Udhamini wa bia haukubaliki

Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Utalii na Michezo,Bihindi Hamad Khamis

SMZ YAPATA KIGUGUMIZI UDHAMINI WA POMBE

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar bado imekumbwa na kigugumizi kikubwa juu ya kuruhusu udhamini wa makampuni ya bia kuja kusaidia michezo ikiwemo mpira wa miguu visiwani Zanzibar.Akijibu maswali la wajumbe wa baraza la wawakilishi Naibu Waziri Habari, Utamduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis alisema kwa kifupi sana kwamba serikali imesikia maoni ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya suala hilo la kuruhusi wadhamini wa pombe lakini ushauri huo umeuchukua na serikali itaufanyia kazi.

Awali Mwakilishi Jimbo la Rahaleo (CCM) Nassor Salim Ali alitaka kujua ni lini serikali itaondosha marufuku ya udhamini wa michezo wa makampuni ya bia kwa kuwa makampuni hayo hayamiliki pombe pekee bali haa vinywaji vyengine vibaridi ikiwemo malta .

“Mheshimiwa Spika ni kwa nini serikali haifikirii kuyaruhusu makampuni ya bia Tanzania kuja kudhamini michezo yetu wakati makampuni haya hayazalishi bia peke yake huwa wana vinywaji vyengine ambavyo sio pombe mfano kama malta na vinywaji vyengine ” alihoji mwakilishi huyo.

Suala la udhamini wa makampuni ya bia katika michezo limekuwa likijirudia kila mara ambapo baadhi ya wawakilishi wakiishauri serikali kuondosha marufuku hiyo ambayo haipo kisheria kwa kuwa michezo imekuwa ikidorora sana kwa kukosa wafadhili.

Hata hivyo serikali imekuwa ikijibu kwamba michezo inaweza kudhaminiwa na makampuni mengine yasiokuwa na biashara ya pombe kama vile simu za mikononi kama zantel ambayo imeshawahi kudhamini mipira wa miguu hapa zanzibar.

Aidha Mwakilishi huyo alihoji ni lini serikali itaona haja ya kuhamisha mchezo mchezo pete ambao huchezwa na idadi kubwa ya wanawake ambapo imekuwa ukileta usumbufu mkubwa kutokana na mchezo huo kuchezwa katika eneo la kiwanja cha Gymkhana ambapo huleta usumbufu kwa wananchi kwani kipo sehemu ya kuendesha biashara ya ulevi.

Mwakilishi huyo aliungwa mkono na baadhi ya wajumbe wengine wa baraza la wawakilishi ambao wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuondosha mchezo wa mpira wa pete katika eneo la Gymkhana ambalo hutumiwa kwa starehe ikiwemo vilabu vya uuzwaji wa pombe.

Naibu Waziri wa wizara hiyo Bihindi alikiri kuwepo kwa usumbufu kwani sehemu iliopo kiwanja hicho ni maarufu kwa biashara ya pombe hapo Gymkkana na hivyo haileti sura nzuri kwa utamaduni wa wananchi wa Zanzibar lakini alisema suala hilo litafikiriwa na kuamuliwa baadae.

“Mheshimiwa spika ni kweli kiwanja kile kipo katika eneo ambalo linaendesha biashara ya ulevi…..ni tatizo kubwa kwani ni kinyume na utamaduni na silka za wananchi wa visiwa hivi lakini suala hili tumelichukua na tutalifanyia kazi”alisema Bihindi.

Alisema Serikali inafanya juhudi za kutafuta eneo jengine la kujenga kiwanja cha mchezo wa mpira wa pete ili kuona unaondoka katika eneo hilo .

Bihindi alisema wananchi wengi ikiwemo vijana hufika katika eneo lile kwa ajili ya kuangalia mchezo huo lakini pia wakati ule ule hufanyika biashara ya ulevi

Kiwanja kikubwa cha mchezo wa mpira wa pete ambacho hufanyika michezo mbali mbali ya kimataifa kipo Gymkhana eneo Maisara Mjini Unguja ambalo ni maarufu na ni la muda mrefu katika uuzaji wa pombe.

Serikali ya Mapinduziya Zanzibar hadi sasa imepiga marufuku matangazo ya pombe pamoja na ufadhili wake katika vilabu vya soka vya hapa ikiwemo katika viwanja vya michezo kwa madai kwamba kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya wananchi wa Zanzibar .

Advertisements

3 responses to “Udhamini wa bia haukubaliki

  1. Asla,m aleikum,
    Mimi nafikiri huyu Nassor na hawa wawakilishi wengine wamechanganyikiwa kwani makampuni ya pombe yakisaidia michezo ndio Wazanzibar wataondokewa na umasikini? kule bara kuna matangazo kibao ya pombe na ndio unasikini unazidi.
    M/mungu kakataza pombe na Mtume S..A.W kasema zaidi ya watu saba 7 M/mungu anawalaa ni kutokana na pombe leo anatokea mtu anajita muislam na kuishawishi Serikali iruhusu matanzazo ya pombe kwa nini M/mungu kampa uwakilishi. M/mungu kawalani na ataendelea kuwalani watu kama hawa mpaka kiama.

  2. Mimi nadhani huyu Bwana Nassor alitakiwa kuweka wazi kwamba hayo anayoyaongea ni maoni binafsi, hajatumwa na wananchi anaowawakilisha, amekurupuka, anapaswa awaombe radhi watu anaowawakilisha vinginevyo watafute namna ya kumfukuza haraka. Huyu akipewa nafasi ya kiutendaji ambapo hatumsikii mawazo yake basi atatenda kutokana na anvyojisikia na ni hatari.

  3. Namimi bidhaa zangu ziko sokoni kutoka Holland ninataka kulidhamini Baraza la wawakilishi wanitangazie biashara zangu ndio njia mbadala na ni sehemu ambayo jamii ya kizanzibar itapaangalia….sijui kama sitopingwa….Usidhani pombe…..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s