaliopo.

Alisema suluhisho la kudumu la matatizo hayo ni kwa kila nchi kukuza uchumi wake pamoja na kuwaomba washirika wa maendeleo kuelewa vipaumbele vilivyoainishwa katika nchi hizo na kutoa misaada yao moja kwa moja badala ya wao (wahisani) kuchagua miradi ya kusaidia.

Katika hatua nyingine Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, maalim Seif Sharif Hamad, alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari na kuzungumzia dhana ya kujivua gamba kwa aliekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi na kusema Watanzania walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua nini kitatokea, baada ya kauli ya Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kutaka viongozi wa chama hicho kujivua gamba.

Hata hivyo Maalim alisema ni vigumu kuelewa kiusahihi nini kilichojiri au kama kulikuwepo na shinikizo hadi Mbunge huyo akaamua kujivua gamba, mbali na taarifa tofauti zinazozungumzwa, na kumalizia kwa kusema “CCM wenyewe ndio wanaojua, huo ni mfano, wacha tutizame mingine ijayao”.

Akigusia mijadala inavyoendelea katika vikao vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Malim Seif alisema hali ni mbaya na haitoi taswira nzuri kwa taifa, huku Bunge hilo likionekana kama kwamba halina sheria au kanuni.

Alisema yale yanayojitokeza katika mijadala hiyo hayaendani na maadili ya Watanzania, na kuanisha kuwa wabunge hao walichaguliwa na wananchi kwendwa kuwatetea na kutoa hoja nzito na zenye mantiki.

Alisema hakuna ulazima wa wabunge hao kutukanana, kila mmoja ana fursa ya kutoa hoja bila ya kumtukana mwenzake.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s